Viongozi wa Afrika : Mohamed Siad Barre

wehoodie

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
991
1,000
BARRE.jpg
Mohamed Siad Barre, au Maxamed Siyaad Barre (amezaliwa 1919. huko Ganane , Somaliland - alikufa Januari 2, 1995 , Lagos, Nigeria) , huyu ni rais wa Somalia ambae alikuwa kiongozi wakidikteta baada ya kufanya mapinduzi ya kijeshi mnamo Oktoba 1969 dhidi ya serikali ya kuchaguliwa, aliongoza kutoka 1969 mpaka Januari 1991, wakati alipong'olewa madarakani katika vita vya umwagaji damu .

Siad alizaliwa 1919 katika familia ya wafugaji kutoka kabila dogo la Marehan ukoo wa Daarood - ukoo toka Italian Somaliland. Alijiunga na jeshi la polisi Somalia baada ya Uingereza kuchukua udhibiti wa Somalia mwaka 1941, alipanda vyeo mpaka kufikia nafasi ya mkaguzi mkuu (Chief Inspector) . Wakati Somalia ikirejeshwa katika miliki ya Uitaliano mwaka 1950, Siad alipelekwa kujifunza masuala ya kijeshi nchini Italia.

Siad alihamia jeshini baada ya jeshi la taifa la Somalia kuundwa (1960), na mwaka 1966 alifikia cheo cha Meja Jenerali na baadae kuwa kamanda mkuu . Baada ya kushika hatamu Oktoba 22 , 1969, Siad alijipa cheo cha mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi na kuanzisha utawala mkali wa itikadi rasmi ya kijamaa " Scientific Socialism. "

Alitengeneza mahusiano na Umoja wa Kisovyeti, na pia kupiga marufuku rasmi tawala za kikoo ( ingawa aliendelea kutumia wazee wa ukoo kutwala maeneo ya vijijini ). Alikuza elimu na alianzisha matumizi ya alfabeti za Kirumi .

Baadaye alivunja mahusiano na Soviets na kuanza kupokea misaada ya Marekani , lakini madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu yalimfanya kuchukiwa na jamii ya kimataifa. Mwaka 1990 mapigano miongoni mwa koo na kati ya wanamgambo na serikali ilamlazimisha Siad kutoa ahadi za mageuzi, ikiwa ni pamoja na uchaguzi huru.

aYDID.png
Mohammad Farah Aydid, maarufu kama Simba wa Afrika huko somalia.

Siad alipinduliwa katika uongozi Januari 1991 na jenerali Muhammad Farah Aydid (maarufu kwa kuwashinda wamarekani katika vita ya mwaka 1992) na mwaka 1992 alikwenda uhamishoni nchini Nigeria ambapo aliishi mpaka kifo chake mwaka 1995.

Toka kupinduliwa kwa Barre Somalia haijapata kuwa na serikali kamili.

nukuu kutoka mitandao mbali mbali.
 

tansoma

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
1,186
2,000
somalia mwanzo ikikua nzuri sana kiuchumi
Tatizo kubwa la huyu bwana alidanganywa na kabila lake darood na kuwafanya vinara ktk kila sector

Walifanya kosa kubwa piaa kuwaua sa isaq ambao waliamua kujitenga na sasa ni 22 miaka wanaishi kwa amani

Damu ya isaq ipo mikonononi mwa siad
 

East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,761
1,195
Toka kupinduliwa kwa Barre Somalia haijapata kuwa na serikali kamili.

Barre alikuwa mchawi mno.Na somalia ina wachawi kila kona.Aliimudu kutawala somalia kwa kutumia uchawi.Tatizo lilitokea pale mganga wake mzee Diric Burhaan alipofariki.Akawa nguvu hana.Akapinduliwa.Akaenda Nigeria kuwaomba waganga wamsaidie lakini tatizo la wanigeria ni kuwa hawana waganga wa mambo ya utawala hivyo hakufanikiwa kurudi uraisi hadi alipofariki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom