Viongozi tumieni mitandao ili kufikisha ujumbe wenu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
3,245
4,402
Habari waungwana,

Tanzania ya sasa imekuwa ngumu sana kuita press conference kwa mtu ambae anaeonekana yupo tofauti kidogo na serikali mfano mzuri jana mh Nape alizuiliwa kufanya mkutano lakini ujumbe aliufikisha kwa wanahabari lakini kwanini iwe hivi?

Leo katibu wa CCM komredi Kinana alikuwa anataka kuita mkutano lakini pia umestopishwa hivi kwanini tumefikia huku?

Ina maana now Tanzania mikutano imesitishwa mpaka watakapoamua wao? Basi tunaomba viongozi kwa sasa tumieni social network kutoa ujumbe wenu sio lazima mikutano ila kwa kutumia mitandao itatufika tena haraka zaidi.

[HASHTAG]#mungu[/HASHTAG] ibariki Tanzania [HASHTAG]#mungu[/HASHTAG] ibariki Dar es Salaam
ef394729dc749592b6a67527b8d8bf5d.jpg
 
Hivi, kama ingetokea mmoja wa wale waliokuwa wanamzongazonga Nape akamsukuma mwenye bastola akajikuta ameshaminya trigger ikatoka risasi ikamuu Nape ingekuwaje? Tena ni kwa nini kumzuia Nape kuzungumza, kwani huyu mtu wa usalama alijua Nape angesema nini? Hivi dunia na sisi Watanzania tutaelewaje hili? Mtu aliyekuwa waziri, anakipenda chama chake na alizunguka nchi nzima kuhamasisha uhai wa chama, akahusishwa sana na chama chake kupata ushindi, leo anashikiwa bastola usoni mbele ya waandishi wa habari zaidi ya mia mbili saa chache tu baada ya kuondolewa kwenye uwaziri? Ingekuwa ni sisi watu wa kawaida ambao hatuna cheo chochote cha kisiasa ingekuwaje? Ee Mungu utunusuru na huu mwelekeo mbaya.
 
Back
Top Bottom