Viongozi hawawezi leta Maendeleo - Mkapa

Dear Mkapa!
Nlikusikilza kwa ufupi kwenye hotuba yako ulotoa majuzi kule Songea kwakti wa sherehe za kumpongeza Askofu wa jimbo hilo. Msimamo wangu, huenda ndiyo msimamo wa wengine katika forum hii ni kwamba:-
1. Maendeleo ya nchi yeyote huletwa na Serikali kwa kuwatafutia raia wake Masoko na vyanzo vya mitaji
2. Kuwajengea/kuwatengenezea miundombinu yenye kurahisisha uzalishaji wao
3. Kulinda mali zao walizojikusanyia ndani na nje ya nchi.
4. ..............
5. ............
mwenye hoja 4,5,6,e.t.c za kumpinga mzee Ben tafadhali ongezea!!

Ninakemea kwa NGUVU zote aina hiyo ya lugha uliyoitoa kwani ni UPOTOSHAJI WA MAKSUDI wenye lengo la kuwafanya raia wa nchi hii waendelee kuwa watumwa ndani ya nchi yao!!
NAWASILISHA!!!!!!!
 
4.Kuweka sera nzuri na kuzisimamia,kwa maana ya kuzitekeleza. 5.Kukusanya kodi na kuhakikisha kodi zinaelekezwa kwa wkt kwenye shughuli za maendeleo na huduma za k kijamii.
 
safi kabisa mkapa, ila mzee unakumbuka wewe ndiye uliwahamasisha majambazi wateke magari kwa kauli mbiu yako eti mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe!!!!!!!!
 
Dear Mkapa!
Nlikusikilza kwa ufupi kwenye hotuba yako ulotoa majuzi kule Songea kwakti wa sherehe za kumpongeza Askofu wa jimbo hilo. Msimamo wangu, huenda ndiyo msimamo wa wengine katika forum hii ni kwamba:-
1. Maendeleo ya nchi yeyote huletwa na Serikali kwa kuwatafutia raia wake Masoko na vyanzo vya mitaji
2. Kuwajengea/kuwatengenezea miundombinu yenye kurahisisha uzalishaji wao
3. Kulinda mali zao walizojikusanyia ndani na nje ya nchi.
4. ..............
5. ............
mwenye hoja 4,5,6,e.t.c za kumpinga mzee Ben tafadhali ongezea!!

Ninakemea kwa NGUVU zote aina hiyo ya lugha uliyoitoa kwani ni UPOTOSHAJI WA MAKSUDI wenye lengo la kuwafanya raia wa nchi hii waendelee kuwa watumwa ndani ya nchi yao!!
NAWASILISHA!!!!!!!

Sitakubaliana hata siku moja kwamba maendeleo huletwa na serikali. Serikali hutoa miongozo na kusaidia kwa njia mbalimbali wananchi waweze kujitegemea.
Ukiniambia kwamba serikali ndiyo inayoleta maendeleo maana yake tukae tu na serikali itatuletea kile tunachotaka, ndo hayo ya kupitisha bakuli kwa wajomba na sasa bajeti tunayopanga ni kwa ajili ya kulipa madeni badala ya kuongeza mishahara ya wafanyakiazi na kuboresha miundo mbinu.

Bila wananchi kujenga uwezo wa kujitegemea katika utendaji na kuzalisha ziada serikali itabaki maskini mpaka mwisho wa dunia. Juhudi za wananchi ndizo zinazokuza uchumi wa taifa na kufanya serikali weze kupata ziada ya mapato ya kodi ili kufanya shughuli zake kwa ufanini.

Alichoongea Mkapa katika hotuba yake ni sahihi kabisa, tisiangalie mapungufu yaliyofanywa katika uongozi wake, hakuna binadamu mkamilifu, ila anachoongea kwa sasa ni bora. Naweza kusema anachosema Mkapa alikifanya katika utawala wake, mfumuko wa bei ulishuka, shillingi ilizidi kuimarika nk.
 
Hii si mara ya kwanza kwa Mzee Mkapa kusema hivi. Ni nani asiyekumbuka enzi zile za "Mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyewe" ? Sera na sheria za madini zinazolalamikiwa na wengi zilitoka katika awamu yake. Huyu mzee kuna mengi alifanikisha ila pia kuna madudu mengi sana pia aliyoyalea na "kuyapa hifadhi". Mambo ya EPA, IPTL, Meremeta na mengineyo mengi tu ni mafuvu ya Mkapa. Mnafiki mkubwa na yeye

PP na mtaji wa fisadi ni upi!? ambao yeye alikuwa nao na ukamuwezesha kuwa bilionea!? Kama ulivyomalizia huyu jamaa ni mnafiki sana anataka kuzungumzia mambo yote lakini si madudu aliyoyafanya akiwa Ikulu ikiwemo biashara. Si ajabu biashara hiyo alikuwa anaifanya na Serikali yake na kuilangua ili kuongeza speed ya uroho wake wa utajiri wa haraka haraka. Alivyo mnafiki sijamsikia hata siku moja toka amalize awamu yake akikemea ufisadi nchini ambao unaingamiza nchi yetu kwa sababu anajijua naye pia ni fisadi.
 
Mzee kalonga!!! Safi sana Mkapa.... that is the truth without chenga!!!!

Ukweli huu umejulikana leo? Ni kiongozi gani ameenda kugombea "asiwadanganye" wananchi kwamba atawaletea maendeleo?

Kuleta maendeleo kunaweza kuwa kwa aina nyingi ikiwemo kuongoza badala ya kutawala ili wananchi wafuate na kufikia malengo ya maendeleo.Kuongoza huko kunapaswa kuwe kwa namna itakayohakikisha nyenzo na rasilimali zinaelekezwa kuleta maendeleo na siyo kuishia mifukoni au matumboni mwa hao hao viongozi. Vile vile viongozi wanapaswa kuweka maslahi ya wananchi mbele na siyo maslahi yao binafsi kama tunavyoona sasa ambapo jitihada zipo zaidi katika kutetea maslahi binafsi ya viongozi kama posho nk.
 
Sasa zile ahadi 98 za JK alizoahidi maendeleo ya kila kona ya Tanzania wakati wa kampeni ina maana ni porojo?
Bado nasubiri Kigoma yetu kugeuzwa Dubai ya Africa na ile meli yetu hapa Lake Tanganyika
 
mkapa ana niambaya bali yeye anawakumbusha wana ccm wezake wanyakue migodi kama yeye muda umeisha.
 
Ukweli katika kauli ya Mh. Mkapa uko wazi ni kama Mh. Mwl. Nyerere alivyosema " maendeleo ya Watanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na serikali jukumu lake ni kutengeneza miundombinu mizuri itakayoweza kurahisisha wananchi kufikia malengo waliyoyakusudia. Ila mimi swali langu kwa mheshimiwa Rais wetu mstaafu ni kuwa "hivi yeye alipo kuwa madarakani hakulijua hilo" Pamoja na baadhi ya mikakati ya maendeleo alioianzisha, ila hakusita kutembeza bakuli kwa wahisani na kama hakufanikiwa kuwajengea wananch uwezo wa kujiletea maendeleo kiasi cha kutotegemea wahisani anajipi na yeye la kujivunia. Natamani kama nae angekua Jamvini nimuulize kuwa si ni katika Serikali yake ndipo Mh. Bazil Pesambili Mramba alipo tuambia hata kama ni nyasi tule ila ile ndege ya Rais ni lazima inunuliwe, ununuzi wa denge na Radi, unamjengea vipi uwezo mwananchi wa kujiletea maendeleo yeye binafsi na taifa kwa ujumla. Mimi nahisi viongozi wakisha staafu wanaziona fursa zaidi ya wanapokuwa madarakani sasa sijui hapa tatizo huwa ni nini? Rejea kauli za viongozi wastaafu juu ya mstakabali wa maendeleo ya Taifa letu na wao walifanya nini au walishinda vipi kutekeleza wanacho kisema sasa.
 
Habari zenu wanajamvi! naomba kuuliza hivi raisi wetu wa awamu ya 3 kapata wapi ujasiri wakujitokeza hadharani na kutoa matamko mazito licha naye kuwa na shutuma za ufisadi, au ameishaona kuwa aliyempokea kijiti ni kilaza zaidi hivyo kaamua kuokoa jahazi?
 
.Kwanza wote ni watuhumiwa wa ufisadi. Pili jk hana uuwezo wa kuyasoma mazingara ya hali zote kama Ben. Tatu jk alitumia vyombo vya habari kuonyesha kwamba Ben ndio fisadi alieasisi ufisadi nchini na kuushiriki pia. Mbinu hii ingempandisha sana jk kama angeweza kuutengeneza uchumi wa kuihusu jamii katika maisha ya kila siku. Sasa imekuwa kinyume chake, watu wana njaa mara nne ya wakati wa Ben. Sasa Ben imeliona hilo na kutambua umma unajuta kuwa na rais wa aina ya Jk, na kwa kupitia uchochoro huo ameamua kujibu mapigo kwa kujinadi kwa wananchi ili waweze kuamua wao wenyewe, kwamba marais hawa wawili nnani zaidi.Kwa mtizamo wangu na ambao nahisi ni wa wengi kulingana na hali ya maisha, naona wote yaani Ben na Jk ni wezi kutokana na mfumo wa chama wanachotoka cha ccm. Bali hata hivyo Ben yuko juu ya Jk mpaka sasa kwa kila kitu.Labda tutarajie muujiza kutoka kwa Jk maana, ana miaka mingine minne bado..
 
Mi naona Mkapa ameshindwa kundelea kuvumilia kushuhudia upuuzi wa kikwete. na ndio maana angalua ameamua kuanza kutoa matamshi mazitomazito. Vilevile naona ameamua "kubutua bora liende" japo kuwa anajijua kuwa naye ni fisadi.
 
Mkapa is only bad bcs aliyemtangulia before( Mwinyi) na aliyemfuta baadade(JK) wote ni worse. Ndani ya CCM kuna worst zaidi ya hao watatu na ndio prosective future presdent candidate. Inasikiskitisha hata Mkapa anaonekena ni bora lakini ndo ukweli wenyewe
 
.Kwanza wote ni watuhumiwa wa ufisadi. Pili jk hana uuwezo wa kuyasoma mazingara ya hali zote kama Ben. Tatu jk alitumia vyombo vya habari kuonyesha kwamba Ben ndio fisadi alieasisi ufisadi nchini na kuushiriki pia. Mbinu hii ingempandisha sana jk kama angeweza kuutengeneza uchumi wa kuihusu jamii katika maisha ya kila siku. Sasa imekuwa kinyume chake, watu wana njaa mara nne ya wakati wa Ben. Sasa Ben imeliona hilo na kutambua umma unajuta kuwa na rais wa aina ya Jk, na kwa kupitia uchochoro huo ameamua kujibu mapigo kwa kujinadi kwa wananchi ili waweze kuamua wao wenyewe, kwamba marais hawa wawili nnani zaidi.Kwa mtizamo wangu na ambao nahisi ni wa wengi kulingana na hali ya maisha, naona wote yaani Ben na Jk ni wezi kutokana na mfumo wa chama wanachotoka cha ccm. Bali hata hivyo Ben yuko juu ya Jk mpaka sasa kwa kila kitu.Labda tutarajie muujiza kutoka kwa Jk maana, ana miaka mingine minne bado..
:bump2:
 
Ni bora mzee wa ruksa kuliko mkapa fisadi ila kiboko ya wote uozooo mara elfu ni MKWEREE
 
Back
Top Bottom