MJIMPYA
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 506
- 272
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, amewataka viongozi wa serikali kuacha kuwadanganya wananchi kuwa wao ndio wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo.
Mkapa alisema hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kumletea maendeleo mwananchi kama hatashirikiana naye kwenye harakati za kupambana na umaskini.
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akitoa salamu ya misa ya Jubilei ya miaka 25 ya uaskofu, 38 ya upadri, 66 ya Ukristo na 66 ya umri ya Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Norbert Mtega, iliyofanyika katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Matias Mulumba Kalemba.
Mkapa, alisema kuwa jukumu la kujiletea maendeleo ni la wananchi wenyewe si la viongozi wa serikali au wahisani mbalimbali wanaofadhili miradi ya maendeleo inayoibuliwa na wananchi au kuandaliwa na serikali.
Aliongeza kuwa wananchi ndiyo wenye uchungu wa nchi yao hivyo wanapaswa waongeze jitihada katika shughuli za kujiongezea kipato.
Alisema kuwa hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, aliwahi kusema kuwa maendeleo ya Watanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na serikali jukumu lake ni kutengeneza miundombinu mizuri itakayoweza kurahisisha wananchi kufikia malengo waliyoyakusudia.
"Mimi nafadhaishwa sana ninaposikia viongozi wa kitaifa wanapowadanganya wananchi kuwa watawaletea maendeleo mbalimbali katika maeneo yao, kauli hizo ni potofu," alisema.
Alibainisha kuwa wananchi wanatakiwa wazipuuze kauli hizo kwani zinarudisha nyuma maendeleo husika pamoja na kujenga ukuta kati ya wananchi na viongozi wao.
Alisema viongozi hao wanapaswa kushirikiana na viongozi wa dini ili waweze kuwaonyesha juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi walioamua kujiendeleza.
Naye Askofu Mtega, alisema viongozi wa serikali wanapaswa kutambua kuwa uhuru na kazi ndio dhana pekee itakayopunguza na kuondoa malalamiko ya wananchi ambayo yanazidi kushamiri siku hadi siku.
Askofu Mtega alisema kuwa nchi haiwezi kuwa na uhuru kamili mpaka itakapojijengea uwezo wa kufanya kazi yenyewe na kujitegemea kiuchumi, kisiasa na kimawazo kulingana na mahitaji ya wananchi wake.
Alisema nchi inapaswa kuwa na dira, mwelekeo ambao utasaidia kuwaongoza viongozi kwa kushirikiana na wananchi kuyafikia malengo, mikakati na mipango waliyojiwekea.
Aliongeza kuwa kama nchi haina mambo hayo na inapenda kunakiri kutoka kwenye mataifa mengine duniani basi haiwezi kuwa na uhuru uliokamilika bali inakuwa na uhuru wa bendera.
Alibainisha kuwa uhuru huo wa bendera unaweza kupotea kwa muda mfupi kwa kuwa hakuna misingi ya kuwafanya wananchi wawe huru na wanaojitegemea.
Alisema msingi wa uchumi wa Tanzania unapaswa kuwa kwenye uzalishaji mali kwa wananchi wenyewe ili waweze kuwa na uchumi imara kwani vyanzo vya uzalishaji mali vipo hapa hivyo ni vema viongozi wakatumia mawazo ya wananchi.
Alisema viongozi wakitumia mawazo yao, ya wananchi pamoja na dira, mwelekeo wa taifa watajenga uchumi imara badala ya kujipendekeza kwenda katika nchi nyingine kuomba misaada.
Alibainisha kuwa katika kipindi hiki cha bajeti ya serikali iliyosomwa juzi mjini Dodoma wabunge wanapaswa kuhakikisha kuwa inakuwa bajeti ya kuwasaidia wananchi katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Alisema wananchi wakiwekewa mazingira mazuri ya kufanya kazi, kuwa wajasiriamali wenye kuzalisha bidhaa zenye tija kwa gharama nafuu itakuwa hatua kubwa ya kumkomboa kutoka katika lindi la umaskini.
Alisema kama serikali itakuwa imeandaa bajeti kwa kunukuu kutoka nchi nyingine au bajeti ya matumizi ya serikali tu basi bajeti hiyo haiwezi kuwasaidia Watanzania.
Alisema mwananchi anapokuwa na fursa ya kuuza mazao au bidhaa aliyozalisha katika mazingira mazuri nchi itaendelea kupiga hatua kiuchumi pamoja na amani na utulivu kuimarika zaidi kinyume na hapo ni kutengeneza matabaka yatakayokuja kuibua vurugu.
Sherehe za Jubilei hiyo ya Askofu Mtega ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mwadhama Kadinari Polycap Pengo, maaskofu zaidi ya 30, Anna Mkapa, na viongozi mbalimbali wa dini, serikali na vyama vya siasa.
Source: TZ Daima