Viongozi CCM wanawajua mafisadi wengine tofauti na tunaodhani sisi wananchi.

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Ukifuatilia hoja za viongozi wapya wa ccm kuhusu mjadala wa kwamba wanaotuhumiwa ufisadi wajiondoe kwenye chama ama wataondelewa,ni kuwa wao wanaofikiria ni tofauti na wananchi wanaowashutumu.

kuna rist iliyotolewa na Katibu wa Chadema mwaka 2007 na hii mpya ya 2011.na katika hiyo yumo Rais Kikwete na mkutano wa juzi wa ccm waliondoa magamba(wanaodhani hawafai) kwa kutumia orodha hiyo lakini JK hanaondolewa.

Viongozi wapya wanapodai kuwa mafisadi ccm waondoke wenyewe ama wataondolewa kwa nguvu wao wanadhani mafisadi ni hakina nani hao.

kwa ufupi.nataka kujua orodha ya mafisadi(kwa tafsiri ya viongozi wa ccm) wanaotakiwa kuondoka,mbona hawataji?
 
yaani mi nikimsikiliza nape najisikia kucheka maana anapayuka payuka tu sijui kama hata anajua nini anaongea...CCM bwana
 
Nape atapoteza heshima yake muda si mrefu, anapoelekea sasa atakuwa hana tofauti na Tambwe Hiza, CCM walitakiwa wapate watu watendaji, sio walalamikaji kama Nape, kama kweli wanataka mabadiliko!
 
Viongozi CCM wanawajua mafisadi wengine tofauti na tunaodhani sisi wananchi.

jibu ni ndiyo mkuu..

kwa mujibu wa spika makinda...fisadi ni mtu anaechukua mke wa mtu...

kwa hiyo wakati wananchi mnamuona EL ni fisadi wao hawamuoni hivyo muda wa kuwa katulia na regina wake...
 
Kwa ccm cheo cha Nape hata angepewa mpiganaji 6, heshima yake ingeshuka fastaaaa! Binafsi nikiona tu yale magwanda ya kijani ghafla hasira inapanda kwa imani ya chama cha wezi au mabaka uchumi wa tz!!! Hima vija wazalendo tufanye maamuzi magumu yakukiondoa chama hiki yenye mafaa kwa kizazi cha sasa na kijacho!!!!!!!!
 
Apoteza mara ngapi?

tena siku moja nilibahatika kukaa naye ni kweli anawachukia mafsadi LAKINI ANA MASIFA SANA!!!!
NINADHANI KWA SASA CHEO ALICHOPATA KINAWEZA KUMHARIBU, INAWEZEKANA WAMEFANYA HIVYO KWA MAKUSUDI KUMMALIZA!

Nape atapoteza heshima yake muda si mrefu, anapoelekea sasa atakuwa hana tofauti na Tambwe Hiza, CCM walitakiwa wapate watu watendaji, sio walalamikaji kama Nape, kama kweli wanataka mabadiliko!
 
Mimi hawa ccm siwaelewi kabisa, badala ya kuwafukuza mafisadi eti wanawapa siku 90 wajitoe wenyewe katika chama, hii inaonyesha wanaogopana!!
 
jibu ni ndiyo mkuu..

kwa mujibu wa spika makinda...fisadi ni mtu anaechukua mke wa mtu...

kwa hiyo wakati wananchi mnamuona EL ni fisadi wao hawamuoni hivyo muda wa kuwa katulia na regina wake...

Wengi hatulijibu lakini neno FISADI ni mtu anaechukua wake za watu au mzinifu wa kutosha. yupo sawa kwa hilo.
 
Mimi hawa ccm siwaelewi kabisa, badala ya kuwafukuza mafisadi eti wanawapa siku 90 wajitoe wenyewe katika chama, hii inaonyesha wanaogopana!!

hahawafahamu na wanajaribu kuchimba mkwara ili atakaejitoa ndo hana bahati. ni mkwara wa kawaida tu kama ule wa kusamehe wafungwa wa epa.
 
Kama inawezekana, nafikiri wangefanya recruitment mpya ya safu zote kutoka vyuoni, kwa watu ambao hawajawahi kushika madaraka kabisa katika chama hicho wala jumuia zake ila ni capable, halafu wao wote wakabaki wanachama wa kawaida au kujitoa kabisa kubaki bila chama, nje ya hapo wanabaki ni wale wale.
 
Watz tuwe wavumilivu, tuanze tathmini kwa uamuzi wa CCM baada ya siku 90 na si vinginevyo! Tuwape dole gumba kwa kutambua ufisadi umeshusha mapokeo ya wananchi kwa CCM, pia WAMETHUBUTU kuwapa taarifa wahusika wajitoe wenyewe ama sivyo cha moto watakiona. Mwenyekiti wa CCM ana kofia nyingine ya URAIS hivyo anaongea baada ya kupata ushahidi wa kutosha. Wana CDM muwe na subira AMA KIWEWE cha makomredi wapya wanaunda sekretaeti kinawatisha????
 
Back
Top Bottom