Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,323
- 18,541
Watoto katika hatua zao za ukuaji na kujifunza wanakuwa na mambo flani flani ya kufurahisha sana yaani mwanao anaweza kukuvunja mbavu balaa.
Mfano
1. Mwanangu (1.5years) anaweza kuwa anatazama TV akisikia unaongea na simu au umeweka music kwenye simu anakimbia kuja kuangalia simu hata kama TV ilikuwa na TV program ya katuni nzuri kiasi gani
2. Ukitaka alale we nenda kitandani weka music kwenye simu yako atakuja mwenyewe hata kama alikuwa anakwepa kulala
3. Anaheshimu simu yangu kama kituo cha polisi ila ya mama yake kashaipasua ukiiona utajua mama yake anafanya kazi idara ya miamba (geology)
4.Kupenda safari akiona mtu anatoka tu anaanza kuaga bye bye akijua nayeye anahusika na safari
5. Chakula kikiwa tayari, kabla sijaitwa kula yeye akiona mambo yako tayari anakuja kunipigapiga mgongoni(hajajua kuongea) akiashiria msosi tayari basi ukipotezea anaenda anarudi mpaka utakapoinuka
6. Mwanangu anatabia flani kama wivu, akiona naongea na mama yake mara nimemshika mkono tunaongea kama jambo la siri anakuja fasta analia anataka mama yake ambembe. Nadhani hajajua kwamba mama yake ni mke wangu
Hivi ni baadi ya vituko vya watoto mdau ongeza vya mwanao
Watoto wanaleta raha sanaaa