Hii mambo ya milingoti na digitali wapi na wapi?
Startimes wanasema ukiona king'amuzi hakishiki vizuri unatakiwa kuongeza urefu wa mlingoti, haya mambo ndo yamepitwa na wakati!
TCRA ni bora iwaambie wananchi wanunue decoder na dish za free channels ambazo hazisumbui na ziko stable.
Ndo maana mi nimeamua nibaki na kitu cha DStv changu, sina tatizo na mtu mwaka wa sita huu! Watoto watakuja kudondoka juu ya mapaa bure eti kisa unatafuta mwelekeo wa kisarawe!
Unatoka kazini kusaka mishiko, unafika home unawasha TV ili ujiburudishe na viuno vya shilole, unaanza kuona scratches na mapumziko yako yooote yanaharibika.
Kama serikali haitokubaliana na DStv kuongeza local channel, basi mi habari za bongo ntakuwa nazipatia JF na kwenye social media zingine lakini siko tayari kuweka takataka nyumbani kwangu.