Ving'amuzi vya EASY TV

Babu wa Loliondo

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
323
Reaction score
106
Asalaam wana JF
Nafikiria kununua king'amuzi cha Easy Tv,ila kabla sijalipia ningeomba kupata maoni yawe chanya au hasi kwa yule ambaye anakitumia king'amuzi hiki.
Natanguliza shukrani zangu
 
Asalaam wana JF
Nafikiria kununua king'amuzi cha Easy Tv,ila kabla sijalipia ningeomba kupata maoni yawe chanya au hasi kwa yule ambaye anakitumia king'amuzi hiki.
Natanguliza shukrani zangu
nakitumia,nikizuri sana japokuwa kuna wakati baadhi ya chaneli zinagandaganda hasa za muvi.sijaweza kubaini tatizo ni nini kama ni king'amuzi chenyewe au ni setting yangu ya antennae ndo sio nzuri.pia star tv mara nyingi huwapotea hewani.kwa sasa ina wiki mbili haipatikani.sijajua tatizo ni nini pia au ndo wameshajitoa.nawasilisha kwa msaada
 
Asante mkuu kwa msaada wako,vipi kuhusu chanel zao local pamoja na international kama BBC World services,na kama wana za michezo hata moja na za east africa kama ubc,citizen na kbc zipo pia?. kuganda linaweza kua ni la kiufundi labda kama ulivyosema
 
Shukrani kwa mchango wako japo ningeomba kidogo maoni yako yawe hasi au chanya na changamoto zake
 
Kinunue tuu hutojutia ninacho natumia bila shaka moja kina Picha za kiwango cha kuridhisha ukilinganisha na dstv niliwahi kutumia pia ila Kati ya channel zao walizotangaza ni moja tuu sijawahi kuona nayo ni MTV BASE niliwahi kuuliza nikaambiwa labda ni eneo nililoset pia tangu mgogoro wa startv wameweka channel mpya zaidi usipolipia bill utaona channel moja tuu tbc pekee kingine kupata vocha za kulipia kuna Tatizo hazipatikani kila mahali kama huduma inavyotakiwa.
 
Shukrani sana mkuu chescomatunda kwa ufafanuzi wako wa kina,sina budi kukinunua tu na nitakupa jibu mkuu
 
Asalaam wana JF
Nafikiria kununua king'amuzi cha Easy Tv,ila kabla sijalipia ningeomba kupata maoni yawe chanya au hasi kwa yule ambaye anakitumia king'amuzi hiki.
Natanguliza shukrani zangu

Nakitumia maskani. Nikifananisha Easy TV na Startimes, ETV is by far the best, ni sawa na kufananisha mafua na Ebola. Bila kusuasua we kinunue tu. Monthly fee ni flat, 9000/-.
Wana channel 5 za Movie, 2 za katuni (Nikkelodeon na Mbc3), 2 za taarifa za kimataifa (BBC na Al Jazeera), MTV na Channel V (Burudani), za dini ziko 4 (Emmanuel Tv, EWTN, na za Kiislamu 2, moja Kiingereza na moja Kiswahili), za Michezo kuna Optima (wanaonesha recorded matches za EPL) na Dubai Sport. Kama we mpenzi wa mieleka basi hapo ndio penyewe. Za hapa nyumbani unapata:-
Itv, Channel 10, Tbc1, Eatv, Clouds Tv, DTV na capital. Star TV imeondolewa (wana ugomvi wa kibiashara, kwa sababu Star Tv wanataka Tv hiyo iwe kwenye kisimbuzi chao tu)

Ndugu, niliuliza wakala wao mmoja, alisema kwamba Star TV hawataki channel yao ipatikane kwenye visimbuzi vingine, wanataka waioneshe kwente Continetal yao tu, ndio sababu wameiondoa. Ila niliambiwa itarejeshwa, kwa sababu suala hilo linashughulikiwa na TCRA
 
Ila vinaishia mbezi mbele ya kibamba huko vinaanza kuleta shida. Kwanini wasivushe mitambo yao mbali maana wana chennel nzuri saana
 
Asante sana tena sana ndugu yangu Idimi kwa maelezo hayo ya kujitosheleza kabisa,soon naenda kukinunua hao Star Tv ni juu yao madhalani nitapata 99% ya local chanels sio mbaya kabisa
 
Mim niko maeneo ya ubungo maziwa nadhani nitakua kwenye eneo lao yaan ''Coverage areas''
 
Ila vinaishia mbezi mbele ya kibamba huko vinaanza kuleta shida. Kwanini wasivushe mitambo yao mbali maana wana chennel nzuri saana

Nilichoambiwa na wakala wao ni kwamba, waliomba leseni ya kurusha matangazo nchi nzima tangu 2009, hawajapewa mpaka leo, wamepewa ya Dar tu. Niliambiwa kwamba kuna wakubwa wapo nyuma hiyo njama kwa sababu wanamiliki hisa pale Bamaga, kwa sababu jamaa wakiruhusiwa kuuza nchi nzima then wale wa Bamaga wenye channel za kukwamakwama na bei za ajabu ajabu ndio kwishnehi. Kwa package ya hawa jamaa, wakipewa licence hata robo ya nchi nadhani wengi watatupa ile ya Bamaga.
 
asalaam wana jf
nafikiria kununua king'amuzi cha easy tv,ila kabla sijalipia ningeomba kupata maoni yawe chanya au hasi kwa yule ambaye anakitumia king'amuzi hiki.
Natanguliza shukrani zangu

achana na presha ya vifumbuzi , nunua ungo a.k.a dish futi 8 ndo mpamgo mzima
 
Idimi,tunashukuru kwa ufafanuzi naomba kuuliza installation cost ni bei gani(gharama za kingamuzi au dish la Easy Tv)
 
Last edited by a moderator:
Belo jamaa niliwauliza wakasema ni TZS 110,000 decoder,antena na charge ya mwez mmoja! Ila mlingoti kwa ajili ya antena ni juu yako.
 
Vp usipolipia iyo 9000 kwa mwezi au ukachelewa, wanakata matangazo yote au chanel za taifa zinabaki?
 
Idimi,tunashukuru kwa ufafanuzi naomba kuuliza installation cost ni bei gani(gharama za kingamuzi au dish la Easy Tv)

130,000/= Pamoja na mlingoti
 
Last edited by a moderator:
mkuu hawa jamaa wapo poa sana na wana channel makini. hivi wakuu hii haichakachuliki?. mia
 
Wana jamii mie nipo Kimara na ninapata zote hizo ili mradi bomba iende juu sana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…