kajirita
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,575
- 638
Habari wana JF.
Jana nilitembelea nyumbani kwa rafiki yangu wa siku nyingi tuliyesoma wote shule ya sekondari, ambae tulikutana mitaani baada ya kupotezana miaka mingi iliyopita.
Yeye ni mtaalamu wa mambo ya IT (Mifumo ya mawasiliano). Nilifika kwake mida ya saa kumi na moja za jioni tukapiga stori na kukumbushia masuala ya zamani. Nilishangazwa sana na kitendo cha rafiki yangu huyo muda wote tunaongea yeye alikuwa ameweka DVDs kwenye deki akiwa anatizama movie.
Sikutaka kuingilia maamuzi yake, lakini ilipofika saa mbili mida ya taarifa ya habari uzalendo ulinishinda! Ikabidi nimuombe aweke taarifa ya habari ili tuweze kujua nini kimejiri siku hiyo.
Akanishangaa sana. Akaniambia yeye hatumii king'amuzi! Akasema king'amuzi ni kifaa ambacho kimewekwa kamera maalumu ambayo inaweza kurekodi matukio ya picha na sauti ambayo yanatokea majumbani mwetu.
Akaongeza kuwa king'amuzi kinasadia polisi wetu, polisi wa kimataifa (Intelpol) na majasusi (kama CIA) kuweza kubaini mipango ya kigaidi na kihalifu ili kuweza kuizuia kabla haijaleta madhara kwa jamii. Hivyo yeye hawezi kukitumia kwa kuwa kinamnyima haki yake ya kuwa na faragha!
Mwanzoni nilifikiri amechanganyikiwa, lakini baada ya kurudi nyumbani nimefikiria mpaka nimeshindwa kabisa kuwasha king'amuzi changu cha chumbani kwa kuogopa mimi na mke wangu 'kurekodiwa'!!
Sasa nawauliza waungwana, Je, hili suala ni la kweli? Je , ni kweli kuhimiza na kulazimisha matumizi ya ving'amuzi lilikuwa ni jambo la kiusalama zaidi na si suala la faida na hasara kwa wale wenye vituo vya televisheni?
Vipi kuhusu sisi ambao tumeweka ving'amuzi vyumbani au wale ambao wapo nyumba za kulala wageni hamuoni mnawanyima haki ya kuwa faragha?
Naiomba serikali kama jambo hili ni kweli basi ipige marufuku matumizi ya ving'amuzi nchini kwani vinaenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na vinaingilia uhuru wa watu kuwa faragha!
Naomba kuwasilisha.