Vincent Nyerere: Sijaona mkataba kati ya ukoo wangu na CCM

Mnadhani nyerere angekuwepo angekuwa chama kimoja na akina lowasa majambazi na mafisadi?

Pengine c.c.m ingeendelea kua na mvuto,maana mafisadi,wauwaji,makaburu na wanyonyaji wa rasilimali za watanzania wangekimbia c.c.m na kuanzisha chama chao,wasingeweza kua chama kimoja na mwalimu!na inawezekana pia mkuu wa kaya hasingeweza fanikiwa kukamata nchi!angekua anaiota tu
 
Kauli nzito sana hii!!! Duhh, angalieni huko hekima zilikolala kwa Baba wa Taifa Mwalimu J. K. (wa ukweli) Nyerere.

Wana JF leo asb ITV katika kipindi cha Kumekucha,katika mahojiano ya Mbunge wa Musoma Mjini na watangazaji wa ITV,eti kwani yeye ni mtoto wa mdogo wake na baba wa TAIFA na Muasisi wa CCM kwa nini yupo CHADEMA.

Duh amewajibu kuwa hajaona mkataba kati ya ukoo wa Nyerere na CCM kwa hiyo hata CHADEMA ni chama cha Watanzania kama CCM.

Ila Dogo yupo fit kwenye mahojiani na waandishi . Sjui nani ana Mapungufu kwenye mashine za CHADEMA(wabunge)
 
Sidhani kama Maria Nyerere anaweza kujitokeza na Chadema. Si unajua tena anaogopa kunyimwa mafao na Serikali ya Magamba. Hata hivyo, Vincent Nyerere ni kiboko, namkubali. Makongoro Nyerere alimsaliti Baba yake (Mwl. Nyerere) kwa kukubali kula matapishi yake - kugeuka jiwe? Baada ya kupata ubumge NCCR mbele ya Baba yake aliamua kurudi kwa magamba. Na sasa ni mwenekiti wa magamba Mkoa wa Mara. Yuko kimya!!!!
 
he he he he he kijana aliongea point nzuri sana....kuwepo au kutokuwepo kwa Mwalimu JK haimaanishi watu wawe na heshima ya uoga ya kujifanya wapo CCM kumbe hamna kitu...
 
Sahihisho! Sio mtoto wa mdogo wake Nyerere (Kiboko) ila ni mjukuu wa mdogo wake Nyerere. Yaani mdogo wa Nyerere kwa jina KIBOKO alizaa binti na binti akamzaa Vincent na wengine.
Hivi wazanaki wanarithi majina ya ukoo toka kwa mama zao? Hebu fafanua hiyo taarifa yako.
 
Sahihisho! Sio mtoto wa mdogo wake Nyerere (Kiboko) ila ni mjukuu wa mdogo wake Nyerere. Yaani mdogo wa Nyerere kwa jina KIBOKO alizaa binti na binti akamzaa Vincent na wengine.

nikusahihishe hapo ni mtoto wa mdogo wake mwalimu nyerere ambaye anaitwa kiboko
 
Kwake huyu kijana Vincent Nyerere naona nuru njema kwa Tanzania ya kesho.

CHADEMA ka-mleeni kijana vizuri apate kuiva vema ki-uongozi huku tukimsubiri Kamanda Makongoro Nyerere kujiunga na 'FANANIA YAKE' humu wakati wowote ule.
 
acha umbea kaeleza mwenyewe kuwa ni mtoto wa Jsephat Kiboko Nyerere ambae ni mdogo wake na Mwalimu Nyerere,kati yako na yeye nani mkweli?

Kweli mkuu huyu ni mtoto wa marehemu Joha Ali Nyabange ambaye aliolewa na Kiboko Nyerere. Hivyo naomba kufuta usemi wanajanvi.
 
Back
Top Bottom