Vincent Nyerere amstaafisha rasmi Ben Mkapa siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vincent Nyerere amstaafisha rasmi Ben Mkapa siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanzaniaist, Apr 4, 2012.

 1. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana huu mwaka wa 2012 ndio mwisho wa Ben Mkapa kisiasa na hata ndio mwanzo wa kuporomoka kwa umaarufu na heshima miongoni wa Watanzania..,Ben Mkapa ulikuwa mwiba mkali uliowashinda Agustino Mrema,Ibrahim Lipumba,James Mbatia lakini kijana mdogo toka kule Musoma Mh.Vincent Nyerere ameweza kuumeza mfupa uliowashinda wapinzani wengi baada ya kumpa Ben Mkapa vidonge stahiki wakati wa Kampeni Arumeru hadi kufikia hatua ya kuhaha kwa ndugu wa nyerere kuomba msamaha...! Namfananisha Vincent Nyerere na David aliyemwangua Goliath (ben mkapa) kwenye mapambano..., Nafikiri kazi aliyekuwa nayo sasa hv Ben Mkapa ni kurudi tu kijijini kwao Mtwara kufanya shughuli za kilimo kama wastaafu wenzake..Baada ya kupata mbabe wake kwenye uringo wa siasa
   
 2. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Nifamilia ya Nyerere (Julius Kambarage Nyerere RIP) iliyomweka Mkapa ktk siasa, maana kabla ya kuwa Raisi Mkapa hakujulikana, Na familia hiyo hiyo(Vicent Nyerere) ndio imemrudisha alikotoka.
   
 3. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa katika historia ya CCM Kijana mdogo Joshua Nassari akiongozwa na makamanda wa chama cha Demokrasia na maendeleo wameweza kulingusha Gamba na Moja na Gamba namba Mbili Livingstone Lusinde aliyeacha asili yake ya wagogo na kujiita Livingstone na Mgogo wapi na wapi magamba hayo pale yamepigwa mweleka wa nguvu nawana Arumeru Peoplesssssssssssssssssssss Powerrrrrrrrrr hawatarudia tena ukianzia kwa mtangulizi wao Yusuph Makamba wamepigwa chaliiiiiiiiiiiii hatarudia tena nawauliza watanzania wapenda Mageuzi kuna aliyebaki kama yupo ajitokeze Segerea kwa Ukimpenda Mzoeeeeeeee.
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Aende zake ,nilimpenda kiasi Ben lakini kwa kuhusika na kumaliza uhai wa Nyerere hapo kwa kweli ntamwona kama mtu wa mataifa
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Piga chini Mzee Nkapa. yeye ndo ufisadi ulikoanzia
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni bora apumzike mambo ya kuongozana na akina lusinde yanampunguzia heshima abaki tu kuwa kaka wa taifa as long as ni mkapa J. Nyerere
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani kwa sasa Mheshimiwa Rais mstaafu anafikiria namna ya kujitoa kabisa katika siasa maana hakutegemea kukutana na upinzani na majibu ambayo aliyapata kutokana na matamshi yake,alizoea watu kumvumilia hata pale inapoonekana kabisa kavuka mipaka ya siasa,kwa hili limekuwa fundisho kwake na hata kwa viongozi wengine ambao wakiwa majukwaani busara hupotea na kujikuta wanaanza siasa za kupakana matope ambazo hawaziwezi.
   
 8. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  "Ninawashukuru sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu, uwezo wangu kifedha, historia ya familia yangu katika siasa, na mapungufu niliyokuwa nayo lakini wakakubali kunichagua!
  Najua walikuja wengi na fedha nyingi,
  Najua walikuja wengi na majina makubwa,
  Najua walikuja wengi na kila aina ya mbwembwe,
  Najua walikuja wengi na bendi nyingi na wakahonga sana,
  ... Najua walikuja wengi wakanitukana na kunisema sana! Lakini hatimaye sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, na lile alilolipanga mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika!

  Walipoambiwa mimi ni mdogo kiumri, walisema siendi bungeni kupeleka mvi au miaka, na wakasema wanahitaji dogo janja na si kubwa jinga,
  Walipoambiwa mimi sijaoa, wakasema mimi siendi bungeni kusuluhisha ndoa,
  Walipoambiwa mimi ni masikini, walisema wanahitaji masikini mwenzao,
  Walipoambiwa sina kitambi, walisema bungeni siendi kucheza mieleka…"


  -Mh. Joshua Nassari
   
 9. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkapa hana heshima yoyote kwanza hajui kuongea kwa busara anatukana tu, ungesema Mwinyi ana heshima yes ila Mmakonde huyo hapana. Heshima ya mtu unaipima kwa maneno yake yana busara kiasi gani. Amewaita wapinzani wapuuzi tena hawana adabu, kisha baadae akawaita vifaranga hapo busara siioni
   
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nataka nifuatilie kitambi cha Kapten John Komba kimewasaidia nini wananchi?????????
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda sana hii analogy

  David (Vicent Nyerere) and The Goliath (Benjamin Mkapa)! Hii hadithi inatueleza kwamba Kijana mdogo David aliua JITU KUBWA lilolokuwa likiogopwa the Goliath kwa silaha duni aina ya KOMBEO.
   
 12. m

  mimdau Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Walipoambiwa mimi ni mdogo kiumri, walisema siendi bungeni kupeleka mvi au miaka, na wakasema wanahitaji dogo janja na si kubwa jinga,
  Walipoambiwa mimi sijaoa, wakasema mimi siendi bungeni kusuluhisha ndoa,
  Walipoambiwa mimi ni masikini, walisema wanahitaji masikini mwenzao,
  Walipoambiwa sina kitambi, walisema bungeni siendi kucheza mieleka…"

  haya si maneno yangu ni ya kamanda josua
   
 13. remon

  remon JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuwa na upara c kuwa akiri nyingi au busara unaweza kuwa unapara na ukawa mjinga wa mwisho kati ya wajinga!!!
   
 14. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ache,nkapa naona aibu kunyima ntu mwili.
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mna maana nyerere aliuawa?
  KUWENI SIRIAS BASI JAMANI?
   
 16. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani angalieni na umri unakwenda, watalaamu wanasema kuwa jinsi umri unavyo kuacha mara nyingi akili nayo hupungua, Mkapa hakujua kuwa anaongea na watu ambao wako makini na wanataka kuondokana na umaskini walio nao,akajua nikisema kuwa Vicent si miongoni mwa familia ya nyerere watu watamponda hatimaye chama chao kiweze kushinda, lakini akasahau kuwa huyo anaye mponda ana akili nyingi pia ni kijana mwenye uelewa sana. Mzee mkapa hoja zikawa zimeshinda akaishia kuomba msamaha na hiyo kisiasa tayari amecheza faulo kubwa ambayo ataijutia kwa sababu hataweza kuheshimika tena. Na hili chama cha mapinduzi inabidi waangalie sana kwenye maisha hakuhitaji masihara kuna hitaji kuwa serious na si mchezo mchezo ambao CCM wanaufanya.Leo hii hali ya uchumi wa nchi ni mbaya Hakuna shughuli za uzalishaji zinaoendelea, ajira hazina uhakika, gharama za maisha ni kubwa nk. CCM badala ya kuangalia hayo kazi ni kutukana kwenye majukwaa na wakasau kazi ya msingi ambayo ni kuandaa maisha bora kwa watanzania

  jamani uongozi ni kazi !!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii tunaiita Panga moja Mbuyu chini
   
 18. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  "ulimi wake mrefu umeliponza bichwa lake" shame on him!! nika kama mtu aliyekua anakunya hadharani.
   
 19. ChaterMaster

  ChaterMaster JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 1,290
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Exactly man
  we n noma!
   
 20. D

  Deo JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Yote sawa ila kwenye red, mh arudi Mtwara? Amepakimbia, amepakana, amebadili ukoo na kuwa mkosi alikohamia. Ile jumba la kifahari pale dari salama ufukweni yenye paa ya kijani kibichi amwacie nani? Labda aende Lushoto! Nako huko wanamchukia au kwa semgi lakini kale ka mama kalimvunjaga mguu na aliwanyanya masemegi awamu yake ya kwanza nao wanausongo naye labda amsaidie pesa mbili pale kibo palece.

  Historia itakukumbuka kwa mengi, mazuri maovu na tabia yako binafsi
   
Loading...