Vimemo katika ajira vinatufanya tuonekane vilaza.

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487

Kama kawaida yangu napenda thread zangu zijikite sana katika kutengeneza Tanzania yenye weredi. Katika thread hii naomba tuchangie hili la ajira za hapa nchini. Mara nyingi kumekuwepo na maelezo kuwa watanzania wengi hawana uwezo wa kujieleza pindi wanapoitwa kwenye Interviews, aidha utakuta wengi wao hawajui wanakwenda pale kufanya nini, hawana feedback ya kampuni au shirika wanalokwenda kuomba kazi na wengine hawajui hata majukumu ya nafasi wanazoziomba.
Tatizo kubwa hapa limekuwa likitokana na watu waliotangulia kuwa katika nafasi zao zenye maamzi kutumia nafasi hizo kulazimisha waajiri kuwapa upendeleo watu wao hata kama nafasi iliyopo ni tofauti na professional yake. Mara nyingi utasikia mtu akipiga simu….. “Naomba umchukue tu ndugu yangu, atajifunza hivyohivyo tu polepole” au anaingia pale ofisini kwa ki-memo, pindi anapoingia ofisini utacheka kwani hajui hata pa kuanzia. Huku kubebana hata pale ambapo hapatakiwi kufanyiwa dhihaka ndiko kumepelekea watanzania tuonekane vilaza mbele ya mataifa mengine, hali hii ndiyo iliyopo katika Taasisi ya vitambulisho vya Taifa NIDA kuwa kama ilivyo kwa sasa. Ni vichekesho tupu, wana jamvi jaribuni kufuatilia hawa waliochukuliwa kama DATA ENTREY, utachoka mwenye kwani pale wamewekwa hata waliomaliza mambo ya hotel management, Surveys, nk, mbaya zaidi nasikia umalaya umetangulizwa mbele kuliko. Haya kazi kwenu.
 
Suala la vimemo nakubaliana kabisa kwamba linadidimiza utendaji kiasi cha kuonekana vilaza aka vihiyo. Ndio maana sehemu zote zenye ulaji utawakuta watoto au jamaa wa karibu wa vigogo (BOT, TRA na hata makampuni makubwa). Wakati mwingine makampuni makubwa yanakubali vimemo ili iwe kinga ya kuyaruhusu kufanya watakavyo. Pamoja ni vimemo ni kweli pia umahiri wa wahitimu wengi wa ngazi mbalimbali ni wa chini, kiasi kwamba kushindwa kukidhi mategemeo ya mwajiri si jambo la kushangaa. Mazingira wanayosomea, uwezo wa waalimu/wahadhiri, uhitahi na utayari wa wanafunzi kujifunza mambo ya msingi nk. vyote hupelekea wahitimu wasiokidhi matarajio ya waajiri wengi. Usishangae wanafunzi wa chuo kikuu ikitokea taarifa ya habari kwenye luninga waondoka, lakini ukifika wakati wa tamthilia ya Kikore/Phillipino nk. wanaacha kila kitu na kuwahi kwenye luninga. Unategemea kuwa na wahitimu wa namna gani?
 
Nakubaliana nawe mkuu, Point taken.
 
Back
Top Bottom