Wana Jamii
Member
- Sep 10, 2020
- 16
- 3
- Thread starter
- #141
Milioni 100 mbona hiyo ni hotel ya zero star kaka. Unajua tunazungumza hapa tukiwa na facts nyingi tu.Yaonekana huijui Biashara ya Hoteli ndio maana unaona Mwajiri wao amejitahidi sana kuwalipa. Labda useme amejitahidi ukimlinganisha na mwajiri mwengine lakini hakuna uungwana wowote.
Waambie waoneshe their financial statements hadharani mujionee ni kiasi gani wanaingiza kwa Mwezi tu mjionee. Unafikiri hoteli yenye gharama ya milioni 100 kwenye mshahara wa wafanyakazi wao wanaingiza kiasi gani kwa mwezi?.
Hio Milioni 100 kwa mwaka net profit nimekutolea mfano tena ni wa hoteli mbuzi tu ata 3 star haifiki vizuri!
Halafu kitu kingine utambue kuwe, katika mwaka kuna kuwa na low season, kipindi ichi hoteli inaweza ikafungwa kabisa, maana yake ata mia haingizi na siku ya kufungua basi wanatumia gharama nyingi katika ufunguzi au huwa wanafanya renovation miezi miwili hadi mitatu, na huwa wanalipa wafanyakazi hela ya likizo full kipindi chote ambacho hawapo kazini.
Sasa swali langu, kwanini wameshindwa kuwalipa hela ya likizo full mara hii na kusingizia corona wakati miaka ya nyuma wakifunga hoteli wanalipa watu?