Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,943
- 6,863
Mbunge nusura agome kushiriki mkutano wa UWT
2008-01-07 10:03:21
Na Selemani Semunyu, Morogoro
Mbunge wa Viti Maalum (walemavu), Bi. Magareth Mkanga, nusura agome kushiriki mkutano wa Baraza la Jumuiya ya Wanawake wa CCM mkoani hapa, kutokana na kufanyika ghorofani.
Hali hiyo, ilijitokeza jana katika ukumbi wa Mount Uluguru, ambapo mkutano huo ulifanyika katika ghorofa ya nne.
Bi. Mkanga, alisema eneo lililoandaliwa kwa ajili ya mkutano huo, halikuwa na miundombinu inayotoa fursa kwa watu wenye ulemavu kama yeye, kufika kwa urahisi.
``Nilikusudia kukataa kushiriki, ili liwe fundisho na kuwakumbusha wajumbe wote waliohudhuria kwa kuwa ni viongozi, mhakikishe kuwa mnawawezesha walemavu kufika wanakotakiwa,`` alisema.
Alisema, hali kama hiyo inawakabili watu wenye ulemavu kama vile shuleni na vyuoni.
Moja ya vitu ambavyo naamini vinaturudisha nyuma kimaendeleo kama jamii ni hii apathy yetu kuhusu masuala kama haya. Hii apathy inaendelea mpaka kwenye masuala ya mazingira, elimu n.k. Ukiangalia watu walio'bother' kuisoma thread hii na wale ambao wanasoma ishu nyingine zinaonyesha wazi priorities zetu. Jamii yakitanzania inapenda majibu rahisi yasiyowalazimisha kujiangalia kwenye kioo. Tumegeuza siasa kuwa kama mchezo wa mpira. Kwa bahati mbaya, hatutaweza kujikomboa kama jamii bila kumjali yule aliye mnyonge katika sisi. Kwa mtaji huu, hawa walemavu watazidi kusota maana jamii yetu haiwatambui na haioni umuhimu wao. Asante Mzee MwanaKijiji na Mzalendo kwa kuonyesha concern zenu.
huwa nawahurumia sana wenye ulemavu- sema tu sina jinsi ya kuwasaidia- huwa nawatetea siku zote![/B]
Watu wanashindwa tu kutambua kuwa hakuna mtu anachagua kuwa mlemavu- hii inatokea tu- na hata leo hii mtu uu mzima- ukipata ajali au ugonjwa pia unaweza kuwa mlemavu!
Tafadhalini sana wana JF...neno vilema si sahihi hapa tutumie, watu wenye ulemavu. Ni muhimu kuonyesha kuwa hawa ni binadamu wenzetu! Tuanze sasa kwa sababu wengine hufikiri watu wenye ulemavu si watu!
Nakusihi pia muanzisha thread urekebishe. Hata kuku anaweza kuwa kilema!. Lugha tunazotumia ku address watu wenye ulemavu saa nyingine huwa stigmatize zaidi!
Wandugu hatuhitaji "kuwahurumia" walemavu. wanchohitaji watu wenye ulemavu ni sera bora na kuwezeshwa, mfumo wa jamii utakaosimamia na kulinda haki zao, fursa zitakazowawezesha na wao kuchangia ktk maendeleo ya taifa.
Hii "charity model" sio sahihi.....
Nope....sikubaliani na wewe kuhusu huruma. Hii inaitwa charity model, kwamba watu wenye ulemavu ni "wakuhurumiwa". Ndio maana unaona kazi hii ilichwa kwa philanthropist..makanisa etc. Model hii inaendeleza "umaskini" kwa wenye ulemavu kwamba they are people to be pitied!
Tuwape nafasi...
FM huruma haitajenga...sanasana itaendelea kuongeza watu wenye ulemavu wenye vibaba wakiomba kama unavyoona pale Salender!Kwa hiyo mama Lao unaona kuliko kuhurumiwa heri waachwe kama walivyo mpaka jamii itakapofikia mahali pa kuwakubali? Si heri tujenge kwenye hiyo huruma, tuibadili kuwa kuwaku bali? Si hawa hawa wenye huruma ndiyo wanaopandikiza mbegu kwa wenye ulemavu kuweza kusimama na kudai utambulizi kama sehemu ya jamii?
FM huruma haitajenga...sanasana itaendelea kuongeza watu wenye ulemavu wenye vibaba wakiomba kama unavyoona pale Salender!
Kinachohitajika ni
Sera..zinazolinda haki za watu wenye ulemavu na kuwapa fursa mbalimbali kama huduma za utengemao, elimu, ajira etc.
Mfano wale wenye baiskeli maalum kundi kama la watu 10 kwanini waendelee kuwa ombaomba pale Salender? Je kwa mfano wangepewa mkopo na kazi ya kuuza vocha za simu...si wange survive? au wangepatiwa eneo maalum la kufanya biashara ambalo liko accessible kwao na kwetu ...[/QUOTE
Mama Lao mbona unajichanganya? Kwa kuWAPA mkopo si tunarudi kulekule kwenye baiskeli? Kitu gani kinakuaminisha kuwa wasingetumia mkopo huo kuolea wake wa ziada, kulewea n.k. kama wanavyofanya wengine? Sera hazitabadilika bila msukumo. Msukumo huu unatakiwa utoke kwa walemavu wenyewe pamoja na wale ambao watakuwa tayari kuungana nao katika vita hiyo. Bila kujenga utambuzi kwa walemavu wenyewe kuwa wao si watu wa kuombaomba tuu hatutafika mbali. Utambuzi huu utajengwa kwa kiasi kubwa na elimu, rasmi na isiyo rasmi. Watu kama nyinyi mkienda, kwa vitendo, kuungana nao na kuwaeleza kwa nini wanastahili kudai na kupewa haki sawa na mtu mwingine yeyote itasaidia kutoa msukumo huo. Pamoja na hiyo haki wanapaswa kuelezwa na majukumu yanayotokana na haki hizo. Wakiendelea kuendekeza kuwa ombaomba jamii itaendelea kuwachukulia hivyo. Wale waliowapa zile baiskeli hawakuwaambia waende nazo Salenda kuombea. Zile baiskeli wangeweza kuzitumia kuwafikisha sehemu nyingine ambako wangeweza kufanya shughuli mbadala za maendeleo yao. Lakini kwa vile wamekubali kuwa wao ni watu wa kuonewa huruma ndiyo maana wamekimbilia Salenda.