Vikosi vya ulinzi na usalama viwanja vya ndege

Vikosi vya ulinzi na usalama viwanja vya ndege

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
20,141
Reaction score
24,449
Tangu mara ya mwisho wakati wa utawala wa mzee ruksa ndio ilikuwa mwisho wa wana usalama wetu kukamata mali uwanja wa ndege kipindi hicho waziri wa mambo ya ndani ni liyatonga mrema,vikosi vikapotea na kuingia kwenye usingizi mzito rasilimali zikapita viwanjani kama hawazioni na zikapewa ulinzi mpaka zinapoishia

Lakini hivi sasa tangu awamu ya tano iingie madarakani naona hali imebadilika hatusikii kusafirishwa wanyama hai na kila baada ya muda tunasikia madini mfululizo yamekamatwa viwanja vya ndege arusha na dar na hii ya bandarini

Swali jee hiki kikosi kilikua kinapewa maslahi madogo au ni uduni wa vifaa au wamekuja vijana wapya

Baba akiwa mkali lazima heshima iwepo nyumbani!!
 
Enzi Hizo nchi hii Ilikuwa shamba la bibi,walanguzi walifanya watakalo kwa kutoa kitu kidogo awamu ya tano haturuhusu uchafu huo
 
kwa iyo unasema uzembe na wizi wa serikali ya CCM ulisababisha nyara na vito kutoroshwa kwenye viwanja vya ndege na bandari??
Ni kweli mabadiliko ya kweli ya uongozi na kuzaliwa ccm mpya imepelekea kila mmoja kupigania rasilimali za nchi mpaka imepelekea madiwani wa arusha kuvutiwa na utendaji wa awamu ya tano chini ya amiri jeshi mkuu JJP MAGUFULI!
 
Enzi Hizo nchi hii Ilikuwa shamba la bibi,walanguzi walifanya watakalo kwa kutoa kitu kidogo awamu ya tano haturuhusu uchafu huo
Tumeshuhudia vichaka vikifyekwa na wala rushwa wakihamia kichaka kipya chadema!
 
Back
Top Bottom