Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
MAROON BERETS (UTURUKI)
Kikosi hiki maalum kinapatikana nchini Uturuki kilianzishwa mwaka 1992 kikiwa chini jeshi la Uturuki yaani Turkish Armed Forces (TAF) . Kikosi hiki kinapokea amri moja kwa moja kutoka kwa Amiri jeshi mkuu na si kutoka kwa wakuu wa jeshi.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi maalum cha Maroon Berets
Maroon Berets katika sare maalum ya kazi
# 9 MARINE JEGER KOMMANDOEN (NORWAY)
Kikosi hiki kilianzishwa mwaka 1953 kikiwa na lengo la kupambana na manazi wa Ujerumani.Kikundi hiki maalum kinafanya kazi kama jeshi la majini na miongoni mwa kazi zake ni kupambana na ugaidi,kuokoa mateka, kupambana na waasi na kusaidia majeshi mengine katika vita.Kikosi hiki kilitoa mafunzo maalum kwa Jeshi la Polisi la Afghanstan pale Kabul mwaka 2008-2009.
Marinejeger kommandoen wakiwa kazini
Marinejeger Kommandoen wakilinda jengo
# 8 KOMMANDO SPECIALKRAFTE (KSK) (GERMANY)
Kikosi hiki namba 8 kutoka Ujerumani kilianzishwa mwaka 1997 ni kikosi kinachopambana na ugaidi hasa baada ya ugaidi uliotokea mwaka 1972 baada ya wanamichezo wa Israeli walioenda kwenye Olimpiki Ujerumani kushambuliwa na wapalestina. Kina zaidi ya wanajeshi 1,100.
Kommando SpecialKrafte wakiwa jangwani tayari kupambana
Kommando Specialkrafte kazini wakiwa na mbwa wao
# 7 GRUPA REAGOWANIA OPERACYJNO-MANEWRAWEGO (JW GROM) (POLAND)
Kikosi hiki maalum jina lake likimaanisha dhoruba kilianzishwa 13/07/1990 jina lake jingine ni Jednostka Wojskowa 2305.Kikosi hiki kiliundwa ili uwezo wake uendane na vikosi kama SAS (Uingereza),Delta Force (Marekani) na SEAL timu 6 (Jeshi la majini la Marekani). Wanaojiunga na kikosi hiki hujifunza udunguaji, uaskari mwavuli na kufanya kazi ndani ya maji. Kina wanajeshi 448 wakiwa katika vikosi vinne.
Wanajeshi wa GROM katika maandalizi ya kwenda kwenye operesheni.
GROM wakiwa baharini
# 6 ARMY SPECIAL FORCES (GREEN BERETS) (MAREKANI)
Kikosi hiki kimeanzishwa 19/06/1952 na liliundwa kipindi vita ya pili ya dunia inaisha baada ya mapatano ya Warsaw (Warsaw Pact). Kikosi hiki hupambana na ugaidi, kuzuia madawa ya kulevya, kusaka wahalifu hatari waliotoroka jela au waliofanya uhalifu mkubwa kiasi kwamba polisi wakawa wanawahitaji. Ili ujiunge na kikosi hiki inabidi uwe raia halai wa Marekani, umri wa miaka 20-30 tu, uweze kuendesha ndege, uweze kuogelea kwa mbinu tofauti, uwe na uoni mzuri na uweze kutunza siri.Pia uweze kukimbia maili 2 kwa dakika zisizozidi 14, upige pushapu 100 kwa dakika 2 na sit ups 100 nazo kwa dakika 2 ili upate alama 300 zitakazokuwezesha angalau ufikiriwe kujiunga na kikosi hiki.
Green Berets wakifanya mazoezi.
Green Berets akipiga saluti kwa wakuu wake
# 5 JOINT TASK FORCE 2 (JTF 2) (CANADA)
Kikosi hiki maalum kwa ajili ya kupambana na ugaidi kilianzishwa 01/04/1993. Kikosi hiki kina kambi yake katika kilima cha Dwyer Ontario, Ottawa na kitahama mwaka 2019 kwenda CFB Trenton. Kilishafanya kazi nzuri kipindi cha mauaji ya kimbari Rwanda (1994), vita ya Bosnia, vita ya Kosovo, maasi ya Haiti, Afghanistan (2001-2012) na Iraq (2006). Kikosi hiki hutumia bunduki aina za Heckler na Koch MP5A3 na magari ya Jackal MWMIK.
Wanajeshi wa JTF 2
Askari wa JTF 2 akiwa katika Jackal
# 4 SPETSNAZ GRU (URUSI)
Hiki ni kikosi maalum cha kwanza kuanzishwa nchini Urusi mnamo mwaka 1949 wakati vita ya pili inamalizika. Wazo la kuanzishwa kwa kikosi hiki lilitolewa na Mikhail Svechnykov mwaka 1938. Malengo yake ni kuilinda kiintelijensia Urusi,
Askari wa Spetsnaz GRU wakifanya mazoezi
Spestnaz GRU wakiwa tayari kwa operesheni maalum
# 3 SAYERET MATKAL (ISRAELI)
Kama ujuavyo mpenzi msomaji Israeli kwa upande wa ulinzi na usalama wanaongoza duniani na wote hatutosahau kikosi maalum kilivyofanya shambulio la Entebbe. Kikiwa kimojawapo kati ya vikosi kama Kidon, Sayeret, Shayetet 13, Sayeret Shaldag, Sayeret Duvdevan, Sayeret Yahalom, Unit 669 na YAMAM pia kikosi hiki kinajulikana kama The Unit. Kilianzishwa mwaka 1957 na kipo chini la jeshi la ardhi la Israeli. Hufanya intelijensia kwa maadui wa Israeli, hupambana na ugaidi na kuokoa mateka. Liliundwa likifuata mfumo wa jeshi la Uingereza la Special Air Service (SAS). Lilifanya kazi nzuri wakati wa vita ya Yom Kippur, vita ya Lebanon (1982, 2006), Intifada I na Intifada II. Baadhi ya makamanda wake ni Ehud Barak, Yonatan Netanyahu, Nehemiah Tamari na Moshe Yaalon.
Sayeret Matkal wakiwa na binti anayependa kazi zao.
Sayerek Matkal wakiwa tayari kwa kazi
# 2 1st SFOD-D & DEV GRU (UINGEREZA, NEW ZEALAND & AUSTRALIA)
1st Special Forces Operational Detachment-Delta au kifupi DELTA FORCE jina ambalo hata mcheza filamu nguli Chuck Norris alishawahi kuigiza sehemu 3 za filamu (kama umeshawahi kuzitazama).Chuck alifanya mission za kupambana magaidi na wauza madawa ya kulevya. Ndivyo pia kikosi hiki hufanya kazi.DEV GRU ni kifupi cha maneno DEVelopment GRoUp ambao hufanya kazi kama kikosi maalum cha kijeshi cha wanamaji
SFOD DEV GRU 1 wakiwa hawapo vitani
1st Special Operational Forces Detachment-Delta (1st SFOD-D) wakijipanga
# 1 Special Air Service (SAS) ,New Zealand SAS na Special Air Service Regiment (SASR)
Vikosi hivi ni vya Uingereza (SAS), New Zealand na Australia (SASR) hivi ndivyo vikosi bora namba moja duniani kwa mbinu kali na mafunzo ya hali ya juu. Pia hutengewa bajeti kubwa na kushiriki kwenye operesheni ngumu na hatarishi kama vita ya Vietnam, Afghanstan, Somalia, Timor ya mashariki na hata kupambana na ISIS na ISIL.
SAS,SAS NZ na SASR wakiwa katika utayari wa kwenda vitani
SAS wakiwa vitani