Viko wapi Vyuo vikuu vya Afrika/Tanzania?

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Tarehe 29 Februari mwaka 1969 Mwalimu Nyerere akiwa anatoa hotuba huko chuo kikuu cha Liberia , Monrovia alisema yafuatayo juu ya vyuo vikuu vya Afrika , nanukuu

"Afrika tunahitaji ukweli kutoka vyuo vyake vikuu. Tunapambana na matatizo mapya, na tunahitajio ujuzi wote unaoweza kupatikana katika kuyatatua.Lakini vile vile vyuo vikuu lazima viwe vyombo vilivyojitoa kutumikia Taifa;vijitoe katika kutafuta maendeleo ya Nchi zetu.Lazima vitoe huduma ya kizalendo, na kwa sababu hiyo itakuwa huduma ya kweli na ya moyo"

Ukiangalia maneno haya ya Mwalimu na ukalinganisha na Maprofesa wetu na wasomi wetu wa leo utaionea huruma Afrika , kwani hawa wameigeuka Afrika na wamekuwa ndio wanatumiwa na watu wenye malengo yao katika kuhakikisha kuwa Afrika inaendelea kudhoofu.

Hii inatokana na ukweli kuwa wasomi wetu badala ya kufanya tafiti aqmbazo zitaweza kutolea majibu changamoto zetu wamekuwa wanawasubiria watu wa Benki ya Dunia, IMF, NEPAD n.k waje na miradi yao ya majaribio na wao ndio wanakuwa wa kwanza kuzishawishio nchi zetu kukubali m,iradi hiyo ya majaribio huku uchumi na rasilimali zetu zikiendelea kudhulumiwa .

Unafikiri wasomi wwetu wanapaswa kufanya nini ili kurudi kwenye kauli ya Mwalimu?
 
Hivi uzalendo huwa unafundishwa darasani, unarithiwa au ni innate hivi (yaani naturally tu mtu unazaliwa nao)?

Tukiweza kuwa na jibu la hili basi labda tunaweza kufahamu tufanye(ie) nini wasomi ili kurudikwenye kauli ya Mwalimu
 
Back
Top Bottom