Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,796
- 12,239
Hali ya fedha katika serikali yetu ni mbaya sana kiasi kwamba motisha ya kufanya kazi kwa watumishi wake imeshuka sana kutokana na kukosa vitendea kazi nyeti na muhimu.
Hii si sawa kabisa!
Wana JF naomba tujadili!
- Ukitembelea ofisi nyingi za serikali watumishi wengi wanapiga soga na kusubiri muda wa kuondoka.
- Mahakamani kesi nyingi ama hazijaanza kusikilizwa au zimeahirishwa kutokana na ukata(Rejea maelezo ya jaji mkuu kwa JK siku ya mahakama)
- Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wamekosa mikopo kwa kuwa serikali haijapeleka fedha.
- Wakandarasi wengi wamepunguza kasi ya kujenga miradi mbalimbali kwa sababu ya kutolipwa madai yao kwa wakati.
- Madaktari interns waligoma kwa kucheleweshewa posho zao za miezi miwili.
- Halmashauri nyingi za wilaya hazijapelekewa fedha za maendeleo kwa takribani miaka miwili.
- Orodha ni ndefu sana!
Hii si sawa kabisa!
- Bunge lina vikao vinne (4) kwa mwaka ambavyo huchukua miezi takribani minne(4) ( Kikao cha bajeti miezi 2 na ushee, Kikao cha Novemba wiki 2, Kikao cha Februari wiki 2 na Kikao cha Aprili wiki 2). Vikao vyote hivi hufanyika Dodoma.
- Vikao vya kamati za bunge ambavyo havina muda maalumu ambavyo hufanyika kabla na baada ya vikao vilivyoorodheshwa hapo juu. Vikao hivi hufanyika Dar es Salaam.
Wana JF naomba tujadili!