Gashu -mwanamke
Sister duu nonino -mwanamke
Mzula -kofia
Mbangu, njagu, pongo -polisi
Denglizi -jeans.
Mtu akiwa haeleweki machepele flan aliitwa chale wakimfananisha na yule mchekeshaji Charles Chaplin.
Mtu ambae kachanganyikiwa kidogo aliitwa kipindi cha michezo RTD waqt huo kilikuwa saa mbili kasorobo sasa badala ya kusema mbili kasoro.
Kulikuwa na vijimisemo enzi zile nikivikumbuka, huwa vinanipa burudani. Vijimisemo kama ''Utabana ngenge - wakimaanisha utakoma! ,du kinaa - yaani hakuna shida, dole tupu - yaani powa tu!! Unakumbuka vimisemo vipi, hebu tupia hapa tukumbushane!!