'Vijimambo vya Mliberia'-Ameaga Kwao

'Vijimambo vya Mliberia'-Ameaga Kwao

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Kpah Sherman ameikataa jezi namba 25 iliyokuwa ikivaliwa na Emmanuel Okwi.

Sherman raia wa Liberia, alikabidhiwa jezi hiyo namba 25 iliyokuwa ikivaliwa na Mganda huyo wakati akikipiga Yanga.


Taarifa zimeeleza kuwa Sherman amepewa jezi namba 9 ambayo aliitumia Danny Mrwanda tokea ametua Yanga siku chache zilizopita na straika huyo wa zamani wa Simba na Polisi Moro, atapewa jezi nyingine.


Sherman aliitumia jezi hiyo mazoezini na baadaye katika mechi dhidi ya Simba ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-0.


Haikuelezwa wazi sababu ya Sherman kuikataa jezi hiyo lakini taarifa nyingine zimesema anaona haina bahati na ana mapenzi na namba 9 aliyokuwa akiitumia barani Ulaya.
 
sijaelewa hiyo picha ya watoto ina uhusiano gani na Maximo
 
Cha ajabu hata hao wachezaji wanaowapiga wenzao miiba wala hawafanikiwi!!! ama kwel ukistajabu ya mussa atayaona ya filauni.
cc: Mohamed Simba Banka
 
Back
Top Bottom