Tango73
JF-Expert Member
- Dec 14, 2008
- 2,173
- 1,288
Miaka 56 baada ya uhuru, shule za chekechea zimekuwa adimu sana vijijini na wala hazionekani kabisaa. Mbali na hayo yoye, maktaba za kujisomea na kuazima vitabu hazifikiriwi kabisaa kujengwa vijijini mahali ambako 71% ya watanzania waitwao wakulima walikojiwekea makazi ya kudumu. Swali la kujiuliza, hivi hawa wabunge ambao wengi wao siku hizi ni wahitimu wa chuo kikuu, hawalioni tatizo hili? Hivi hata hawa viongozi wa dini wasemao hivi sasa Tanzania maisha ni mazuri, kwa nini hawagusii swala la shule za chekechea na ujenzi maktaba vijijini? Mbunge bora ni yule aliyepeleka maktaba na shule za chekechea vijijini kwake na wala sio kuongea sana bungeni.. kama serikali ina uwezo wa kumnunulia kila mbuge gari na kumlipia dereva, je inashindwaje kujenga hata shule za chekechea katika majimbo ya watokayo wabunge? Jamani maktaba na shule za chekechea ni bora sana katika kuelimisha na kupanua misuri ya elimu hapa nchini.