Vijijini hakuna shule za chekechea wala maktaba-maendeleo yapo wapi?

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
2,128
1,225
Miaka 56 baada ya uhuru, shule za chekechea zimekuwa adimu sana vijijini na wala hazionekani kabisaa. Mbali na hayo yoye, maktaba za kujisomea na kuazima vitabu hazifikiriwi kabisaa kujengwa vijijini mahali ambako 71% ya watanzania waitwao wakulima walikojiwekea makazi ya kudumu. Swali la kujiuliza, hivi hawa wabunge ambao wengi wao siku hizi ni wahitimu wa chuo kikuu, hawalioni tatizo hili? Hivi hata hawa viongozi wa dini wasemao hivi sasa Tanzania maisha ni mazuri, kwa nini hawagusii swala la shule za chekechea na ujenzi maktaba vijijini? Mbunge bora ni yule aliyepeleka maktaba na shule za chekechea vijijini kwake na wala sio kuongea sana bungeni.. kama serikali ina uwezo wa kumnunulia kila mbuge gari na kumlipia dereva, je inashindwaje kujenga hata shule za chekechea katika majimbo ya watokayo wabunge? Jamani maktaba na shule za chekechea ni bora sana katika kuelimisha na kupanua misuri ya elimu hapa nchini.
 
Wewe kwa umri wako umejenga chekechea ngapi zaidi ya kubwabwaja tu kwenye mitandao ya kijamii?
hili swali ungemuuliza aliyetangaza kwamba "tanzania itabadilika muda si mrefu". vijiji vingi tu ukiuliza chekechea ni nini, hawajui hata maana. na hapohapo wizara hiyo inasimamiwa na prof. na mtihani wanaopewa watoto ni uleule tz nzima. hata hivyo sisi watoto wa vijijini tuna akili sana kuweza kuwashinda hata hawa wa mjini?

binafsi katika somasoma yangu, nilitoka kijijini, hata likizo nikirudi dafftari natupa huko, lakini nikija shule naongoza darasa. sijawahi kusoma tuition miaka yangu yote sita, lakini nilikuwa nawaburuza wanaotoka dsm na mijini ambao walikuwa wanasoma tuition. walikuwa wananikera tu kwenye mtihani wanavyotazamia kwangu na kuwakatalia naogopa kwasababu wameshanipatia sukari ya kwenye uji ambayo mimi wazazi wangu hata hawakuwa na uwezo kununua.
 
Back
Top Bottom