Vijana wenzangu tufanye mazoezi, lift zina wakati wake!!

HARRISON ONE

Member
Jan 8, 2014
42
30
Nipo hoteli moja hapa dar es salaam maeneo ya sinza!!chumba nilichopo kiko ghorofa ya tatu tu!!! asubuhi hii natoka chumbani nikijiandaa kwenda restaurant ambayo iko ground floor!!!

Kuna jambo lilinishangaza kidogo!!! kwenye mlango wa lift kulikuwa na vijana kama watano hivi wenye umri wangu around 27-35 hivi full vitambi!!! mmoja hadi mgongo unapinda kwa kunenepa bila mpangilio!!!wanasubiri lift iliyokuwa upper floor hadi ishuke!!!hadi mimi niliyetumia ngazi za kawaida ambazo hazikunichukua hata dk mbili hadi kufika ground floor.

Zilipita dakika kama kumi hivi nao ndio wakawa wanafika chini na lift yao!!!

Sasa najiuliza kwa shape walizokuwa nazo kwanini wasitumie ngazi za kawaida kwa floor tatu kama hizo!

Vijana wenzangu tupende mazoezi tusibweteke!
 
Ndiyo maana maradhi hayaishi kuwasumbua kwa kupenda kujipweteka kiasi hicho.
 
Mtu anakaa Goba Matosa atembea kwa mguu tokea Goba mpaka mbezi, akifika Mbezi apande daladala kuanzia Mbezi mpaka Posta kasimama. akishuka hapo kiuno chote kimeishapinda...

halafu unataka apande ngazi wakati lift ipo?


MUWAACHE WAPUMUE....
 
Huwezi jua labda wameshafanya mazoezi yao chumbani ama usiku kucha walikuwa na mazoezi.... just kidding, you have a point. ungewachoraa tuu
 
Kuna sehem nimekuta vijana wanapanda lift hata floor ya pili. Nilishangaa sana. Tena ni vijana wa chuo.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Ni kweli sasa hivi hili ni janga.Unakuta mtu ni wa around 28-35 years old amenenepa sana hata kutembea ni shida.Kama kijana huna muda panga muda wa kuhudhuria gym za kisasa.Tatizo ni life style ya sasa tofauti na wazee wetu ambapo miili yao ni imara sana,unakuta kijana muda wote kuendesha gari,ofisini muda wote ac,bar feni,bia na red mnyama,nyumbani kufika na kuangalia tv,then chumbani kulala ac inapuliza mpaka asubuhi,mlo wa mchana take away kutoka supermarket,hakuna mazoezi hata walau kwa siku kutembea,ukikutana naye hadi huruma,muda si mrefu utasikia kisukari,pressure,kukosa nguvu za kiume n.k.ndo maana hata mitaani kuna waganga wengi wa kienyeji,TUBADILIKE KWA KUSHUGHULISHA MIILI YETU.
 
Back
Top Bottom