Vijana wenzangu hakika nawaambia kupitia hili nimejifunza....

Wanaume tunafanya makosa sana kutaka wake zetu wawe sawa na mama zetu. Hicho ni kitu kisichowzekana in a practical world.

Kwa mfano mimi na Marianah tunaishi kwa kubebeana mapungufu yetu. Kamwe siwezi mlinganisha na mama yangu naye hawezi nilinganisha na baba mkwe wangu.

Ni lazima tuelewe kwamba kila mmoja ana tabia zake vilevile makuzi ya mama zetu si makuzi ya wake zetu. Ukikosa ufahamu wa haya mambo ndoa yako lazima iwe jehanam ndogo.
 
Jana nimeamka asubuhi nikatafakari kwa kina sana juu ya maisha haya. Kubwa zaidi ni namna aliyewahi kuwa mpnz wangu aliponishambulia sana kuwa nimempa pesa kidogo,(aliniomba 150,000/= lakini mimi nilimpatia 100,000/=) kwa sababu nilikuwa najua kabisa kuwa ana pesa yake nyingine nyingi tu,kwa hiyo nikafanya jaribio la makusudi kuona reaction yake ingekuwaje baada ya kumpa kiasi pungufu na alichokiomba!

Lahaulaaa,lawama nilizopokea sasa....,"haujali shida zangu, najua unanikomoa, sawa,ila kumbuka mimi ni mke wako mtarajiwa,kama leo hii unashindwa kunisaidia 150k,sijui huko baadaye itakuwaje"

Nilipomaliza kusoma meseji nilivuta pumzi nikazifuta zote,nikajisemea moyoni,kuwa huyu hanifai kabisa....(na ndiyo ukawa mwisho wa mimi na yeye,japo mpaka sasa sijamwambia chochote)

Kilichofanya nije hapa ni baada ya kuamua kumtumia mama yangu mzazi kiasi cha sh.ELFU HAMSINI TU YA MATUMIZI,maombi niliyopokea hakika niliumia sana moyoni,sanaaa,kwamba mpenzi wangu nilimtumia sh.LAKI MOJA akaishia kunilaumu na kunisema sana,lakini mama yangu nimemtumia sh.50k shukrani alizotoa ni nzito sana! Hii imeniongezea hasira juu ya wanawake wasioridhika na kingi tunachowapatia,ilhali wazazi wetu wanapata kidogo na bado wanashukuru kweli kweli!

Haya ni maombi ya mama baada ya kutumiwa kiasi kidoogo sana cha pesa
Vijana wenzagu,tuwakumbukeni wazazi wetu wana baraka nyingi sana kwetu
View attachment 1206408
Nimependa walivyoimba. Kikundi chao kinaitwaje? Nisaidie tafadhali.
 
Mkuu umenikumbusha nilikuwa na mwanamke mmoja mama yangu alikomaa na mm nimuoe,alikuwa jobless kwa hiyo tukikubaliana nimsapoti laki kila mwezi.
Nikatuma mwezi wa Kwanza hakusema asante Wala nimepata.Sikumuuliza kabisa
Mwezi unaofata nikashusha dau kufika 50,000 akaniambia mbona Umetuma nusu?
Nikamwambia Kumbe na ile nyingine ulipata Kwanini hukusema japo Asante ya kinafiki?akanijibu"yani Unaona hiyo hela ni nyingi kwamba ntajengea nyumba Ndio maana nikushukuru?"nikapiga tigo wakanirudishia na tukaishia pale pale.
Hii habari ilitakiwa iwe ya kwanza kabisa katika huu uzi ili mawatu yajifunze hekima.
 
Wanaume tunafanya makosa sana kutaka wake zetu wawe sawa na mama zetu. Hicho ni kitu kisichowzekana in a practical world.

Kwa mfano mimi na Marianah tunaishi kwa kubebeana mapungufu yetu. Kamwe siwezi mlinganisha na mama yangu naye hawezi nilinganisha na baba mkwe wangu.

Ni lazima tuelewe kwamba kila mmoja ana tabia zake vilevile makuzi ya mama zetu si makuzi ya wake zetu. Ukikosa ufahamu wa haya mambo ndoa yako lazima iwe jehanam ndogo.

Ni kweli mkuu ila kuna kitu kinaitwa "maadili" mwanamke asiyeweza kushukuru hafai kuwa mama bora. Na hapo ndipo msingi wa wadau wengi ulipo kuwa na 'shukrani'

Ni kweli hatutakiwi linganisha 'care' ya wazazi wetu kwetu na ya wapenzi wetu kwetu. Ni vitu ambavyo kamwe haviwezi lingana

Ila "maadili" tunaweza linganisha ili tuchague yaliyo bora kwetu na kwenye jamii.
 
Hongera sana kwa kugawana na mama zaidi!
Mimi huyu nilikuwa ready kumhudumia kwa sababu psychologically nilishaanza kumfanya mke wangu wa siku chache sana zijazo,ila kumbe naye mpuuzi tu
Kwahiyo jimbo lipo wazi mkuu ,watu tugombee u mother house to be?, ila huyo Dada kazingua, ilibidi akushukuru sana ukiomba kitu kuna kupata au kukosa yeye kaomba 150 kapata 100 analalamika ,ungemwambia airudishe ili ujipange umtumie 150 afu usimtumie kabisa aargh
 
Sasa utampaje hela wakati haujamuoa!! Hilo ni kosa.Hiyo ni sawa na hongo ili akubali ombi lako la kumuoa na hapo ndipo wanaume tunafeli.

Ni sawa na kurusha jiwe gizani.Tazama sasa pesa zako nyingi amekula na haujamuoa!!! So painful mkuu.

Hata kama ana mipango ya MAENDELEO(kumpa mtaji) usimpe mpaka utakapo muoa.

Zamani mabinti walikataa pesa ya mwanaume kabla ya kuolewa but siku hizi ni tofauti.

Fanya hivyo kwa wanawake unaowataka kimwili tu na isiwe pesa mingi kiasi hicho labda angalau 10k- 17.8k sio mbaya WHY? Coz mwanamke mwenye akili atakuona wewe hauna mpango wa kumuoa na ataanza kukupiga mizinga tu na siku ya mwisho mtaachana.
Hahahaaaa kwa mke mtarajiwa unatoa tu mbona
 
Kwahiyo jimbo lipo wazi mkuu ,watu tugombee u mother house to be?, ila huyo Dada kazingua, ilibidi akushukuru sana ukiomba kitu kuna kupata au kukosa yeye kaomba 150 kapata 100 analalamika ,ungemwambia airudishe ili ujipange umtumie 150 afu usimtumie kabisa aargh
Mwaka mzima umeenda bure tu,wakati target yangu yote ilikuwa kumalizana na ubachela kabisa
 
Ni kweli mkuu ila kuna kitu kinaitwa "maadili" mwanamke asiyeweza kushukuru hafai kuwa mama bora. Na hapo ndipo msingi wa wadau wengi ulipo kuwa na 'shukrani'

Ni kweli hatutakiwi linganisha 'care' ya wazazi wetu kwetu na ya wapenzi wetu kwetu. Ni vitu ambavyo kamwe haviwezi lingana

Ila "maadili" tunaweza linganisha ili tuchague yaliyo bora kwetu na kwenye jamii.
Mkuu. Kama mchumba wako mtarajiwa hana tabia ya kushukuru anza kumfundisha kwa matendo.

Ukisema umkimbie utaenda kukutana na bedwetter. Utakimbia utaenda kukutana mlozi. Utamkimbia utaenda kukutana na hasiyejua kupika.

Ni lazima ifike mahali tujifunze kuwakubali wenzetu na kuanza kuwa shape katika hali au mtazamo ambao tungependa wawe nao.
 
Sasa utampaje hela wakati haujamuoa!! Hilo ni kosa.Hiyo ni sawa na hongo ili akubali ombi lako la kumuoa na hapo ndipo wanaume tunafeli.

Ni sawa na kurusha jiwe gizani.Tazama sasa pesa zako nyingi amekula na haujamuoa!!! So painful mkuu.

Hata kama ana mipango ya MAENDELEO(kumpa mtaji) usimpe mpaka utakapo muoa.

Zamani mabinti walikataa pesa ya mwanaume kabla ya kuolewa but siku hizi ni tofauti.

Fanya hivyo kwa wanawake unaowataka kimwili tu na isiwe pesa mingi kiasi hicho labda angalau 10k- 17.8k sio mbaya WHY? Coz mwanamke mwenye akili atakuona wewe hauna mpango wa kumuoa na ataanza kukupiga mizinga tu na siku ya mwisho mtaachana.
Preeeeeaaaaaach
 
Back
Top Bottom