Vijana wazalendo watoa tamko

Robethn

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
2,103
352
TANZANIA TUITAKAYO VIJANA ipo mikononi mwetu vijana.

Ni jukumu letu mimi na wewe MTANZANIA mwenzangu kuhakikisha tunaipata Tanzania Tuitakayo kwa kupiga kura za ndio kwa kiongozi muadilifu na mchapa kazi pasipo ushabiki na kubuluzwa na wale wote wenye uchu wa madaraka na makandokando mengi.

Tusikilize sera za pande zote kwa makini na tutafakari kwa kina ni vipi zinatekelezeka!

Tusidanganyike vijana wenzangu tukaiuza nchi yetu tukufu kwa vielfu kumi kumi na nwisho tukaiweka rehani nchi yetu tukufu!

Itakua ni dhambi kubwa sana isiyosameheka tukipiga kura za ndio kwa kiongozi asiye na sifa na nidhamu ya UONGOZI!
Ee Mtanzania mwenzangu, tafakari, chukua HATUA

MUNGU IBARIKI AFRICA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Naomba kuwasilisha!
 
Kura yangu kuanzia udiwani mpaka uraisi ni kwa ukawa, sihitaji ccm tena. Baada ya miaka kumi nitapiga kura tena kuweka chama kingine. Hukuna chama kudumu madarakani
 
Tamko la vijana wa wapi hilo?

Baada ya maccm kuzidiwa kila mwanaccm anaandika upuuzi
 
lowasa ndo habari ya mjini,ccm washatufungia kwenye umaskini kwa mda mrefu,mnataka tuongeze tena na makufuli?? Hebu pumzikeni ccm mmeshindwa kusimamia raslimali za nchi na pia kutekeleza ilani yenu,habari ya mjini ni "mabadiliko" nje ya ccm
 
Mwadilifu ni lowassa aliyekubali kujihudhuru kwa ajili ya kuikoa serikali na chama chake.

Tusichague ccm maana wamemaliza tembo wote wameingiza nchi kwenye ufukara na kuwasababishia watanzania maisha magumu yasiyoelezeka

tumeiamini miaka 53 hatuwezi tena kurudia kosa
 
Vijana wengi tumeamua tunataka kuiondosha serikali DHALIMU ya CCM mara hii. Tumechoka na uongo wenu. Munasemaje vijana hapo...
 
Mwadilifu ni lowassa aliyekubali kujihudhuru kwa ajili ya kuikoa serikali na chama chake.

Tusichague ccm maana wamemaliza tembo wote wameingiza nchi kwenye ufukara na kuwasababishia watanzania maisha magumu yasiyoelezeka

tumeiamini miaka 53 hatuwezi tena kurudia kosa

Jana sumaye ktk kampeini za ukawa dodoma kaibua ufisadi wa ujangili ya kwamba kuna report imetolewa kuwa ndani ya siku 14 tembo 30,000 wameuwawa na meno na pembe za hao tembo kukamatwa huko china na Hongkong,mm nadhani kuna ulazima wa kumonitor mwenendo wa wachina hapa nchini
 
Back
Top Bottom