Vijana wasomi wa Kiislamu na Pombe

Vijana wasomi wa Kiislamu na Pombe

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,664
Wakuu naomba mchangie mada hii.

Ni kwamba mara nyingi imetokea vijana wengi wa kiislamu wanapokuwa katika umri wa miaka kabla ya 25 huwa wanashika sana dini kwa maana ya ibada na kufuata nguzo zote za dini ya kiislamu.

Lakini wanapoingia vyuoni na kuhitimu degree zao (elimu dunia) kisha kuanza maisha mambo hubadilika sana. Ile dini waliokuwa wanaifuata kwa kuzingatia masharti yote huanza kuiacha.

Kikubwa wanachokipenda sana ni pombe. Wanabadilika na kuwa walevi sana kushinda walevi wengine.

Hii imekuwa inanisumbua sana chanzo cha haya yote.

JE ni mfumo wa maisha unawazidi kiasi kwamba dini inaonekana ni mzigo ama ni nini?

Nimekuwa najiuliza sana.
 
hiyo hutokea kwa vijana wote siyo waislamu pekee hata wakriso pia.Kitu kinachosababisha ni kuwa marafiki wabaya.Mimi binafsi nlijikuta najaribu kuvuta chaArusha nliambiwa ina boost akili.
 
Hulka ya mtu! ... usiseme vija wote wa kiislam !.....
 
Sijasema vijana wote.......nimesema vijana wengi......
 
Huko Rombo, na maeneo mengine ya Kaskazini kuna vijana wengi walevi tu ni vijana wasomi wa Kiislam?
 
Huko Rombo, na maeneo mengine ya Kaskazini kuna vijana wengi walevi tu ni vijana wasomi wa Kiislam?

hahahahaha kaka ushaanza maanake ww ukija hupigi risasi ya mguu unapiga direct kichwani hahahahaha
 
Naweza kua sina jibu la swali lako sababu labda sijalielewa vizuri. Hii observation au analysis yako uliifanya pia kwa wasomi wa kikristo?

Maana yake naona huko Chuo tunapita wote na hata tukija kukutana baa tunakutana wote pia. Isitoshe tukiwa baa hatuulizanagi dini.

Labda ufafanue zaidi swali lako
 
Ni vijana wote tu. Sio wa kiislamu. Kwa mazingira haya kijana akishika hela kuna wakati kichwa kinapata moto anakosa balance. Akikua anaacha.
 
hiyo hutokea kwa vijana wote siyo waislamu pekee hata wakriso pia.Kitu kinachosababisha ni kuwa marafiki wabaya.Mimi binafsi nlijikuta najaribu kuvuta chaArusha nliambiwa ina boost akili.

Cha Arusha!!!!,bado unakivuta au ulishakiacha?.
 
Mwezi huu ni kipindi kibaya mno kwa wafanyabiashara za bar, na nyumba za kulala wageni

Nikwa sababu wakiristo wanauheshimu mno mfungo huu wa ramadhani.ushahidi ninao marafiki zangu wakiristo wanasema wanaona aibu kunywa pombe mwezi huu hivyo wameamua kuwaunga mkono waislam kwa kutoshiriki pombe na ufuska mwingine.
 
hiyo hutokea kwa vijana wote siyo waislamu pekee hata wakriso pia.Kitu kinachosababisha ni kuwa marafiki wabaya.Mimi binafsi nlijikuta najaribu kuvuta chaArusha nliambiwa ina boost akili.

Ulikuwaje ulivyojaribu :?
 
yap ni kwel ukisemacho lakn hapo mi naona ni kutofuata maamlisho ya alllah na kuiga vitu vya kigeni pia na makundi ya kitwautiii ndo maana wengi waliosoma dini wanapoteaa

lakn pia sheitwan huwa karbu sana na watu ambao wamehifadhi amri za mwenyez mungu ilii awapotezee kabsaaaaa kikubwa hpa ni kuwa na msimamo wa Iman yakooo
usitetereke kwa kitu chochoteee
 
Nikwa sababu wakiristo wanauheshimu mno mfungo huu wa ramadhani.ushahidi ninao marafiki zangu wakiristo wanasema wanaona aibu kunywa pombe mwezi huu hivyo wameamua kuwaunga mkono waislam kwa kutoshiriki pombe na ufuska mwingine.

Sidhani kama sahihi. Mimi ninaishi upande wa 99% waislamu. Baa wateja waliobaki ni wachache wakristu tu! Baada ya sikukuu zinajaa. Huu ndio ukweli. jamani na hao waislamu wanaokunywa pombe ni binadamu kwani mangapi yanakatazwa watu wanafanya? Cha muhimu ni kuwahimiza kufuata vitabu vya Mungu. Imani inakataza kunywa pombe waumini wanajitahidi kutokunywa pombe wale wanaoshindwa ndio basi angalau wanajitahidi kwa mwezi huu na wengine huenda wanapania kuendelea kuacha baada ya mwezi lakini kiubnadamu wanashindwa. Dini zote zina makatazo ya Mungu na tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kuyafuata lakini kiubnadamu now and then tunaanguka na kuinuka.
 
Back
Top Bottom