Vijana wangu msiuache mfumo dume

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Vijana wangu, nawahurumia mno na dunia hii tuliyopo sasa. Mfumo dume si kupiga piga wala kunyanyasa wanawake au kutosomesha watoto wa kike, mfumo dume si kutoa maneno ya udhalilishaji kwa wanawake unapolewa. Mfumo dume ni pamoja na kuheshimu wanawake na kuwalinda.

Mfumo dume ni nini?

Ili maisha yaende ni lazima, hususani katika ngazi ya familia, LAZIMA mmoja ajishushe ili maisha yaende. Na maandiko YOTE matakatifu (kwa mnaoamini Mungu) yameshaweka hili bayana.

Wa kujishusha ni mwanamke, kwa nini? Jibu analo Mungu aliyesema iwe hivyo. Matatizo mengi ya siku hizi yanatokana na kutaka kwa hali na mali kumuangusha mwanaume kileleni kwenye nafasi yake ya mamlaka na utawala.

Ndoa zinavunjika siku mpaka siku, kwa wanawake kutaka kuingilia utawala na mamlaka ya waume zao. Kuchelewa kurudi mpaka kurudi asubuhi, kutopika kwa wakati bila taarifa maalumu, na kuwa mkali ukiulizwa sababu.

Yaani katika maamuzi ya familia mwanamke naye anataka ashiriki 50% zote, khaaa! Hii haiwezekani na haitowezekana, na wanawake hawataki kukubali, wanataka wawe sawa kwa kila kitu ukiacha kuzaa na maumbile tu. Zamani ndoa ilikuwa inaheshimika ila si sasa.

Sio kwamba zamani wazee wetu walikuwa wananyanyasa wanawake kama propaganda za magharibi zinavyosema, si kwamba wazee wetu walikuwa hawajastaarabika na hawana akili, si kwamba wazee wetu walikuwa watu wa hovyo hovyo, hapana!

Wazee wetu walisimama KIKAMILIFU kwenye nafasi zao, na waliweka sheria kali za kuwalazimisha bibi zetu wasimame kwenye nafasi zao, hili ndilo feminists huligeuza na kuliita lilikuwa ukandamizaji kwa jinsia ke, kitu ambacho ni totally wrong.

Walitakiwa waanze kumlaumu Mungu na kumuita mkandamizaji, feminists na wafadhili wa haki sawa hawawafahamu wanawake kama Mungu mwenyewe anavyowafahamu.

Kumlazimisha mwanamke kusimama kwenye nafasi yake kimaandiko, na KITAMADUNI ZA AFRIKA SI UKATILI, NA SI UKANDAMIZAJI. Ni kuinusuru jamii na kizazi cha miaka ijayo, kwani hali hii ya sasa na hili vugu vugu likiendelea, Afrika naiona ikiangamia mbeleni, na rangi nyeusi itatoweka.

Sehemu yoyote yenye ukinzani lazima ugomvi uwepo, angalia rate ya mauaji ya wanandoa dunia hii ya sasa, angalia namna vijana wa kiume wanaozaliwa, wanavyokosa maadili ya kiasili ya mwanaume wa kiafrika?

Angalia misemo ya kishetani inayokua kila siku? 'Hakuna anachoshindwa mwanamke, anaweza kufanya kama mwanaume na zaidi', ni ushenzi.

ITOSHE KUSEMA AFRIKA TUMECHEZEWA SANA NA HAWA WA MAGHARIBI, TUMEKOSA KUSIMAMIA TAMADUNI ZETU ZA ASILI ZENYE KUJALI HESHIMA, UTU, ADABU, UPENDO NA MSHIKAMANO.

TUJIULIZE MBONA URUSI NA CHINA HAWACHEZEWI HOVYO HOVYO? MBONA KUNA UKANDAMIZAJI WA WANAWAKE(KAMA WANAVYOITA WENYEWE), ILA HAWAINGILIWI?

TUAMKE, TURUDIE ASILI YETU, HAKI SAWA NI PROPAGANDA YA KUWANYIMA SAUTI WANAUME WENGI WA KIAFRIKA, HATUPO SAFE, MAUAJI YATAZIDI MNO KWA TREND HII YA SASA. HIVI HAMJIONEI? Tuendelee

Jiulize kwa nini siku hizi majina kama vibamia yamekuwa mengi? Siku hizi wanawake wanatoa siri za waume zao kuliko zamani, unajua kwa nini? Haki sawa! Hii yote ni kuhakikisha jamii inamdharau mwanaume, ikiwemo kumpotezea kujiamini mbele za watu na kwa mkewe.

Hii ni kufanya fadheha alizopata mwanamke na mwanaume apate ili wawe sawa na iwe rahisi kupoteza kujiamini kwake.

Tafadhali, vijana msiache mfumo dume. Maamuzi 98% asikudanganye mtu, unatakiwa uyatoe wewe, mkeo akichelewa kurudi pasi taarifa ni lazima uulize alikuwa wapi, hata kama na wewe ulishawahi kurudi na hakukuuliza. Na akijibu jeuri usisite kumzaba hata vibao(zingatia usimpige mbele ya watoto), huyo ni mkeo una mamlaka naye, una wajibu wa kumuadhibu kwa maslahi mapana ya familia yako. Usimuogope, narudia, usimuogope mkeo, piga makofi mpaka mashavu yawe mekundu.

Akitaka kutoka ni wajibu na haki yako kuombwa RUHUSA, iwe yeye ndio ana kazi, au wewe ndio una kazi. Na kama unaona aendako hakuna tija kwake wala kwa familia, mzuie asiende, kuwa mwanaume halisi wa kiafrika.

Ila wewe huna ulazima wa kuomba RUHUSA, ila mpe taarifa. Ifike wakati hata muda mwingine dada wa kazi anapumzika, anapika mkeo chakula chako, hayo ndiyo maisha yaliyonyooka.

Amkeni, don't be fooled! Hao wanaopigania haki sawa wenyewe hawakubali kupandiwa au kutoa 50% za maamuzi kwa wake zao. Na kwa wanawake, wengi wa aina hii wameshindikana, jeuri na hawana adabu.

Hii haki sawa ni mpango wa kuwaburuza wanaume wajinga ambao ndio wanaonekana kuwa wengi kwa sasa. Shtuka! Unafikiri Biden au Obama wamewapa wake zao 50% za maamuzi? Kila upuuzi wanausukumia Afrika!

Amkeni, hakuna haki sawa, MWANAUME SIMAMA KWENYE NAFASI YAKO, MKEO ANATAKIWA AFUATE AMRI YAKO KWA MAENDELEO CHANYA YA FAMILIA YENU.

WAKATI MWINGINE HAKUNA HAJA YA KUMSHIRIKISHA KILA KITU, ANASHTUKA KITU KIMEFANYIKA TAYARI, PLEASE! USIKUBALI HAKI SAWA, WACHACHE WATANIELEWA HAPA.

Haya, ukikubali sawa ukikataa sawa! Mimi nakwenda.
 
Nakubaliana na wewe 50% ni ushetani ambao lengo lake ni kufanya mwanaume awe useless,

Eti mwanamke awe huru kurudi saa anayotaka?kufanya maamuzi bila ruhusa ya mwaume,nani kasema? ndio maana mauaji yameshamiri sana,wanaume wanaona wakienda kwenye madawati ya jinsia hakuna msaada maana huko ndio wamejazana watendaji wenye akili za Kibeijing,hivyo wanaamua kuchukua sheria mkononi.
 
Hiki ulichokiandika ndio mimi mtupu. Anayetaka abaki,asiye taka safari njema. Siwezi kuingiza mfumo wa maisha ambao unakinzana na mpangokazi wa Mungu. Na hii haijalishi nina hela au sina hela. Kama Mungu alivyo na wivu na mamalaka yake vivyo hivyo Mamlaka yangu kama mume haipaswi kuguswa na kiumbe chochote.
 
Hii ni miongoni mwa sababu kubwa kabisa jamii za kimagharibi kuupiga vita Uislam. Samahanini najua watakuja watu hapa na kusema naleta Udini, lakini hapana sileti udini Bali nazungumzia uhalisia.

Dini hazikubaliani na mambo ya haki sawa. Kila mtu kati ya mwanamke na mwanamme ana haki zake ambazo ni tofauti na haki za mwengine. Na zipo haki za pamoja.



Samahani kwa ntakaowakera
 
Hiki ulichokiandika ndio mimi mtupu. Anayetaka abaki,asiye taka safari njema. Siwezi kuingiza mfumo wa maisha ambao unakinzana na mpangokazi wa Mungu. Na hii haijalishi nina hela au sina hela. Kama Mungu alivyo na wivu na mamalaka yake vivyo hivyo Mamlaka yangu kama mume haipaswi kuguswa na kiumbe chochote.
kila mtu apambanie mamlaka yake
 
Hii ni miongoni mwa sababu kubwa kabisa jamii za kimagharibi kuupiga vita Uislam. Samahanini najua watakuja watu hapa na kusema naleta Udini, lakini hapana sileti udini Bali nazungumzia uhalisia.

Dini hazikubaliani na mambo ya haki sawa. Kila mtu kati ya mwanamke na mwanamme ana haki zake ambazo ni tofauti na haki za mwengine. Na zipo haki za pamoja.

View attachment 2091375

Samahani kwa ntakaowakera
Ni kweli!
 
Anasubiri meno yabaki mawili.
Sasa hapo si tutakuwa tumezeeka wote mkuu! Jeuri ataitolea wapi? Hata akiileta, msingi nitakuwa nimeshauweka, kama ni watoto watakuwa wameshakua na nitakuwa nimeshawatengenezea future, kifupi wajibu wangu nitakuwa nimetimiza kwa 90%
 
Naunga mkono hoja walaqhi', wanaume wajitahidi kubaki kwenye nafasi zao, uanaume umechezewa sana hivi sasa, umedharaulika mno, ile heshima ya kiume imetoweka kwa kasi, nawahurumia mno watoto wetu wa kiume, Mungu atusaidie kiukweli..!
 
Aisee ukimfuatilia Mungu jinsi anavyokomaa kuitetea mamlaka yake unajifunza kwamba hata Samia yupo sahihi kabisa kudeal na wote wanaomkwamisha au kumuhujumu.
Hutakiwi kuwa na huruma kumuadhibu yeyote anayeonesha dalili za kukunyang'anya mamlaka YAKO. Mwanamke anatakiwa kuheshimiwa si kuonewa huruma, ni kama masikini, masikini hasaidiwi. In Taikon wa Fasihi voice.
 
Naunga mkono hoja walaqhi', wanaume wajitahidi kubaki kwenye nafasi zao, uanaume umechezewa sana hivi sasa, umedharaulika mno, ile heshima ya kiume imetoweka kwa kasi, nawahurumia mno watoto wetu wa kiume, Mungu atusaidie kiukweli..!
Mashoga ndio usiseme, yanakuja kwa kasi sana! Yaani heshima ya mwanaume hailsi inapungua kwa kasi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom