Vijana wa target group waliojiajiri kwa ufadhiri wa NEOLIFE imeandaa semina ya vijana kuhusu ujasiriamali na kipato

robert_k

Member
Sep 27, 2019
42
19
Hello. Katika kila ngazi kuanzia ya kifamilia hadi kitaifa, kijana ni mtu muhimu sana. Kwanza kwa sababu ni umri wa mtu mwenye nguvu na pili ni umri wa kufanya maamuzi sahihi ili baadae uzeeni ufurahie mapambano yako

Kwa kuliona hili, vijana wa target group waliojiajiri kwa ufadhiri wa NEOLIFE imeandaa semina ya vijana kuhusu ujasiriamali na kipato. Wewe kijana ambaye uko katika ajira na unataka kutengeneza kipato, vile vile wewe kijana ambaye huna kazi, mimi naomba niseme tu wazi HAKUNA KITU KIBAYA DUNIANI KAMA KIJANA ALIYEFIKIA UMRI WA KUPAMBANA NA YUPO HANA KAZI, ni jambo mbaya sana. Akili iliyolala ndio mwanzo wa fikra mbovu, karibu kijana ukutane na vijana wajasiriamali maarufu nchini walioanza biashara zao kidogo kidogo na sasa wako.mbali. Utakutana na vijana walioanza kujiajiri wakiwa shule na pindi walipomaliza wakaendelea na maisha yao ya ujasiriamali

Kama kijana mwenye kuandaa malengo mazuri ya mwaka 2020 hii semina sio ya kukosa. Tutajadili ujasiriamali wa vitu vya kawaida sana ambavyo vinahitajika na jamii yani consumer goods. Sio kuhusu kiwanda, sio kuhusu kampuni ni kuhusu kuanza na consumer goods hizi hizi hadi unakua kwenda ngazi ya juu ya kiwanda huko.

Siku ni jumamosi ya 19th oktoba 2019 pale kituo cha ITV, jengo la NEOLIFE. Karibu sana kijana, wanenaji wa panel mbali mbali ni hawa hawa vijana wenye makampuni, viwanda, tv stasheni, wakulima na wafugaji wakubwa. Pia kutakuwa na mada muhimu sana UMUHIMU WA SOCIAL MEDIA KATIKA BIASHARA YA KIJANA, tusidharau nguvu ya mitandao ya kijamii katika kujitangaza kibiashara kama kijana. Mwisho kutakuwa na kamchezo kafupi cha kufikirika kwa watakaowahi, unaweza kuongoka na zawadi. Tutashiriki chakula cha mchana pamoja na kupata nafasi ya kupiga story na kijana yeyote aliyefanikiwa katika sekta yake aliyopo, kuna walioanzisha app kubwa tu zinazofahamika, kuna wenye makampuni ya fashion vijana tu chini ya 40yrs, kwa nini usiwe we. Karibu sana sana

Semina ya kufunga mwaka, semina inayolenga kuleta changamoto mpya katika maisha ya vijana wa kitanzania hasa katika dhana ya ujasiriamali. 19th oktoba 2019, karibuni. Kwa mawasiliano ya kuweka nafasi yako katika semina hiyo ili itusaidie katika bajeti piga 0766317197/0693307877
 
Back
Top Bottom