Vijana wa Tanzania tunajifunza nini kuteuliwa kwa Waziri Mkuu wa Ufaransa mwenye miaka 34?

Anasahau vingi Salim Ahmed Salim aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri akiwa na umri wa miaka 19

Kichwani ndiko huamua sio porojo
Acha uongo wako wewe .Salimu alikuwa na miaka 22 alipoteuliwa kuwa Balozi nchini misri.hata hivyo kwa zamani wakati wa Nyerere vijana wengi walipewa majukumu makubwa kwa kuwa walikuwa wasomi wachache ukilinganisha na sasa.ba hata vijana walipopewa nafasi walionyesha uwezo mkubwa sana wa kiuongozi. Vipi kwa sasa? Wanaweza wakapewa nafasi za juu na wakamudu Vyema majukumu yao? Wanaaminika kwa jamii? Wanaweza wakawaunganisha Watanzania?
 
Mbona Africa imetoa Marais wengi vijana kuliko huyo, hakuna jipya hapo
Nazungumzia Tanzania na siyo Afrika.kumbuka kwa Tanzania kijana wa miaka hata 39 haruhusiwi kugombea urais kwa kuwa katiba yetu inasema ili ukidhi vigezo vya kugombea urais ni lazima uwe na miaka 40 na kuendelea huko.
 
Lucas ni mtu mkubwa sana, we ni mtu mojawapo ktk wale mitume 12 wa Yesu. Lucas hiyo ni bahati na fursa tu, coincidental event. Baba wa Taifa letu ktk umri huo alikuwa mtu mkubwa sana, hatuna cha kujifunza ila tu tumpongeze
Ni kweli wakati tunapata uhuru vijana wengi waliokuwa na elimu walipewa na kushika nafasi kubwa sana serikalini.lakini kwa sasa hakuna kijana anayeweza kugombea Urais hapa nchini akiwa chini ya umri wa miaka 40, kwa kuwa katiba yetu inasema ili ukidhi vigezi vya kugombea urais ni lazima uwe na miaka kuanzia 40 na kuendelea. Kwa hiyo hapo unaona kuwa vijana wana fursa ya kumchagua Rais ila siyo kuchaguliwa katika nafasi hiyo haya wakiwa na umri wa miaka 39 na miezi 11
 
Uchawa wa Luka ni mbaya sana hebu tazama anavyojitoa ufahamu ktk thread zake na hapo hajala hata 100 piga hesabu kapewa kacheo si atakuwa the so called Zombified mummy?
Hapana ndugu yangu mimi ni mzalendo na sifanyi kazi kwa ajili ya malipo au kulipwa fadhila.
 
Viongozi wetu wanahusuda na wivu vijana wanaopewa nafasi ni vijana wao na wanawafunda uhuni wao ndio maana taifa lina vijana ambao hatuoni mabadiliko vijana wenye uwezo wanaojitosa kwa nguvu zao wanafilisiwa wanapewa kesi za ajabu ajabu wametengenezewa chuki kwa wananchi maadamu mapinduzi ya upuuzi wao uendelee si jambo rahisi kumpata kijana atakayeleta mabadiliko ktk taifa letu mathalani mmojawapo aasi upuuzi wa watangulizi wake

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani huku Tz vijana wenye miaka 34 hawapo? Wewe twambie huyo jama wa Ufaransa kabla ya hapo, alikuwa na cheo gani?
 
Vijana wenye makdirio ya umri huo katika nchi yetu wengi bado wanajitafuta walichofanikiwa ila wanandoto kubwa wakisapotiwa na kuaminiwa wapo wenye uwezo wa kuwa waziri mkuu hata kuwa raisi wa nchi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Emmanueli Macron amemteua Gabriel Attal kuwa waziri mkuu wake, kijana mdogo kabisa katika Historia ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 aliyezaliwa tarehe 16 march 1989.

Je vijana wa kitanzania tunajifunza nini katika uteuzi huo wa kijana mdogo kabisa aliyeaminiwa kuwa waziri mkuu katika Taifa kubwa kabisa na lenye historia kubwa kabisa barani ulaya na Duniani kwote? Ikumbukwe hata Rais Macron alitwaa madaraka ya Urais akiwa na umri wa miaka 39.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Malizia waziri mkuu Punga
 
Vijana wenye makdirio ya umri huo katika nchi yetu wengi bado wanajitafuta walichofanikiwa ila wanandoto kubwa wakisapotiwa na kuaminiwa wapo wenye uwezo wa kuwa waziri mkuu hata kuwa raisi wa nchi
Nashukuru kwa mchango wako.lakini kumbuka ya kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ili uwe Rais au kugombea urais ni mpaka ufikishe miaka 40. Kwa hiyo vijana hawawezi kuchukua Fomu ya Urais au kumchangia kijana mwenzao kuchukua Fomu ya Urais maana katiba imewafunga mikono.
 
Back
Top Bottom