Vijana wa Mwema waua tena

ketwas

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
212
36
JESHI la Polisi limeingia katika kashfa nyingine tena, baada ya askari wake kuwaua kwa risasi watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa katika vurugu zilizozuka wakati wa jaribio la kuwaondoa wananchi wanaodaiwa kuvamia eneo la Nyamongo la mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Africa Barrick.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa mauaji hayo akisema watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi za moto na mmoja kujeruhiwa majira ya jioni juzi katika mapambano baina ya polisi na wananchi waliokadiriwa kuwa kati ya 800 na 1000.
Kamugisha alisema katika tukio hilo, askari polisi mwenye namba E.6059 D/CPL Julius alikatwa panga usoni na kupata majeraha mdomoni na mgongoni na kuanguka wakati wakiwaondoa wananchi katika eneo la mgodi.
Kamanda huyo aliwataja waliouawa kuwa ni Paulo Sarya (26) mkazi wa Nyangoto, Kata ya Matongo na Rodgers Mwita (18) mkazi wa Kimusi, Kata ya Nyamwaga, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Alimtaja aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa kulia ni Mseti Chacha (20), mkazi wa Nyamwaga wilayani hapa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Serikali ya wilayani hapa, Nega Marco, alikiri kupokea maiti na majeruhi hao, lakini akakana kujua lolote kuhusiana na polisi aliyedaiwa kujeruhiwa na wananchi.
Marco alisema, miili ya marehemu hao imehifadhiwa chumba cha maiti katika hospitali hiyo na kwamba tayari ilifanyiwa uchunguzi na inasubiri kuchukuliwa na ndugu.
Hata hivyo, ndugu wa marehemu hao, hawakuwa tayari kutoa tamko lolote kuhusiana na mauaji ya ndugu zao wala kujua hatima ya tukio hilo.
Inadaiwa kuwa, wananchi hao juzi walivamia mgodi huo eneo la Gokona na Rampad uliopo katika vijiji vya Kewanja na Nyangoto wakitaka kupora dhahabu.

source tanzania daima
 
Serikali inayowageukia Wananchi wake, hata wa Vijijini, na Kuwapiga Risasi ambazo zimenunuliwa kwa kodi wanazokatwa Wananchi hao, Haistahili tena kuwaongoza wananchi hao.
 
Back
Top Bottom