Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 61,980
- 127,433
Fanya ufanyavyo,bisha ubishavyo....heshima ya mwanaume pesa. Hata kama hujazipata walau uonyeshe juhudi za kusaka hizo pesa. Sio kwa wadada tu hata jamii inayokuzunguka itakuheshimu ukiwa mpambanaji...
Ngoja niwape kisa....
Ninapoishi mimi naishi na rafiki yangu.....ni m'bangaizaji tu kama mimi hapa. Sasa jana asubuhi natoka mama mwenye nyumba alikuwa anatoka pia...kufika mbele kidogo akasimama kunisubiria akaniamba 'khantwe nina shida na wewe' . ( Ni mama mtu mzima anakimbilia kwenye 60 kama sio amefikisha kabisa). Akaniambia 'huyo rafiki yako mwambie bwana....yule boyfriend wake sio....si lolote si chochote'. Mimi heee...mbona mi simfahamu huyo shemeji? Akaniambia 'anatoka na kijana huyo wa nyumba ya tatu hapo....anakaa kwao hana hata shughuli ya maana...mi roho inaniuma bwana....na binti inaonekana huwa anampa vihela....'
Bas yule mama anaongea hayo mi sina mbavu. Kusema kweli mi sikuwahi kuona wala kuhisi dalili yoyote ya 'shemeji'...nadhani ni kwa sababu kila mtu yuko bize na mambo yake mara nyingi huwa tunaonana asubuhi wakati tunajiandaa kutoka...ila baada ya yule mama kuongea nikaanza kuunganisha dots nikajikuta nacheka tu....nikakumbuka mambo mawili matatu. Mi huyo kijana hata simfahamu ila kwa maelezo ya yule mama nitamsaka hadi nimjue kwa kweli.
Angesema binti mdogo tungesema mabinti wa siku hizi wanapenda hela...na huyu mama mtu mzima je..???
Tuseme tu ukweli kijana ukiona umekua kiasi cha kufikia kuwa na mahusiano usharobaro hata kama unaupenda tupa kule...jishughulishe....
Ni hayo tu..