Vijana wa Kiafrika na kutojishughulisha

Vijana wa Kiafrika na kutojishughulisha

Intel5500

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2019
Posts
738
Reaction score
655
Hawa vijana wa miaka 18 mpaka 23 hadi 26 wanaishi maisha ya ajabu sana, yani utakuta mtu kuanzia asubuhi mpaka jioni mtu amekaa tu barazani kusikiliza visingeri.

Huku mtaani ukimkuta kijana mwenye umri huo kashika kitabu anajisomea cha kuongeza maarifa basi kiama kesho kutwa.

Huku mtaani vijana wanafanya kazi ya kukimbizana kama kuku ili tu wafanye ngono.

Yani mtu afikirii miaka 17 ijayo yeye atakua kwenye hali gani mtu unaishi kama kuku, kazi kulishwa na baba na mama yako tu huna hata plan za maisha kwanini usiwe sawasawa na kuku.

Unaamka asubuhi unakunywa chai na maandazi ya mama; unaenda kwa wahuni wenzako kufanya ujinga unarudi mchana unakula ugali na dagaa wa mama then unatoka unakwenda kwa wahuni wenzako unarudi usiku. Usiku unakula wali na maharagwe ya mama unakwenda kulala. Ikifika asubuhi unafanya kilekile cha jana. Hii kwa waliokwenda shule na wasiokwenda shule.

Tumia muda wako kufanya vitu vya maana ambayo labda vitakua na faida kwako na kwa taifa lako sio kulilia ajira, tumia elimu yako kutatua changamoto zinazokuzunguka wewe na jamii yako na sio kulilia ajira kwani wewe huko shule ulikwenda kufundwisha ajira? Kasablanka kabisa, hii kwa wale waliokwenda shule kupoteza muda Kisha kuja kulilia ajira, upuuzi tu.

Huku mtaani ukiwakuta vijana wamekaa sehemu wenyewe wanaita kijiweni hayo maongezi yao ukisikia unaweza ukatikisa kichwa hadi kikang'oka. Wanaongea vitu vya ajabu mno: mademu, ngono, mpira ya Ulaya ila hata sentence moja ya Kiingereza hawaijui. Hutosikia wakiongea kuhusu maisha yalivyo ili wasolve changamoto zilizowazunguka, yaani wao kuishi na changamoto ni kawaida kabisa na hii ni moja ya sababu inayofanya Africans masikini wengi hiyo kwa wote aliyekwenda shule na aliyekwenda kabisa.

Wazungu wanaendelea kutokana na vijana wao wa kipindi hicho kushindwa kuishi na changamoto hivyo wakisolve tatizo hili na akili yao inatanuka ndo maana hadi leo wapo mbali na wao wanaendelea kurithisha vizazi vyao tabia hizo...

Ila kijana wa Kiafrika akipata changamoto anamwachia Mungu na kuendelea kulala huku akifikiria ngono na upuuzi mwingine, na wakati huo akirithisha vizazi vyake. Hata humu wapo wengi tu...

Hawa vijana ukiwaambia ukweli watakuona wewe ndo boya na mjinga na huku wanakutukana matusi...Watakukosoa kwa dharau na kejeli kumbe ni wajinga wanaoshindwa kutumia elimu zao kupambana na changamoto na kuishia kutoa nyodo; hii kwa waliokwenda kusomea ujinga shuleni...

Nyie vijana mbadilike; ngono na mambo mengine ya kijinga hayatowasaidia muda ndo huu hakuna second chance sio mkifika 30 hauna hata bakuli unakuja humu kulialia..

Ukweli siku zote unauma.
 
Mkuu Chimbuko la tatizo linaanzia "Ikulu"

- Influencers, Marketing, Media, Strong Men, Celebrities wana impact kubwa sana kwenye maisha ya watu.

Mtu yuko tayari kunywa Pepsi kwa kuwa Diamond kapewa pesa aseme ni soda nzuri.

Mtu anawekeza kwa Mr. Kuku kwasababu Joti kapewa pesa aseme ni uwekezaji mzuri ( ingawa yeye hawekezi huko ).

Unapokuwa na Rais ( ambaye maneno yanapewa uzito sana na media+makanisa+misikiti )anahamasisha ngono na kuzaana unategemea ngumbaru watakuamini wewe?

Rais anapo discourage matumizi ya lugha ya kiingereza ( kwa kuwa yeye hajui ) unategemea watu wahamasike kujifunza ?

Halafu, Anataka watu wakafundishe Kiswahili nje ya nchi ( Utafundishaje Mwanafunzi lugha yako wakati lugha yake huijui )

Binafsi Nilijitutumua sana kujifunza English baada ya kumwona Kikwete anaongea kwenye podia kubwa kubwa.

In Short, Baba/Mzazi ndio first role model wa wanao.
 
Mama anauza komoni,
Baba fundi baiskeli,
Kaka anakodisha Cd,
Dada kungwi,
Familia kama iyo kuitoa na kutaka iwe level unayotaka ki taifa.
Ni ndoto maana hakuna hata inspiration kushoto kulia kote hamna wenye msaada w kifedha Wala ono la biashara, wameridhika na dhiki maana wamezaliwa zinawatolea macho😲
 
Unachomaanisha kwamba hivi vitu vimeanza baada ya jiwe kuingia madarakani..??

Ukiwa mpinzani haimaanishi kila lawama umrushie opponent wako...hata kama hahusiki..
Swala la kuwa jobless limeanzia utawala wa magufuli??
 
Mama anauza komoni,
Baba fundi baiskeli,
Kaka anakodisha Cd,
Dada kungwi,
Familia kama iyo kuitoa na kutaka iwe level unayotaka ki taifa.
Ni ndoto maana hakuna hata inspiration kushoto kulia kote hamna wenye msaada w kifedha Wala ono la biashara, wameridhika na dhiki maana wamezaliwa zinawatolea macho😲
Yes hilo ndo lengo la uzi na jamiiforums kama wapo watu wenye maisha na mawazo yaliyoganda basi wakisoma huu uzi watashtuka tu dunia ni Kijiji siku hizi......ila sio lazima ufikie level ya kitaifa kusolve changamoto zako mwenyewe na kuboresha ndicho cha msingi na hapo ndo mwanzo wa kila kitu...hata ngazi utaanza kupanda mojamoja mpaka utafika juu.....
 
Aise pilipili usioila yakuwashia nini,unavyotafsiri mafanikio sivyo mwenzako anavyotafsiri
Mind your own business.
 
Mnapoachana na wapenzi wenu muachane jumla jumla sio mnarudiana rudiana mnatufanya sisi tunaosambaza habari tuonekane waongo

Stress tu
..seriously?? nani apoteze muda kufikiria ujinga unaoitwa mapenzi....alafu kesho ajui anakula nini....wewe nae upo pale kajisome...
 
.....Mods vizuri kwa kuedit uzi wangu...ila kichwa mmekiharibu....
kichwa kinasema: VIJANA WA AFRIKA...

na sio: vijana wa AFRIKA na kutojishughulisha...
 
Back
Top Bottom