Vijana wa Geita wasipuuzwe

Vijana wa Geita wasipuuzwe

Hawamtambui rais ila wanaenda kutaka kumuona, jambo gani lililoshindikana levo (level) zote za uongozi mpaka litatuliwe na mkuu wa nchi? Je wameweka ahadi ya kumuona ama ?

inawezekana kabisa wakawa ishu muhimu sana kuhusu madini jinsi wawekezaji wanavyochukuwa kama ya kwao na kuwaacha watanzania wanaozunguka hiyo migodi kuwa na hali mbaya ya maisha
 
Hizo nguvu walizotumia kutoka Geita mpaka Dar es Salaam wangetumia kwenye kilimo cha mahindi na pamba wangepata mavuno mengi sana.

Mavuno mengi sana ambayo hayana soko la kuuzia yana faida gani? Hujasikia wakulima wanalia kuwa mahindi yao yanaozea ndani na hifadhi ya taifa ya chakula wanasema hawanunui tena hawana fedha? Na wakipeleka nje wanaambiwa ni walanguzi na wahujumu uchumi? Labda hilo nalo walitaka kumwambia Rais wao!
 
Hizo nguvu walizotumia kutoka Geita mpaka Dar es Salaam wangetumia kwenye kilimo cha mahindi na pamba wangepata mavuno mengi sana.

Wakishayapata watayauzia wapi?!
Wanaolima kila siku tunawaona kwenye Tv wakilia na masoko.
 
Hizo nguvu walizotumia kutoka Geita mpaka Dar es Salaam wangetumia kwenye kilimo cha mahindi na pamba wangepata mavuno mengi sana.

hizo pesa walizo kwiba viongozi zingetumika kujenga zahanati vijiji vingapi?, zingejenga na kukarabati madaraja mangapi Tanzania?, zingesomesha vijana wangapi kuhusu kilimo?,zingenunua ambulance ngapi?,tungepunguza gepu la vifo vya mama wajawazito kwa kuwalipa madocta na wasaidizi leo hii tungekuwa tunasimlia Mambo mengine tu. hawa vijana waachwe wakatoe ya moyoni kwani wangechukua hatua ya kuanzisha kundi la fujo tungekuwa tunasimlia mengine. japo wamefikisha kwa natembezi tu haina shida na tusiwavunje mioyo kwani ungelikuwa wewe je fikiri kabla hujaandika. mungu wanyooshee waja wako.
 
si wangeenda kuwambia baba zao bana?,
ama bwanashamba wa kijiji cha geita

Hata Tunisia alijilipua kijana mmoja tu kwa moto. Matokeo yake yanaonekana mpaka leo hii!! Mzarau mwiba mguu uota tende.
Rais wapokee hawa vijana!!
 
Hizo nguvu walizotumia kutoka Geita mpaka Dar es Salaam wangetumia kwenye kilimo cha mahindi na pamba wangepata mavuno mengi sana.
Mkuu haya unayoyasema ilitakiwa waambiwe na Rais, tena asiongee juu juu tu, awaambie ni kwanini ktk historia ya nchi hii hakuna shujaa wa kulima mahindi ila kuna shujaa aliyefia njiani akitembea kuelekea dar es salaam kama njia ya kuunga mkono Azimio la Arusha (Seth Benjamin), pia asiishie hapo awaeleze pia ni kwanini alikubali kuonana na yule aliyetumia baiskeli kwa ajili ya kumpongeza Rais lakini sasa anakataa kuonana na waliokanyaga kwa mguu tena wakiwa na ujumbe wa kizalendo. Akishawaeleza hao vijana amalizie kwa kuwaambia watz ni kwanini yeye na chama chake CCM bado wanaamini wanaweza wakafanikiwa kwa kupigiwa makofi na kusifiwa wakati dunia ya sasa inahitaji kufanyia kazi makosa ili kuwe na mafanikio, hivyo kukosolewa ni muhimu zaidi kuliko kusifiwa.
 
Is as simple as that!!Ni kuwakaribisha, kuwasikliza baasi. Si lazima ukubaliane na ujumbe wao lakini kama wananchi na watanzania ni haki yao kuonana na Rais wao.I think tatizo hapa ni moja; wamejitanabaisha toka mwanzo kuwa ni CHADEMA na kama Rais huyu anataka ofisi yake iwe accessible kwa wana CCM wenzake tu, then hili ni tatizo na udhaifu mwingine kwa utawala wa Kikwete ambao tunaweza kuupa description ya "utawala uliojaa woga na kutojiamini" kusikokuwa na sbb!!Rais ni kiongozi wa wote bila kujali itikadi za kisiasa; ni kiongozi wa hata mataahira,wachawi,walevi na kila aina ya binadamu so long as ni wananchi wake!!Lililo muhimu hapa hawa watanzania wenzetu kama kuna taratibu wanazopaswa kuzifuata ili wamwone Rais/kiongozi wao wa nchi waelekezwe kuzifuata kwa upendo na kwa amani tu na si ku - treat kama criminals.....ni ujinga na hakika ni upumbavu wa kiwango cha juu sana. Je,ni kwa sbb labda kwa nini si wewe, yule au wale? Na kwa nini tujiulize maswali kama haya kwa sababu wao ni wao na sisi ni sisi.....kamwe haiwezekani tukawaza na kufikiri sawasawa na wao au mimi nikafikiri sawasawa na wewe!!Viongozi wetu wanapaswa kulitambua hili., na wakitambua hili kamwe hawatapata shida kuongoza watu kama amabavyo Mungu aliyetuba sisi sote asivyopata shida kuongoza watu wake. Na sbb ni moja tu anaheshimu mawazo na uhuru wa lila kiumbe alichokiumba!!Huyu Mungu angekuwa kama kina Kikwete na wenzake wenye mamlaka kwa niaba ya huyuhuyu Mungu sijui dunia hii ingekuwa vipi tu!!
 
Mch.Mtikila ni mtu muhimu sana nchini. Kwa nini Kikwete akubali kuonana na wanaompongeza lakini awakatae wanaomkosoa,huu sio udikteta? Ni madikteta pekee wasiokubali kukosolewa!... Heko kwa mtikila kwa kumweleza huyu kikwete ukweli
 
Ni jambo la kibaguzi la watawala wetu, na ni ujuha kutokubali kukosolewa kwani sote ni binadam,na hakuna aliyekamilika sasa ni kwa nini wavaa heleni na wavaa vichupi wapewe vipaumbele kwenda magogoni,kupiga picha na kula tu wakati watu wenye ujumbe na mawazo ya kujenga wakataliwe? SIFA HAZIMJENGI MTU BALI HUMPUMBAZA.
 
Back
Top Bottom