Vijana wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana

Vijana wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Tangu nimejiunga ndani ya CCM, nimepata fursa ya kufanya tafiti na kugundua tofauti kubwa sana kati ya viongozi, wanachama na hasa vijana ndani ya CCM na wale wanaotoka vyama vya upinzani, vikiongozwa na CHADEMA.

Lakini hali hii inatokana na mfumo wa Chama Cha Mapinduzi ambao umejikita katika malezi na mafunzo kwa vijana wake kupitia jumuiya yake ya vijana (UVCCM) ambayo imejibainisha kuwa ni tanuru la kuoka viongozi wa chama na Serikali.

Kitu cha kipaumbele ktk uongozi na shabaha ya UVCCM ni kuongeza maarifa kwa vijana wa chama. Vijana wengi wameendelezwa kielimu (kwa fedha ya jumuiya) katika vyuo vikuu mbalimbali, jambo ambalo vyama vya upinzani hawafanyi, hawana mfumo wa ku-groom vijana wao na badala yake vijana wamekuwa wakijiongoza wenyewe na hivyo kupoteana.

lakini pia, Vijana wa UVCCM wana matumaini zaidi kuliko Vijana wa Chadema na wapinzani wengine, leo vijana wa Chadema na Wapinzani wanatamani wangekuwa CCM ili wanufaike na fursa za kupata maarifa na kujengewa uwezo, ndio maana akina Yericko Nyerere, Ben Saanane na wengineo wanafanya kazi za wagombea wa CCM kwa kuwa wamepoteza matumaini na viongozi wao kwenye vyama vyao.

Uwezo mdogo wa vijana wa chadema unajidhihirisha kwenye CV zao, kwani wengi ni mangumbaro wasio na elimu ya kutosha, lakini pia maneno wanayoandika kila kukicha katika jukwaa hili yanadhihirisha uwezo wao mdogo, thread za akina Henry Kileo, Tumaini Makene etc zinawavua nguo vijana wa Chadema.

USHAURI.
VIJANA wa vyama vya upinzani jiongezeni, mnalalamika hamna ajira wakati elimu ya kuunga unga, mnafikiri mtapata kazi kwa kuandamana..? Ongezeni maarifa ili muweze kuajirika, sio mnakesha kwenye ma-movement yasiyo na tija halafu mnategemea maisha bora.
 
Naomba uweke cv yako hapa ....laa sivyooo ondoka...mimi nimekuwa nasoma na vijana wengi wa ccm kule shule za kata walifel ....vijana wenye mafanikio Tanzania hii ni wa vigogo au mafisadi mfano watoto wa mkuu wa kaya...,lowasa ..sumaye...membe ...ndo wengi wamefanikiwa na wengi wanakuwa wameungaunga .Nape mwenyewe kaungaunga na division four yake..Tanzania ukiwa ccm unapewa ...chet..elimu co vyeti maarifa....
 
Uwezo mdogo ktk mambo gani!Je kufanya vurugu?Kuwatukana viongozi na kuwafanyia vurugu kama alivyofanya Makonda?
Je wewe ulikuwa na uwezo mdogo ulipokuwa CDM baada ya kufukuzwa ukaenda huko uliko umeongezeka uwezo by induction?Hawa ndo unasema wana uwezo mkubwa,je wanachokifanya ni sahihi kulingana na halmashauri ya ubongo wako?
 
Attachments

VIP movements za ccm Kama 4m friends of lowasa na hizo ni vyama vya upinzani?
 
Juliana Mimi nakushangaa sana kwa Maelezo unayotoa ni kama mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia.
Lakini kumbuka chadema ndio waliokufundisha siasa wakakulea vizuri ndio maana ccm wanakuona lulu sasa hivi.Pia tambua chadema ni chama makini sana hata ww unalifahamu sana ila tatizo lako njaa inakusumbua sana ndio maana unafanya utafiti kengeza,sisi vijana makini hatuyumbishwi na maneno yako tunasonga mbele tena tunaomba Mungu asikuchukue mapema uone gharika ya mwaka huu itakavyokuwa.
 
Juliana Shonza
Benazir,

Naomba tuheshimiane sana sana.Hii Obsession ya kunitajataja Ovyo si ya kiungwana na haipendezi

Unaweza kuleta ushahidi wa hizo tuhuma dhidi yangu?Ni mgombea yupi wa CCM?

Hizi sifa za kutafutia Ukuu wa Wilaya hazifai na sikutarajia utafikia hatua ya kunituhumu kwa sababu hiyo au sababu binafsi tu

Usizihamishie huku public.Hebu kuwa Mstaarabu sasa
 
Last edited by a moderator:
Tangu nimejiunga ndani ya CCM, nimepata fursa ya kufanya tafiti na kugundua tofauti kubwa sana kati ya viongozi, wanachama na hasa vijana ndani ya CCM na wale wanaotoka vyama vya upinzani, vikiongozwa na CHADEMA.

Lakini hali hii inatokana na mfumo wa Chama Cha Mapinduzi ambao umejikita katika malezi na mafunzo kwa vijana wake kupitia jumuiya yake ya vijana (UVCCM) ambayo imejibainisha kuwa ni tanuru la kuoka viongozi wa chama na Serikali.

Kitu cha kipaumbele ktk uongozi na shabaha ya UVCCM ni kuongeza maarifa kwa vijana wa chama. Vijana wengi wameendelezwa kielimu (kwa fedha ya jumuiya) katika vyuo vikuu mbalimbali, jambo ambalo vyama vya upinzani hawafanyi, hawana mfumo wa ku-groom vijana wao na badala yake vijana wamekuwa wakijiongoza wenyewe na hivyo kupoteana.

lakini pia, Vijana wa UVCCM wana matumaini zaidi kuliko Vijana wa Chadema na wapinzani wengine, leo vijana wa Chadema na Wapinzani wanatamani wangekuwa CCM ili wanufaike na fursa za kupata maarifa na kujengewa uwezo, ndio maana akina Yericko Nyerere, Ben Saanane na wengineo wanafanya kazi za wagombea wa CCM kwa kuwa wamepoteza matumaini na viongozi wao kwenye vyama vyao.

Uwezo mdogo wa vijana wa chadema unajidhihirisha kwenye CV zao, kwani wengi ni mangumbaro wasio na elimu ya kutosha, lakini pia maneno wanayoandika kila kukicha katika jukwaa hili yanadhihirisha uwezo wao mdogo, thread za akina Henry Kileo, Tumaini Makene etc zinawavua nguo vijana wa Chadema.

USHAURI.
VIJANA wa vyama vya upinzani jiongezeni, mnalalamika hamna ajira wakati elimu ya kuunga unga, mnafikiri mtapata kazi kwa kuandamana..? Ongezeni maarifa ili muweze kuajirika, sio mnakesha kwenye ma-movement yasiyo na tija halafu mnategemea maisha bora.

ccm nje ya ruzuku inaniliki vitega uchumi vingi sana tofauti na vyama vya upinzani mfano viwanja vyote vya mipira vipo chini ya ccm pili mtaji wa kuwepo madarakani muda mrefu tatu wazee wengi wa ccm wamejilimbikizia mali za umma sasa watashindwaje pesa zingine kuwagawia uvccm na kuwaendeleza pia umesahau kwamba ndani ya ccm kuna makundi ambayo yanagawa zawad kwa hao vijana ili iwe rahis kupata uongoz pindi wanapoutaka nakukihakikishia hata cuf ikiingia madarakani kwa mfano ni lazima itawajali vijana wake kwa hiyo mleta mada angalia na ukongwe wa ccm madarakani unachangia nyie kuish vizur mna mitaj mingi sana tofaut na upinzani mfano singasinga seth kama anahonga serikali pesa nyingi serikali ya ccm sasa uvccm mtashindwaje kuambulia na kuendelezwa?
 
Samahani dada. Hivi wewe umesomea nini? umeajiriwa na nani na wapi? tunaomba CV yako ili tujifunze.

CV yangu unaweza kuigoogle tu.,its that international. Ila kwa kifupi ni kuwa nimemzidi kielimu Mwenyekiti wako, Makamu Mwenyekiti wako, Nimemzidi Naibu Katibu Mkuu wako, Nimemzidi Mkurugenzi wako wa Uenezi, Nimemzidi Mkurugenzi wako wa mafunzo, kwa kifupi nimewazidi almost wakurugenzi wenu wote.

Ila hilo ni ni tisa, BAVICHA hakuna hata mmoja mwenye kunifikia kwa CV!
 
Ukweli ccm wanadharau sana sisi walipa kod ..nimegundua kama huna elimu usiwe ccm...et huwafai hayo majigambo...cc vijana wajasiriamali kwrli ccm imetukataa....kwa hichobulichoandika ni dhahir tusio soma kwasababu wazaz wetu ccm imewanyonya na kuwatelekeza mnatuona wajinga....tunataman kusoma ila mfumo wa nchi yetu ...her chadema walituaombia tungesoma bure ..tumewapigia kura leo mnatudharau ahsante Shoza
 
Juliana on board! Wenzako wameshalamba ukuu wa wilaya masikini sijui ulisahaulika wapi!

Sikusahaulika mkuu ni suala la muda tu hatuwezi Pata wote lazina wengine wapate wengine wakose CCM chama kubwa wakina Mboni na Makonda wanatosha kutuwakilisha vijana.
 
Juliana Shonza

Ongera sana kwa kulitambua ilo na karibu kwenye jumuia ya vijana makini wenye oja ambao siyo kurumbana kwa matusi.
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli CCM mna dharau! Umesahau hali waliyo nayo hawa vijana ni matokea ya mfumo mbovu chini ya CCM? Na bahati mbaya hali hii sio kwa vijana wa wapinzani tu bali vijana walio wengi nchini.

Yaani kuingia CCM juzi tu tayari dharau zisizo na mfano kwa wananchi! Hivi ukibahatika kupata ka-uDC si utawakanyaga waTz vichwani wewe? Mungu apishe mbali.

Mfumo huo huo unaouita mbovu ndio umetutoa sisi maskini kutokana na juhudi za kujiendeleza na kujituma, nyie kalieni kulalama na kungojea maandamano muone kama mtapata maendeleo bila kujituma, hata atawale Yesu bila kujituma hupati maendeleo ng'o!
 
Kwahiyo ulivyoingia CCM tu ukasoma then ukirudi CDM usomi wako woote unafutika baadae ukirudi CCM usomi unarejea tena?

Maprofesa mna mambo.
 
CV yangu unaweza kuigoogle tu.,its that international. Ila kwa kifupi ni kuwa nimemzidi kielimu Mwenyekiti wako, Makamu Mwenyekiti wako, Nimemzidi Naibu Katibu Mkuu wako, Nimemzidi Mkurugenzi wako wa Uenezi, Nimemzidi Mkurugenzi wako wa mafunzo, kwa kifupi nimewazidi almost wakurugenzi wenu wote.

Ila hilo ni ni tisa, BAVICHA hakuna hata mmoja mwenye kunifikia kwa CV!

wao wamekuzidi uwezo wa kufikiria na utendaji ww ni bingwa wa cv pia unaweza ukawa umamzid hata la proffeseli wa kichina kwa cv
 
Back
Top Bottom