Vijana umri unaenda sasa muanze kuwa serious. Shauri yenu, mtakuja kutulaumu bure

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Jamaa yangu ana mdogo wake kamaliza chuo mwaka Jana. Amekaa Mtaani kodi imeisha akakosa pa kukaa. Kaka yake ni mtu wangu wa karibu. Akanambia mdogo wake anakosa pa kukaa. Jamaa yupo Dodoma.

Pale home nina Servant Quarter. Nikamwambia aje akae pale mpaka akichoka. Vyumba viwili, jiko,s ebule na choo. Anakaa kijana wa kusaidia kazi home wa Kiume. Basi bwana mdogo amefika home Umarekani Marekani mwingi sana.

Ilibidi nimpe Darasa kuwa pale home muda wa kurudi mwisho saa mbili, asivae nguo zinazoacha makalio nje, asivae nguo za kubana sana mwili. Nikamwambia anadhani ataweza hayo? Maana kwa kweli ni changamoto na mimi nina watoto pale home. Akajibu ataweza. Nikamwambia hamna shida.

Baada ya week tu akaleta Demu pale chumba anachokaa. Hakujua mimi naona kwenye CCTV Camera. Akalala naye. Kesho nikamwita nikamwambia aache ule ujinga.

Dogo 24/7 yupo na simu. Anakuja kula huku anachezea simu. Akimaliza tu kula anaondoka bila kutusubiri sisi wengine. Anaweza akatangulia kula nyie mmejikusanya mnakuta keshakula kaondoka.

Sasa juzi nlimtumia text kuwa kuna sehemu nataka aende akafanye Interview. Akaa kimya though alisoma text after 5 hours ananitumia text "bro ile issue ya job imekaaje kaaje. Ili niangalie michongo yake kama ipo au vipi" sikuweza mjibu mpaka hii leo. Hiyo nafasi nilimsaidia mtu mwingine mwenye nidhamu.

Hawa vijana wa sasa akili wanapoteza wakiwa na umri gani? Au wanapotezea wapi? Na huyu ni graduate kabisa wa Sheria. Very hopeless. Sasa baadaye ataanza lalamika kuwa amekaa na mimi nmemtesa maana sijaruhusu alete demu ghetto. Naonekana mimi mkoloni n.k vijana badilikeni muanze kuwa serious sasa. Muda unaenda sana.
 
Ushamfukuza au unasubiri akuibie?

Mnawezaje kukaa na "mdogo wa rafiki yangu" unamuamini vipi? Akichezesha mchongo akawapa ramani wahuni yeye ale tu 10%?

Me nadhani wewe haujamsaidia kwa kumpa nafasi ya kukaa. Ni bora ata usingempa kabisa maana dogo anaonekana kabweteka.
 
Mimi nitabaki naamini watanzania umri wa kujitambua ni kuanzia miaka 30 aliye sema 18 huyu alifata umri wa wenzetu wazungu sisi bado sana.

Kwa kisa hiki unazidi nithibitishia mawazo yangu kuna mpumbavu kama huyo nilimuungia kazi ya ukarani akakataa mwenzake akaubali baada ya mwaka amekuwa meneja wa eneo lile.

Jamaa anabaki nambia sikuwahi mwambia kama inawezekana kupanda cheo kuwa meneja.
 
"bro ile issue ya job imekaaje kaaje. Ili niangalie michongo yake kama ipo au vipi" sikuweza mjibu mpaka hii leo. Hiyo nafasi nilimsaidia mtu mwingine mwenye nidhamu.
Ulifanya la maana sana, yaani sijui kwa nini wanaona ulaini sana? Kuna mmoja alitafutiwa mahali akawa analalamika ni mbali sana anachoka wakati huyu aliyemtafutia anakwenda same place na wanaishi pamoja pia.Nilikereka kupita maelezo.
 
Mimi mzee alinionyesha ukauzu kuwa hanitaki tena kwake nikiwa second year tu nilivyomaliza chuo nilikaa miezi miwili nikatimka home kusaka ngawira mkoani kujipigia dili za kilimo cha mpunga cha ajabu huku huku ndi nikapata na ajira kabisa ila hadi leo.

Cha ajabu baada ya miaka 2 mzee anataka nirudi home kuendeleza mali zake kwa kisingizio amechoka wakati mimi mwenyewe nshajipanga nafanya yangu
 
Na suala la ajabu unakuta Kuna vijana wengine wazuri mno kitabia na ki'akili pia, ila balaa lipo kwa walezi au wazazi walio nao ni wakoroni, wanyanyasaji, walevi, sio watu wa maendeleo, sio watu wa kujari wala kusupport jambo la msingi in short wanapitia Wakati mgumu kujinasua tofauti na huyo bwege.

Hivyo; Kwenye miti hakuna Wajenzi.
 
Acha kutuandikia chai wewe nawe.

Nyumba yenye CCTV, muda wa kula hadi muanze kusubiliana ? Manakula kwenye sinia moja au mnakula kwa ndiki ? 😆😆😂

Huu uzi naomba upuuzwe, hauna la maana.
Mkuu suala la kula pamoja ama kila mtu kwa wakati wake ni suala la utaratibu tu

Mie leo nikienda home lazima nile na mzee piga ua

Kula kwa pamoja sio kukaa sinia moja hapana kila.mtu na.sahani yake ila meza moja
 
Back
Top Bottom