Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,332
- 10,911
Habari wakuu.
Wito wangu kwa vijana wenzangu, wasomi na wale wasio wasomi. Sisi ndio vijana wa taifa hili. Tusipochukua hatua sasa itatugharimu sana. Kumuacha mpaka 2025 itatugharimu sana, wengi tutakuwa tumefikisha miaka thelasini na ushee huku wengine wakipiga arobaini. Kwa kweli tutakuwa tumepoteza muda mkubwa sana.
Wanawake wetu wanahitaji tuwaoe, wanahitaji tuwapatie watoto lakini tutawapatiaje watoto ikiwa hali ya maisha ipo hivi. Tutawaoaje ikiwa hatuna kazi za uhakika. Ni jukumu letu kama vijana kuchukua hatua madhubuti kuokoa jahazi hili. Kurudisha matumaini kwa dada zetu. Dada zetu na ninyi tambueni yakuwa hakuna mwanaume asiyehitaji mwenza wa maisha, kila mmoja anahitaji siku moja awe na mke wake ampendaye kwa dhati lakini yote yatawezekana ikiwa hali ya uchumi itakuwa nzuri. Wanawake mulio humu ndani na wale msiohumu tuungane katika jambo hili ili zile ndoto zetu ziweze kutimia. Nyie ndio wake zetu na sisi ndio waume zenu. Tusipoungana tutakuwa watumwa katika nchi yetu wenyewe.
Kisiki hiki kitatutoa wengi kucha hasa sisi watembea kwa miguu bila malapa. Kimetoboa soli za wenye viatu na hata wenye kata mbuga sasa wanahaha. Kisiki kinapasua mpaka matairi ya magari na kusababisha ajali zenye kumwaga damu za watu wasio na hatia.
Kisiki kinachoma watoto wetu miguuni wachezapo na kutembea. Watoto wetu hawana amani hata ya kutembea barabarani kisa kisiki. Watoto wetu hawatakiwi kuongea kwa uhuru kisa kisiki.
Kisiki kinakata mipini ya majembe ya wakulima huko mashambani nadhani wenyewe mmekuwa mashahidi. Wafanyakazi na vibarua wanalia kwani tayari kisiki kimewatoboa miguuni tena wengine wamekiangukia tumboni. Malipo yao ni kidunchu licha ya kuwa wanasulubika haswa kufanya kazi zao kwa moyo.
Kung'oa kisiki yahitaji moyo, sururu na shoka. Yahitaji matata, simile hakuna. Vijana nadhani mmenielewa.