Vijana tusimame tuililinde nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana tusimame tuililinde nchi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kulunalila, Dec 3, 2011.

 1. k

  kulunalila Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwanini vijana wa kizazi hiki hatuna uthubutu, kwanini ni vigeugeu. Hatuna nidhamu ya kazi, hatuna uzalendo,hatuna malengo,hatuna subira. Natoa wito vijana wenzangu tusimame tuitetee nchi yetu,tuilinde nchi watu wake na rasilimali zake kwasababu kizazi cha miaka hamsini ndo kinaondoka. Tutekeleze wajibu wetu popote tulipo katika maeneo yetu ya kazi
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sure,
  ila waloupokea uhuru wanazngua
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Karibu sana japo hujapiga hodi
  Inaonyesha ni uzalendo wako ndo umekusukuma kuingia humu! Karibu sana!
   
 4. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,867
  Likes Received: 2,808
  Trophy Points: 280
  Vijana wenyewe wako wapi? Unamaanisha hawa waliopigwa maisha hawa? Ambao wakipewa 500 tu wanauza uhuru? wala hawatusaidii! wanaoweza kutukomboa ni wale rika la kati 35 to 45 period!
   
 5. s

  semako Senior Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ni mtoto wa kigogo?maana kauli zako zinaonesha kama umetumwa.Watu tunaanzzisha miradi tunakamatwa eti tunachafua mji sasa tufanyeje?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ni vigumu sana vijana kujituma na wakafanikiwa chini ya huu utawala mbovu wa serikali ya waizi akina jk!

  Imagine vijana wanalima mazao yao, lakini wakivuna wanataka kuuza kwa faida wanakuja walanguzi wa serikali hiyo hiyo ya waizi wanawapangia bei bila kuuliza gharama na muda waliotumia kulima na kuvuna hayo mazao!

  Vijana wakiamua wanaweza, kwa kuanzia labda niwashauri vijana wenzangu ni kuanza na mkakati wa kuipindua serikali ya waizi kwa njia yoyote ile, either kwa njia ya kura, au mapinduzi ya nguvu ya umma!
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja kwa asilimia zote! Vijana tuamke, tusimame na kuhakikisha tunaiondoa serikali hii dhalimu na kuweka serikali ya umma. Otherwise tutabaki kulalamika na kunyonywa hadi uzeeni.

  Saa ya ukombozi ni sasa!
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Hiyo ya kuanzisha miradi na kukamatwa kwa sababu cheap kama hizo ilitakiwa iwe ndio kichocheo cha kuhitaji mabadiliko ya kiuongozi ili kupata uongozi utakao tuonesha njia na sio kuziba njia.

  Hapo ulipouliza tufanye nini sasa, jibu langu ni simple. Vijana tuhamasishane sisi kwa sisi kwanza, akina mama na baba zetu, na mengine wote ili kufanikisha kuleta mabadilikn "ya kweli" kwa kukichagua chama mbadala kwenye uongozi. Nasema mabadiliko ya kweli maana tusije kuishia kuwa kama watu wa Mtera waliobadilisha afadhali na kutuletea upuuzi!
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mungi na Filipo tuko pamoja yaani huwa natamani vijana tupewe silaha maana naona kuwaondoa kwenye sanduku hawa kenge ni vigumu sana angalia katiba walivyo anza usanii tutegemee nini..
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Filipo kichocheo tunacho basi chadema au chama chocho hakina nia ya kuchukua nchi hii kwa nguvu ya umma lakini na kuhakikishia leo hii chama makini kama chadema wakiitisha maandamano nchi nzima..MAGAMBA TUNAWANGOA..
   
 11. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Hapa nina maswali magumu.

  Je kwa nini CCM wanapenda sana ulaghai na usanii katika uchaguzi? mfano pombe, mchele, kununua shahada za kura, vitisho?

  Kwa nini CCM wanaogopa ushindani katika fair ground?

  Hapa nina vijisababu, bado naweza kusahihishwa.

  - Ahadi hazijatekelezwa.....
  -Huduma duni (afya, elimu, maji, barabara) kwa jamii
  -Uvivu wa kufikiri (hakuna ubunifu)
  -Ubinafsi

  Je kwa nini ahadi hazijatekelezwa au kwa nini sababu hapo juu. - Hakuna hela

  Ila Hazina ya Nchi inavuja, panya wanatafuna, na paka wanakunywa maziwa.

  So jawabu ni kutafuta CHama mbadala. Je wananchi wako tayari, labda 50%.

  je hao wengine 50% ni wajinga? Ndio, wanahitaji elimu ya Uraia.

  Ofisi za vyama vya upinzani vijijini waanzishe elimu ya uraia, kuelimisha wananchi.

  Namna gani, hapa namkaribisha akina Crashwise wachangie.
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  unataka tuthubutu kufanya nini?

  ni vigeugeu kwa lipi?

  nidhami ya kazi zipi? au kwa kuwa wewe una ajira unafikiri kila kijana ana ajira?

  uzalendo kwa nani? kwani mtu ku-qualify kuwa mzalendo anahiaji nini?

  malengo yapi?

  subira ipi?

  kajipange upya.
   
 13. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  tulinde nchi??? Wanajeshi wanalipwa mishahara kwa kazi gani? Acheni kutuzingua kitaa life tough ajira hamna, ukijiajiri ktk sekta isiyo rasmi mara unafanya biashara sehemu isiyoruhiwa, ukiwa mvuvi kwa zana duni wewe mvuvi haramu, uchimbaji mdogo wa madini mizinguo eti umevamia eneo la wawekezaji, mkaa nao kuchoma ni kosa maafsa misitu wanabana uje mjini sasa fungua hata saloon umeme wa mgao, hayo makampuni ya kukopesha menyewe yako kifedha zaidi kuliko kusaidia vijana ktk elimu ndo hivyo tena mnapelekwa wengi shule huko hamna walimu, vitabu wala vifaa yaani ni kwenda kulundikwa ukifaulu ukafika mbali chuo miyeyusho kupata mkopo hadi kwa mabomu, kwenye mziki ndo hivyo tena mavirusi wa kutosha mtangazaji dj wote magumashi, ktk nyumba za ibada hivyo hivyo tunahimizwa kutoa wakati hela ya kula mzozo yaani tumebanwa kila angle serikali inacheki tu yaani naweza kuandika vikwazo hadi jioni ni vingi saaana. Afu unatuambia tuwe wazalendo kwa lipi??? Sasa bora nchi iuzwe tugawane chetu tujue moja kuliko sasa wanafaidi wachache na watoto wao eti uzalendo kawambie wanajeshi wanaolipwa mishahara mizuri kwa wakati ila sio walimu wala wauguzi yaani mnanichefua uzalendo, uzalendo my ***
   
Loading...