Sigara Kali
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 3,623
- 8,428
Nimetafakari sana na kushindwa kumwelewa huyu rais wa awamu ya 5 ndugu Pombe Magufuli
Utawala huu unaonekana wazi hauna nia ya kuboresha Maisha ya vijana wa Nchi hii ambao ndio robo tatu ya watu wote ,ndio wapiga kura na ndio wachapa kazi wa Nchi hii
Vijana wa Tanzania tunakejeriwa,hatuthaminiwi,tunaitwa wavivu wapiga dili.
Vijana wametoka chuo wameshindwa kuajiriwa,sawa nafasi za ajira chache tuwezeshwe basi hata mitaji tukalime mchicha huko na nyanya,raisi hana muda anajali kujenga reli na kununua vipanga boi na terrible teen(Boeing dreamliner)
Vijana wa Nchi hii wamekosa dira,wamekosa malezi mema ya viongozi wao,hawajajengewa mazingira rafiki ya kujiajiri,wanaishia kusimangwa,kubaguliwa,kukejeliwa na kuonwa wavivu wakati nchi haijawaandalia msingi
Serikali ya awamu ya 5 ndo inaonekana kabisa haina time na vijana wa nchi hii, Leo hii vijana watanzania wamekua wakiishi Maisha ya kubahatisha,kijana ili ale inabidi akabeti, akacheze kamari kwenye mashine za wachina na hii inafanikiwa baada ya kupambana kupata mia 5 akafanye shughuli hiyo
Wanasiasa,viongozi wamewasahau vijana wa Nchi, wanawadharau, hawawathamini wanaowaona kama ni wajinga, wazembe, wavivu, tegemezi hawana manufaa kwa nchi yao
Leo vijana wengi wamekata tamaa kwenye nchi yao has a baada ya kuingia huu utawala wa awamu ya 5 chini ya Magufuli
Vijana hawajajengewa mazingira yoyote bora ya kuboresha Maisha yao leo lawama zote kwao, Serikali inaona bora kuwekeza kwenye mambo yasiyomnufaisha mtanzania wa kawaida hasa kijana nguvu ya nchi hii wanadeal na vitu vinavyowanufaisha wachache akiwemo raisi na ukoo wake na wale wote wenye nazo
Vijana wa Tanzania wanaishi kwa kudra za Mungu waliowaamini kuwatengenezea mazingira mazuri kwao wamewasaliti, hawawajali, wanawadharau, kuwakejeli na kuona vijana hawa wanastahili tabu , mateso na shida katika nchi yao.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki vijana wote wa taifa ili la Tanzania