Vijana tuna hali ngumu sana katika utawala huu wa awamu ya 5

Ninayo mahindi mabi
Kama vijana tupo serious kuna mambo kadhaa tunaweza kufanya
1. Kufanya mobilization.Tuanzishe forum tukutane tuunde kundi tujisajili tukachukue mikopo halmashauri.Maneno bila vitendo ni sawa na bure.
2.Tutafute maeneo yenye rutuba tufanye KILIMO chenye tija kwenye kilimo serikali imeondoa tozo SUMBUFU na watu wanapiga mpunga kupitia KILIMO tuwe serious.kama kuna mtu aliye serious na hii ishu ajitokeze.Kukaa kulaumu mtandaoni sio solution.
3.Tunaweza hata humuhumu kuanzisha forums kwa ajili ya kupeana mikakati ya kupiga biashara.Kukaa kulaumu serikali tutalaumu hadi kuzeeka.
Kama upo serious muda ni huu kama unataka kuendelea kuwa mlalamikaji JF basi utabaki kila siku kulaumu serikali,[/QUO


Ninayo mahindi mabichi vi-ekari vitatu nataka kuyauza yakiwa mabichi, hakuna mnunuzi anayeeleweka. Shida sana hii
 
Tanzania tulishakwenda kombo sana hivyo kurekebisha makosa kwa haraka lazima wath wengi waumie.tulizoea fedha nje ya kazi ngumu sasa mambo yamebadilika. Kibaya zaidi kiongozi anasema tuko kwenye 'raiti traki' hivyo tutembee kifua mbele! Sijui kifua gani huku watu aamekonda wamebaki mifupa.
Chamuhimu kwasasa tafuta shughuli na uipambanie haswa maana hamna lelemama saii. Waajiriwa wenyewe haliyao ningumu
 
Gharama za kujenga uwanja wa ndege chato zingesaidia vijana wangapi kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wengine?
Hivi chato itatoa ajira kama ambavyo hiyo pesa ingetumika kuwawezesha vijana kufanya shughuli za uzalishaji kwenye mashamba???
Kama nchi na serikali inayoongozwa na CCM na mwenyekiti na rais wa nchi Magufuli, tunakosea sana na tumekosea mno. Kuna mambo yanapswa kushauriwa kwenye uongozi huu na wawasikilize vzr sana washauri hawa. Ipo siku utatamani hawa vijana waongee kwa midomo au maandishi na wakati huo hautakuwepo tena. Tuwe tunajifunza vitu na historia.
Mheshimiwa rais ninakusihi kwa moyo mweupe kabisa angalia sera za serikali yako kwa vijana na masuala ya uchumi wa moja kwa moja. Kujenga reli ni sawa, kununua ndege ni jambo jema kabisa lakini hawana wananchi wako wamekta tamaa hawana matumaini tena.
Wasikilize na ikiwezekana kaa nao baadhi yao uwasikilize waulize waseme waziwazi kwako!!
 
Nimetafakari sana na kushindwa kumwelewa huyu rais wa awamu ya 5 ndugu Pombe Magufuli a.k.a Jiwe

Utawala huu unaonekana wazi hauna nia ya kuboresha Maisha ya vijana wa Nchi hii ambao ndio robo tatu ya watu wote ,ndio wapiga kura na ndio wachapa kazi wa Nchi hii

Vijana wa Tanzania tunakejeriwa,hatuthaminiwi,tunaitwa wavivu wapiga dili.

Vijana wametoka chuo wameshindwa kuajiriwa,sawa nafasi za ajira chache tuwezeshwe basi hata mitaji tukalime mchicha huko na nyanya,raisi hana muda anajali kujenga reli na kununua vipanga boi na terrible teen(Boeing dreamliner)

Vijana wa Nchi hii wamekosa dira,wamekosa malezi mema ya viongozi wao,hawajajengewa mazingira rafiki ya kujiajiri,wanaishia kusimangwa,kubaguliwa,kukejeliwa na kuonwa wavivu wakati nchi haijawaandalia msingi

Serikali ya awamu ya 5 ndo inaonekana kabisa haina time na vijana wa nchi hii,Leo hii vijana watanzania wamekua wakiishi Maisha ya kubahatisha,kijana ili ale inabidi akabeti,akacheze kamari kwenye mashine za wachina na hii inafanikiwa baada ya kupambana kupata mia 5 akafanye shughuli hiyo

Wanasiasa,viongozi wamewasahau vijana wa Nchi,wanawadharau,hawawathamini wanaowaona kama ni wajinga,wazembe,wavivu,tegemezi hawana manufaa kwa nchi yao

Leo vijana wengi wamekata tamaa kwenye nchi yao has a baada ya kuingia huu utawala wa awamu ya 5 chini ya Magufuli

Vijana hawajajengewa mazingira yoyote bora ya kuboresha Maisha yao leo lawama zote kwao,serikali inaona bora kuwekeza kwenye mambo yasiyomnufaisha mtanzania wa kawaida hasa kijana nguvu ya nchi hii wanadeal na vitu vinavyowanufaisha wachache akiwemo raisi na ukoo wake na wale wote wenye nazo

Vijana wa Tanzania wanaishi kwa kudra za Mungu waliowaamini kuwatengenezea mazingira mazuri kwao wamewasaliti,hawawajali,wanawadharau,kuwakejeli na kuona vijana hawa wanastahili tabu ,mateso na shida katika nchi yao.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki vijana wote wa taifa ili la Tanzania

Hapo juu kwenye reli na ndege. Naona vijana wengi wamapata ajira, hasa reli tu ni vijana wengi sana au wameajiriwa au fursa ya kujiajiri. Mfano hata mama lishe, madereva, mafundi, watoa elimu na wengineo wengi sana na wanazidi kuajiriwa kila kukicha.

Nalitetea hili ninalolifahamu la reli na ndege ambalo kweli watalii wameshaanza mumiminika.
 
pambana na hali yako hakuna wa kukupa msaada apaa.uncle magu kaza tena kaza sisi ma kada wako tunakusapoti kwa kilimo cha nyoka na njegere
 
Back
Top Bottom