Katika hali hii, ujasiri wa kusema awamu ya 6 iendelee 2025 wanautoa wapi?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,801
71,223
Hakuna umeme, Ugumu wa maisha, vijana hawana mategemeo ya future yao, Ubadhilifu na wizi serikalini na mashirika ya umma, na pamoja na yote hakuna kabisa kabisa ubunifu katika kuondoa mikwamo hiyo lakini ndio kwanza kelele za "mama anaupiga mwingi apewe mitano tena".

Katika hali kama hii, hao wanaopita huku na kule tena kabla ya wakati kumpigia kampeni ya uchaguzi 2025 UJASIRI huo wanautoa wapi ndani ya aibu kubwa namna hii katika utawala?

Tokea uhuru nadhani kila awamu ilikuwa na matatizo yake lakini sio siri hii imekuwa ya hovyo sana na haya madeni yanavyo ongezeka kauli ya Ndugai itakumbukwa siku moja.
 
Chawa wanalipwa ili kusema hivyo. Nasikia mpaka kwa siku yaani hamnahamna wanakunja laki.
Ambazo pia ni dalili za anguko hizo! If you are best kwa nini ulipe watu wakusifie?
Mama atunze heshima yake kwa kujipumzikia na mumewe na wajukuu, haya mengine yamemshinda! Period.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ili ujenge kaghorofa lazima uwe chawa , unadhani wataachaje kumsifia ?
Kuna mwenzao mmoja sijui nani huru msiba alisifia weeeee.mpaka akapitiliza. Na kweli vighorofa amejenga lakini akitembea hana amani. Hawezi hata kukaa sehemu na kunywa kabia kake kwa amani na utulivu
 
Watanzania wanajazana kwenye mikutano ya Makonda na kwenda kueleza shida zao, ikimaanisha bado wana imani na CCM
 
Watanzania wanajazana kwenye mikutano ya Makonda na kwenda kueleza shida zao, ikimaanisha bado wana imani na CCM
Sasa wanaenda watu 5000, wanasikilizwa wawili kuhusu ndoa zao, watatu madai ya pension, wawili viwanja na mtoto mmoja kutopata matunzo ya baba yake imeisha anaondoka na majukumu anapewa DED au Takukuru business as usually.
Hamjui watanzania wengi wanakuja kuona maofisa wa serikali wakiumbuliwa na kushangilia bila kujua hao wote lao ni moja tuu.
 
Kitu chochote kikiisha uwezo wake kina tabia yakujitutumua kionekane bado kinafaa.Sijasema tu mimi.
 
Back
Top Bottom