Mandingo
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 5,845
- 7,596
Amani ni agenda muhimu kwa kila Mtanzania, hususan vijana wenye ndoto za mafanikio. Bila amani, haiwezekani kufikia maendeleo ya kweli, iwe ni binafsi au ya taifa. Vijana hawawezi kutumia kikamilifu fursa zilizopo kama mazingira hayana utulivu. Hata mtu akiwa na mali nyingi, bila amani ndani ya nafsi na familia, mafanikio hayo yanakosa maana.