Vijana tuanzishe chama chetu cha siasa tujipiganie wenyewe

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,379
2,533
Habar wakuu,vijana nchi hii ni zaidi ya asilimia 60 hivyo kwenye taifa hili vijana tunanafasi kubwa sana ya kufanya maamuzi dhidi yetu kwa sasa vijana tumetupwa hakuna mikakati wala mipango yyte ya kuwainua vijana, vijana watz tumekosa wa kutusemea tumekuwa tunatumiwa na mamlaka pamoja na vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi yao.Nimefikiri kwa kina nikaona vijana tujipiganie wenyewe kwa kupitia chama cha siasa kianzishwe na vijana kwa lengo la kujipigania kwani kwa miaka mingi hakuna mtu mwenye uchungu na vijana nchi hii inakila kitu lakini vijana tumetupwa hakuna anayetuona.
Afrika kusini wameamua kufanya hivyo kupitia kwa kijana Julius Malema
 
Mkuu nakushauri utafute shamba ulime uza mazao upate kipato cha kuendesha maisha yako. Nchi hii ni ya chama kimoja (Nchi ya Kijamaa) na kitabaki kuwa kimoja tu. Hivi unavyoviona tumeweka kama magheresha ya kupatiwa misaada IMF na WB.
 
chama chenye maslahi mapana na vijana ni CCM, karibu mkuu CCM acha kupoteza kwa kuwaza visivyowezekana
 
Wazo zuri na lenye busara sana, watakao kupinga ni wale wasiokuwa na muelekeo, na ni wachumia tumbo.

Kabla ya chama kwanza vijana mgejenga muungano wa kiharakati wa vijana yuu, tena muwe na msimamo wa kupigania haki za watanzania bila kujali itikadi zao za siasa.

Kitu muhimu ni kupinga kuungwa mkono na chama chochote, na msionekane mkishirikiana na wanasiasa kwa jambo lolote lile. Wakimiunga mkono, wakataeni, kwani vyama vingine vitachukua fursa hiyo na kuonyesha kama mko upande wao.

Somo zuri ni wale vijana wa chuo kikuu walipoungana kupinga mauwaji ya aquiline , na juhudi zao zikatekwa na vyama vya upinzani na kuifanya ajenda yao.

Na pia muwe wakweli, linapofanywa jambo zuri mlisherekee na kuliunga mkono, baya lifanywapo mlikemee vikali lakini kwa lugha ya busara na itakayowavutuia wakubwa kwa wadogo.

Tafuta wenzako na mjitengenezee mitandao yenu pa kujumuika.
 
Habar wakuu,vijana nchi hii ni zaidi ya asilimia 60 hivyo kwenye taifa hili vijana tunanafasi kubwa sana ya kufanya maamuzi dhidi yetu kwa sasa vijana tumetupwa hakuna mikakati wala mipango yyte ya kuwainua vijana, vijana watz tumekosa wa kutusemea tumekuwa tunatumiwa na mamlaka pamoja na vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi yao.Nimefikiri kwa kina nikaona vijana tujipiganie wenyewe kwa kupitia chama cha siasa kianzishwe na vijana kwa lengo la kujipigania kwani kwa miaka mingi hakuna mtu mwenye uchungu na vijana nchi hii inakila kitu lakini vijana tumetupwa hakuna anayetuona.
Afrika kusini wameamua kufanya hivyo kupitia kwa kijana Julius Malema
Akili komavu kabisa hii
Maana dah
 
Back
Top Bottom