Vijana nyinyi ndio mabadiliko yenyewe

Vijana nyinyi ndio mabadiliko yenyewe

Amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana
Hizi takataka zako zimekuwa maudhi sasa.

Kumbe na wewe ni chizi namna hii?

Najuwa wewe ni mtu wa karibu sana na Genge la Samia; kwa hiyo uchizi huu ni matokeo y damu isiyo na kosa mliyoimwaga.
Mtachanganyikiwa sana katika maisha yenu yote yaliyobaki.
 
View attachment 3517134

My people,​

Utangulizi

Uhuru wa kutoa maoni na mawazo unaenda sambamba pamoja na kusikiliza maoni na mawazo ya watu wengine, si mwenye busara mwenye kutaka kusikilizwa tu, bali mwenye busara ni yule ambaye yupo open minded kusikiliza na upande wa pili hata kama ahafikiani na maoni na mawazo yao,na huo ndio ukomavu

Twende kazi..

Raisi Obama aliwahi kusema kwenye speech ambayo ilikuwa maarufu sana hapa duniani

"Mabadiliko hayatakuja kama tukisubiri mtu mwingine au wakati mwingine, bali sisi ndio mabadiliko yenyewe"

Vijana wa Tanzania nyinyi ndio mabadiliko yenyewe,msisubiri eti atakuja mtu kuwaambia kwamba Linda uhai wako kwa kuepuka fujo na vurugu,bali nyinyi ndio mseme sasa hatupo tayari kutumiwa tena kwa faida ya watu wengine

Nyinyi ndio wa kuamua kwa sauti kubwa kusema hatuwezi kuchoma nchi yetu Tanzania kwa maslahi ya watu wachache wenye malengo mahususi.

Ifike kipindi mseme inatosha sasa,hatuwezi kupoteza uhai wetu kwa mikakati ambayo haina tija,mikakati ambayo haina mwisho mwema,

Raisi wa Afrika Kusini bwana Nelson Mandela alisema hivi:

"Mabadiliko ya kweli hayafikiwi kwa chuki au kwa kulipa kisasi,ila kupitia kusameheana na kupitia mazungumzo"

Huyu ni mtu aliyefungwa miaka 27 jela kwa kupigania taifa la Afrika Kusini,baadae akaja kutolewa na kuwa raisi wa Nchi hiyo

Alikuwa na kila sababu ya kulipiza kisasi na kuwafunga watesi wake au kuwafukuza pale Afrika Kusini ndani ya masaa 24 tu. Lakini allichagua kusamehe na mazungumzo

Huu ni utajiri mkubwa wa nafsi yenye uelewa wa hali ya juu sana,ukomavu wa hali ya juu sana na roho yenye kusamehe

Tunatambua tumeumizwa sana na mioyo yetu inavuja damu,kutokana na madhila yaliyo wakumbuka ndugu zetu,lakini suluhisho sio kuandamana na kujawa na hasira na kuharibu mali na miundo mbinu,hio sia njia sahihi

Njia sahihi ni kupitia mazungumzo,njia ya mazungumo duniani kote ndio imekuwa mwarobaini wa changamoto nyingi sana,kwahiyo tuwe na subira kubwa wakati suluhu ya kuliponya taifa ikiwa katika pipeline

Tukumbuke nyinyi ndio mabadiliko yenyewe basi chagueni mabadiliko chanya

Ni hayo tu!
So kwa akili zako za kinyumbu kudai mabadiliko ni kukaa kimya wakati watu wanatekwa na kuuwawa, wakati uchaguzi unaporwa mchana kweupe, wakati familia za viongozi zinagawana vyeo, wakati rasilimali za nchi zinauzwa etc. Vijana tukae kimya kwamba tunalinda amani? CCM ndo culprit wa kwanza kupotea kwa amani nchini
 
Hakuna kijana anasubiri kuambiwa na ww au HAYA LAND HOV. Hakuna mazungumzo hayawajawahi kuombwa. Hadi uchaguzi tukaomba usogezwe mbele mkawa mnatuona wajinga. Katiba mpya mpaka ikawa wimbo, mkafikia hadi kusema kwa kejeli hadharani kuwa katiba haileti ugali mezani! Ni mazungumzo gani mnayataka sasa wakati hamko madarakani kwa ridhaa ya umma?
Hii movement haihusiani na serikali wala ccm, hayo maswali na maoni yangepaswa kupelekwa kwao

Sisi baada ya kuona madhara yaliyo patikana 29 Oct, tunaona si wakati tena wa vijana kutumiwa kwa njia ile ile iliyofeli hapo awali na ambayo inaweza leta athari zile zile
 
Nyinyi hampo kiulaumu serekali, ila mpo kuhakikisha serekali haihusishwi na mauaji na wizi wa kura. Sisi hatuchezi hiyo ligi yenu ya kikubwa maana inaweza kuwa ni ya makubwa jinga, sisi tunacheza ligi ya haki, haijalishi umri, mahali ama hali.
Hatupo hapa kwa niaba ya serikali,kwahiyo lawama za kutumia nguvu kubwa kwa waandamanaji serikali itakuja na majibu

Hivi turudie mara ngapi kusema kwamba sisi hatupo kwa niaba ya serikali

Tupo hapa kwa ajili ya vijana wa nchi hii wasitumiwe kupitisha ajenda za watu wengine kuichoma nchi hii
 
Chawa piga kimya. Ukiwa chawa post zako zinajionyesha tu.
 
You blame the victims instead of blaming the oppressors? Mlikuwa wapi kwenye utekaji? Kuiba kura? etc etc

You are ruining the future of all generations because of your selfishness.

Hizo buku saba zitawasibisha hadi lini. Even if you are given a ministerial job that money you steal or you get will not last a generation but that curse will live in your hearts until you die. Those are dead today, but for a purpose and are in heaven as heroes, but what about you? How will you die? Satanic
Tukuulize na wewe ulikuwa wapi kwenye utekaji na kuiba kura

Listen bro, utekaji sijui kuiba kura sio mission yetu now,lwasababu hatukuwa kwenye hizo mambo

Baada ya 29 Oct tukaona things are getting ugly , halafu wakati huo huo tukaona wanaharakati uchwara bado wana nia ile ile ya kuwafanya vijana wengine chambo tena

Tukaona hapana this time hatuwezi kukaa kimya we must do something against hawa watu wenye nia ovu ya kutuingiza kwenye machafuko kupitia maandamano

Kwahiyo msitupe lawama ambazo hazitustahili
 
Chawa piga kimya. Ukiwa chawa post zako zinajionyesha tu.
Unajua nini hamna hoja now tumewakalisha,ndio maana imebaki chawa chawa,mara tusisome post zao,mara tuwa ignore

Pinga hoja kwa hoja
 
Ujue mbogamboga ni wapumbavu sana, ukiwauliza nchi ilichomwa wapi watakwambia mabasi ya Esther 😃😃
Oh my GOD ndio uelewa ambao umeujua tunaposema kuchoma nchi

Kuchoma nchi hapa ni kuleta machafuko,vurugu,nchi isitawalike,amani itoweke,hapo ndio tunakisudia kuichoma nchi ndugu yangu
 
Mkuu umeremba shingapi huko lumumba maana hukuwa hivi wewe unaweza ikana hata Dini yako kisa buku saba.
Nikikwambia sijalipwa huwezi amini, tufanye nimelipwa itakuwa much better
 
Unajua nini hamna hoja now tumewakalisha,ndio maana imebaki chawa chawa,mara tusisome post zao,mara tuwa ignore

Pinga hoja kwa hoja
Mmmhhh, duuu basi mmepata mabwege kama wanawalipa kwa kuona mmekuja na bonge za hoja.
 
Hizi takataka zako zimekuwa maudhi sasa.

Kumbe na wewe ni chizi namna hii?

Najuwa wewe ni mtu wa karibu sana na Genge la Samia; kwa hiyo uchizi huu ni matokeo y damu isiyo na kosa mliyoimwaga.
Mtachanganyikiwa sana katika maisha yenu yote yaliyobaki.
Kalamu,

Trust me pamoja na kwamba huwa tunapigana spana hapa mimi na wewe,ila nakuheshimu sana, namna uavyojadiili huwa mara nyingi unaenda kwenye hoja

Sio chizi ila napush ajenda,unajua kwanini Coca-Cola imekuwa maarufu sana kuliko Pepsi, ni kwakuwa walipush matangazo mengi sana,na kawaida ukikiona kitu au kukisoma mara nyingi zaidi huwa kinakubadilisha au kukuathiri

Sasa nguvu mliyotumia kupush ajenda ya kutembea na viberiti,petrol na visu na mapanga,na kuchoma miundo mbinu mpaka ikawakaa vijana kichwani

Sasa tunatibu kwa kurewire ile damage mliyofanya,tunatibu kwa kurewire a new mantra amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana
 
So kwa akili zako za kinyumbu kudai mabadiliko ni kukaa kimya wakati watu wanatekwa na kuuwawa, wakati uchaguzi unaporwa mchana kweupe, wakati familia za viongozi zinagawana vyeo, wakati rasilimali za nchi zinauzwa etc. Vijana tukae kimya kwamba tunalinda amani? CCM ndo culprit wa kwanza kupotea kwa amani nchini
Wewe ulikuwa wapi wakati hayo yote yanatokea?

Ulifanya chochote??
 
Mmmhhh, duuu basi mmepata mabwege kama wanawalipa kwa kuona mmekuja na bonge za hoja.
Kwakuwa nyie watu wa vurugu na fujo mnalipwa kwahiyo unadhani kila mtu ana price tag kifuani kwake

Wengine hatuna bei tunafanya kwa kuwa tunaamini katika kuleta mabadiliko
 
Kalamu,

Trust me pamoja na kwamba huwa tunapigana spana hapa mimi na wewe,ila nakuheshimu sana, namna uavyojadiili huwa mara nyingi unaenda kwenye hoja

Sio chizi ila napush ajenda,unajua kwanini Coca-Cola imekuwa maarufu sana kuliko Pepsi, ni kwakuwa walipush matangazo mengi sana,na kawaida ukikiona kitu au kukisoma mara nyingi zaidi huwa kinakubadilisha au kukuathiri

Sasa nguvu mliyotumia kupush ajenda ya kutembea na viberiti,petrol na visu na mapanga,na kuchoma miundo mbinu mpaka ikawakaa vijana kichwani

Sasa tunatibu kwa kurewire ile damage mliyofanya,tunatibu kwa kurewire a new mantra amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana
Ajabu ya kusikitisha kabisa ni kulifanyia mzaha hili janga linaloikabili nchi yetu na kulijadili kama maswala ya hivyo vinywaji.
WaTanzania wanapoteza uhai wao kutafuta haki ndani ya nchi yao; leo wewe hapa unakuja na mzaha wa namna hii?

Wewe hapa unajuwa wazi husimamii "AMANI" hiyo ni njia ya ulaghai tu mnayotumia ambayo watu wamekwishajua maana yake ni nini hasa mnayoilenga.

Unalinda amani kwa kuua watu, ambao wewe mwenyewe ndiye uliyesababisha kwa kuwanyima haki ya kuchagua viongozi wao kwa haki na huru?

Unataka uambiwe matra ngapi ndiyo uelewe?

Lugha unayotumia ni ile ile anayotumia Samia na Genge lake lote, na BAKWATA. Nyinyi nyote vichwa vyenu vitakuwa vimeunganishwa kutojuwa kuwa AMANI hutokana na HAKI? Kama HAKI ipo, kuna sababu zipi za watu kupigania haki wanayopokonywa. Ni nani anayevuruga AMANI, kama siyo nyie mnaolazimisha mtawale waTanzania kwa nguvu, bila ya kuchaguliwa na hao mnaotaka kuwaongoza?

Haya yote unayajuwa, lakini unakomaa na hizi takataka za kuwauzia watu Coca Cola na Pepsi, huku mkiwaua!

Kawaida huwa nina mwisho wa subira. Sasa majibu yangu kwako na yenyewe yataendana na hivi vichekesho unavyoleta humu ili tucheke kwa waTanzania kunyimwa haki yao ya kuishi; ili Samia Suluhu hassan aendelee kubaki madarakani kutimiza ndoto zenu mnazolenga kwa kisingizio cha AMANI.
 
Kwakuwa nyie watu wa vurugu na fujo mnalipwa kwahiyo unadhani kila mtu ana price tag kifuani kwake

Wengine hatuna bei tunafanya kwa kuwa tunaamini katika kuleta mabadiliko
Uslamu ni dini ya haki
🤣🤣🤣🤣
 
Ajabu ya kusikitisha kabisa ni kulifanyia mzaha hili janga linaloikabili nchi yetu na kulijadili kama maswala ya hivyo vinywaji.
WaTanzania wanapoteza uhai wao kutafuta haki ndani ya nchi yao; leo wewe hapa unakuja na mzaha wa namna hii?

Wewe hapa unajuwa wazi husimamii "AMANI" hiyo ni njia ya ulaghai tu mnayotumia ambayo watu wamekwishajua maana yake ni nini hasa mnayoilenga.

Unalinda amani kwa kuua watu, ambao wewe mwenyewe ndiye uliyesababisha kwa kuwanyima haki ya kuchagua viongozi wao kwa haki na huru?

Unataka uambiwe matra ngapi ndiyo uelewe?

Lugha unayotumia ni ile ile anayotumia Samia na Genge lake lote, na BAKWATA. Nyinyi nyote vichwa vyenu vitakuwa vimeunganishwa kutojuwa kuwa AMANI hutokana na HAKI? Kama HAKI ipo, kuna sababu zipi za watu kupigania haki wanayopokonywa. Ni nani anayevuruga AMANI, kama siyo nyie mnaolazimisha mtawale waTanzania kwa nguvu, bila ya kuchaguliwa na hao mnaotaka kuwaongoza?

Haya yote unayajuwa, lakini unakomaa na hizi takataka za kuwauzia watu Coca Cola na Pepsi, huku mkiwaua!

Kawaida huwa nina mwisho wa subira. Sasa majibu yangu kwako na yenyewe yataendana na hivi vichekesho unavyoleta humu ili tucheke kwa waTanzania kunyimwa haki yao ya kuishi; ili Samia Suluhu hassan aendelee kubaki madarakani kutimiza ndoto zenu mnazolenga kwa kisingizio cha AMANI.
Excellent and well said
 
Halafu ni ajabu sana ujue,movement waliyofanya wao ya kuhamasisha vurugu,fujo na mambo kadha wa kadha wamesahau kwamba what goes around comes around

Sasa ni zamu yetu wapenda amani na utulivu wa nchi hii tunaonekana ni wabaya, inashangaza sana

Lakini hatutakatishwa tamaa kwakuwa ndani ya nafsi zetu tunajua tunapambania jambo sahihi,na siku zote mafanikio au njia ya mafanikio ina changamoto na mitihani mingi sana
Una mpambania nani wewe? [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom