ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Utangulizi
Uhuru wa kutoa maoni na mawazo unaenda sambamba pamoja na kusikiliza maoni na mawazo ya watu wengine, si mwenye busara mwenye kutaka kusikilizwa tu, bali mwenye busara ni yule ambaye yupo open minded kusikiliza na upande wa pili hata kama ahafikiani na maoni na mawazo yao,na huo ndio ukomavu
Twende kazi..
Rais Obama aliwahi kusema kwenye speech ambayo ilikuwa maarufu sana hapa duniani
"Mabadiliko hayatakuja kama tukisubiri mtu mwingine au wakati mwingine, bali sisi ndio mabadiliko yenyewe"
Vijana wa Tanzania nyinyi ndio mabadiliko yenyewe,msisubiri eti atakuja mtu kuwaambia kwamba Linda uhai wako kwa kuepuka fujo na vurugu, bali nyinyi ndio mseme sasa hatupo tayari kutumiwa tena kwa faida ya watu wengine
Nyinyi ndio wa kuamua kwa sauti kubwa kusema hatuwezi kuchoma nchi yetu Tanzania kwa maslahi ya watu wachache wenye malengo mahususi.
Ifike kipindi mseme inatosha sasa, hatuwezi kupoteza uhai wetu kwa mikakati ambayo haina tija,mikakati ambayo haina mwisho mwema,
Raisi wa Afrika Kusini bwana Nelson Mandela alisema hivi:
"Mabadiliko ya kweli hayafikiwi kwa chuki au kwa kulipa kisasi,ila kupitia kusameheana na kupitia mazungumzo"
Huyu ni mtu aliyefungwa miaka 27 jela kwa kupigania taifa la Afrika Kusini,baadae akaja kutolewa na kuwa raisi wa Nchi hiyo
Alikuwa na kila sababu ya kulipiza kisasi na kuwafunga watesi wake au kuwafukuza pale Afrika Kusini ndani ya masaa 24 tu. Lakini allichagua kusamehe na mazungumzo
Huu ni utajiri mkubwa wa nafsi yenye uelewa wa hali ya juu sana,ukomavu wa hali ya juu sana na roho yenye kusamehe
Tunatambua tumeumizwa sana na mioyo yetu inavuja damu,kutokana na madhila yaliyo wakumbuka ndugu zetu,lakini suluhisho sio kuandamana na kujawa na hasira na kuharibu mali na miundo mbinu,hio sia njia sahihi
Njia sahihi ni kupitia mazungumzo,njia ya mazungumo duniani kote ndio imekuwa mwarobaini wa changamoto nyingi sana,kwahiyo tuwe na subira kubwa wakati suluhu ya kuliponya taifa ikiwa katika pipeline
Tukumbuke nyinyi ndio mabadiliko yenyewe basi chagueni mabadiliko chanya
Ni hayo tu!