Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 11,084
- 12,329
Mambo vipi kijana mwenzangu? (hata usio kijana) naona uko poa na unaendelea kulibandika viraka taifa letu pendwa. Leo mwenzako kuna jambo nime liona ktk jamii yetu inayo tuzunguka, ambalo sipendezwi nalo. Kuna tabia ya vijana kutumia misamiati au majina ya vitu husika sehem zisizo husika. Tabia ambayo naona inazidi kuota mizizi na kuichafua Lugha yetu ya Kiswahili. Huwa sipendi ninapo sikia mtu anapo litumia neno "jembe" kwakumuita mwenzie. Hivii jina hili ni sahihi kuitana sisi vija? Binafsi mimi mtu wa pwani unapo niita "jembe" nalitafsiri jembe kama jembe. Jembe ninini? Jembe ni chombo kinacho rahisisha kazi za mikono ktk kulima, kukat etc. Pia jembe lina kitobo kwa nyuma kitobo ambacho hudumbukizwa kipande cha mti ili lifanye kazi ( kulima) kwahiyo kumuita mwenzio "jembe" nisawa na kumuita mwenzio ni chombo kinacho tiwa kitu kwa nyuma sawatu na kumuita SHOGA ila wenyewe hatu jui. Chengine, kuna msanii wa muziki wa kizazi kipya anae jiita "Mnyama" huwa nnashangaa kweli! Aliwaza nini mpaka kufikia uwamuzi wa kujiita "Mnyama", amesababisha mpaka watoto wetu mitaani wanaitana "Mnyama" ivi kweli binaadamu unajisikia faraja mwanao anapo itwa "Mnyama" mbeleyako? Kwakweli ina udhi kama si kukera. Nakumbuka mwaka m-moja nili nusurika kulamba makofi, baada ya kumuita mzee flani hivi hapa mtaani kwetu, nakumbuka nilimuita "Mdingi" dah! Sinto sahau mzee aliamaki sana karibu ya kutokwa na povu. Bahati mzuli alitokea mama m-moja anae nifaham vizuli (kitabia) akaniombea msamaha, mama yule namkumbuka kwa heri kwanza alini nusuru nisipigwe, pili alini fanya nijue madhara ya kutumia misemo ya hovyo, nashukuru mpakaleo situmii Lugha chafuzi kama hizi.(nikikutajia maana ya "Mdingi" hutakaa umuite tena babayako jina hilo) Nakuomba kijana mwenzangu usitumie misamiati vibaya kwakisingizio cha kurembesha Lugha yako. Mbona ukinyoosha ina pendeza tu. NIHAYO TU
