Vijana muogopeni Mungu, la sivyo mtaishia jehanam

Jun 17, 2020
75
268
Asilimia kubwa ya idadi ya watu duniani ni size ya kati ya miaka 14-55 ambao wengi ni Vijana! Hiki ni kizazi kilichotabiriwa kizazi cha nyoka ambacho hakitataka kuyasikiliza maneno ya Mungu! Ni kizazi ambacho haya ndo kinachoyafurahia.

1: Kumiliki pesa nyingi ambazo sio za jasho!
2: Kupenda starehe na anasa kuliko kumpenda Mungu na kufanya Kazi
3: Kuajiriwa sehemu nzuri ya kupiga pesa za udhalimu, na ukifanya hivyo na hata kujenga na kufanikiwa familia na watu wa karibu wanakusifu na kukupa heshima na kukuita kuwa ww ni Mtu wa Maendeleo au mjanja kumbe moyoni unajua ww ni mwizi
4: Kumiliki pesa, majumba, viwanja ni ufari kumbe ufahari kumjua Mungu wa kweli na kuridhika na ulichonacho
5: Vijana wapo tiyari kumwaga damu ili wapate utajiri
6: Kufunjika ndoa, usaliti kwenye ndoa ni jambo la kawaida
7: Vijana hawataki kuoa, na kuolewa kukwepa majukumu na wakati huohuo wanafanya uasherati usiku na mchana
8: Ni kizazi ambacho michepuko kwenye ndoa ni jambo la kawaida
9: Kizazi kimeukana uumbaji wa Mungu, kimefuata mafundisho ya shetani, kinaamini kwenye ukisasa, kujichubua, kujichora mwilini, lipstick, nywele bandia, mitindo ya kunyoa ya kipepo, wanawake kuvaa suruali, ole wao!
8: Vijana hawana muda wa kumtafuta Mungu, muda wao mwingi, ni mitandaoni, kuangalia movie, Mpira,na kubeti
9: Kizazi ambacho hawataki kuwaadhibu watoto badala yake ni katooni za kipepo ndo malezi ya watoto
11: Kizazi kinachoamini kwenye miujiza ya akina mwaposa, geodavo, mzee wa upako wala sio mafundisho ya uzima ya akinia kakobe, mbarikiwa mwakipesile, ni
12: Kizazi kisichoogopa dhambi kinaogopa mimba na ukimwi
13: Kizazi kisichotangaza madhara ya uasherati au uzinzi badala yake kinatangaza watu kujikinga na magonjwa na mimba!
14: Kizazi ambacho ukioa unaonekana huna maana mbele ya Vijana ulitakiwa uendelee kula ujana( dhambi)
15: Kizazi ambacho wacheza uchi majukwaani ndo wanataka kwenda bungeni kutunga sheria za kuongoza nchi
16: Kizazi ambacho ukitenda haki au kusema ukweli unachukiwa!

Note: Moto wa jehannum upo na mbingu IPO! Ubishe au ukubali, yapo maisha baada ya kifo! Maisha ya umelele jehannum ya moto au mbinguni unayatengeneza ww mwenyewe! Kizazi hiki kikaidi kinachoamini kwenye Elimu, ole! Ole! Ole! Ole! Yesu anarudi kuchukua kanisa!

Mpe Yesu maisha yako! Hiyo Elimu yako unayojifunia, cheo chako, umaarufu wako, pesa yako! Ipo siku utaviacha hivyo vyote na tutakuzika kama wengine! Utakuwa wapi jiulize ww mwanadamu uliye mavumbi! Udogo tu! Hicho kiburi chako kitaisha siku hiyo!
 
Huyo Mungu ushawahi kumwona au umekaririshwa story tu
Inawezekana ww hujawahi kumuona na kwako ikawa ni stori na mambo ya kutungwa

Lakini mtu kama mimi najua sana umuhimu wa MUNGU sio kwa sababu ya stori na kuhamasishwa ila ni kwasababu ya badiliko la kweli kwenye maisha yangu
Nikitazama nyuma kabla ya MUNGU na baada ya MUNGU naona vitu viwili tofauti na naweza kusema yajayo yanafurahisha zaidi kuliko yaliyopo sasa

Wewe endelea kuto kuamini ni vyema kabisa kwa mtazamo wako ila kwa watu kama sisi ata uweke nini sio rahisi kumuamcha MUNGU kuna wakati tulipita hakuna wala mzazi angeweza kututoa lakini MUNGU alitutoa alafu wewe from nowhere unasema MUNGU hayupo tunacheka tu nakuzidi kukaza buti maana yajayo ni matamu zaidi ya haya ya sasa
 
Umesahau hayo yote yanatokana na mahangaiko ya kidunia mkuu.
Huna hela hata ya chakula,
Nguo tangu ununue ulivyozioteaga,
Huna nyumba na ulikopanga Kodi imeisha una miezi mitatu afu huelewi 🤣🤣,
Mkeo anakudharau kutokana na ufukara sugu uoonao,
Ndugu hata simu hawakupigii , wakipiga unaitwa kikao cha masuruhisho,

Kwa maisha Kama hayo , utapata furaha na huyo Mungu saa ngapi! ?
 
Inawezekana ww hujawahi kumuona na kwako ikawa ni stori na mambo ya kutungwa

Lakini mtu kama mimi najua sana umuhimu wa MUNGU sio kwa sababu ya stori na kuhamasishwa ila ni kwasababu ya badiliko la kweli kwenye maisha yangu
Nikitazama nyuma kabla ya MUNGU na baada ya MUNGU naona vitu viwili tofauti na naweza kusema yajayo yanafurahisha zaidi kuliko yaliyopo sasa

Wewe endelea kuto kuamini ni vyema kabisa kwa mtazamo wako ila kwa watu kama sisi ata uweke nini sio rahisi kumuamcha MUNGU kuna wakati tulipita hakuna wala mzazi angeweza kututoa lakini MUNGU alitutoa alafu wewe from nowhere unasema MUNGU hayupo tunacheka tu nakuzidi kukaza buti maana yajayo ni matamu zaidi ya haya ya sasa
Amina, wengi tunakiri uwepo wa Mungu kutokana na uhalisia wa mambo aliyotufanyia SIO kwasababu ya story au kwasababu ya kuaminishwa NO.
 
Watu wengi wanaodai wameokoka ndiyo wenye hizi sifa zote ulizotaja.

Siku hizi ulokole ni kutengeneza picha nzuri mbele ya jamii kuwa ni mcha Mungu halafu ujitahidi mambo yako mengi uyafanye gizani yasijulikane.

Wengine wameenda mbali zaidi wanafanya mambo ya ajabu hadharani wakiulizwa wanakwambia kuokoka siyo kimwili ni kiroho ili mradi mimi najua mahusiano yangu na Mungu wangu.

Unajiuliza hivi kilichoko ndani mwako si kitajidhihirisha nje kupitia matendo yako?
 
Umesahau hayo yote yanatokana na mahangaiko ya kidunia mkuu.
Huna hela hata ya chakula,
Nguo tangu ununue ulivyozioteaga,
Huna nyumba na ulikopanga Kodi imeisha una miezi mitatu afu huelewi 🤣🤣,
Mkeo anakudharau kutokana na ufukara sugu uoonao,
Ndugu hata simu hawakupigii , wakipiga unaitwa kikao cha masuruhisho,

Kwa maisha Kama hayo , utapata furaha na huyo Mungu saa ngapi! ?
Tatizo Sio pesa peke yake ndugu.
Kuamka ukiwa mzima wewe unamlipa nini Mungu? Ukiwa mwenye shukrani kwenye mambo ambayo wengi wanaona ni madogo hata Mungu mwenyewe atatuinua na kukufungulia milango ya baraka zaidi
 
mkuu enzi za Nuhu kulikua na mabaya kuliko haya uliyoorodhesha hapo!......


Sodoma na gomora zilitisha mno kwa kufuru mpk kutaka 'kuwapiga' malaika.........


btw, hakuna jipya chini ya jua....... huu unaouita uasi ulikuepo, upo na utaendelea kuwepo mpk mwisho wa dunia!


.........JESUS CHRIST IS THE LORD.......
 
Neno la Mungu Lazima Litimie.

2 Timotheo 3:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Timotheo 3:2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
2 Timotheo 3:3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
2 Timotheo 3:4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
2 Timotheo 3:5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
2 Timotheo 3:6 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
2 Timotheo 3:7 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
2 Timotheo 3:8 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
2 Timotheo 3:9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
 
Back
Top Bottom