Vijana msipoteze muda kwenye project zenu za kiteknolojia

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,554
2,000
Kuna wimbi kubwa la vijana wanahangaika ni kudevelope ma idea ya project kubwa kubwa za kidigitali na ki technolojia mfano.

1. Sijui app ya alarm sjui ya nyumbani ukiwa kazini mtu akifungua mlango unapata notification.

2. Mara program ya visima vya maji umwagiliaji.

3. Mara program ya nini sijui etc etc etc

Vijana wenzangu hizi technolojia na the likes kwa nchi kama yetu hii utasubiri sana kwa mwekezaji kuweka hela... vijana wengi mnajikita kwenye biashara ngumu ngumu kiukweli niwambie hizo hazina helaaaa. Africa bado sana

Jikiteni kwenye mambo ya kawaida tu...usiumize kichwa snaa .. we unamwona Bakheresa au mo biashara zao... wanauza viberiti, unga, juice etc

Nenda Kariakoo uone matajiri wafanyabiashara wanafanya nini wanauza vitu vya kawaida kabisa.

Kilimo etc etc.... buy and sell vitu rahisi rahisi tu ... sasa mtu unahangaika weee... daah.

Kilichofanya niandike uzi ni kwamba nina ndugu yangu anamaliza chuo... nimemwambia anipe mchanganuo wa biashara nimpe mtaji yaani unaenda mwezi wa sita huu ananipa michanganuo ya ajabu ajabu hadi nauliza amerogwa nini.
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,094
2,000
Usiwakatishe tamaa wenzio tunazinunua hizo app mi nina app ya kufungua geti na nimemuunga dogo na wateja wengine kumi anapiga hela.

Tengeneza app ya kumwagilia mpunga, tafuta soko kwa wakulima wa mpunga take trouble piga hela nunua gari honga uza app nyingine tena circle iendelee maisha yaende
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,208
2,000
Hata kwenye app Usifanye mambo magumu kama kufungua geti sijui kilimo app... fanya app zinazoruhusu watu wa enjoy maisha na wafanye upuuzi.. uone utavyopata watu wengi

Mfano app ya Tik tok ni upuuzi tu.. wanawake wanavyopenda upuuzi wameipokea kwa mikono miwili na imekuwa ndio app inayoongoza kwa profit dunia nzima.. na value yake inapanda kila siku
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,554
2,000
usiwakatishe tamaa wenzio tunazinunua hizo app mi nina app ya kufungua geti na nimemuunga dogo na wateja wengine kumi anapiga hela.

Tengeneza app ya kumwagilia mpunga, tafuta soko kwa wakulima wa mpunga take trouble piga hela nunua gari honga uza app nyingine tena circle iendelee maisha yaende
Mnanunua wangap hzo app mjomba mbona unataka mchelewesha ndugu yako.atatoboa ndio ila kwa tabu sanaaa
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,554
2,000
Hata kwenye app Usifanye mambo magumu kama kufungua geti sijui kilimo app... fanya app zinazoruhusu watu wa enjoy maisha na wafanye upuuzi.. uone utavyopata watu wengi

Mfano app ya Tik tok ni upuuzi tu.. wanawake wanavyopenda upuuzi wameipokea kwa mikono miwili na imekuwa ndio app inayoongoza kwa profit dunia nzima.. na value yake inapanda kila siku
Sasa ndugu zako na bachelor zao app zao unaweza sema hii itanipeleka sayar ya mars..ma app magum magum
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,554
2,000
Acha kuwakatisha tamaa wenzako. Tena ninawaasa wabunifu wa mifumo ya kiteknolojia hakikisheni mnasajiri kazi zenu COSOTA hakika hamtajutia. Kwa leo au kesho inaweza kuonekana mnapoteza muda ila nakuambieni technology ni pesa
Wadanganye wenzio tu...mchina keshamaliza hzo tech zote tena kwa cheap manufacturing.hakuna jipya..waingize chaka wenzio..wakinga na wachaga wanatajirika kwa kuuza mchele tu
 
andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,234
2,000
Kuna wimbi kubwa la vijana wanahangaika ni kudevelope ma idea ya project kubwa kubwa za kidigitali na ki technolojia mfano.

1. Sijui app ya alarm sjui ya nyumbani ukiwa kazini mtu akifungua mlango unapata notification.

2. Mara program ya visima vya maji umwagiliaji.

3. Mara program ya nin sjui etc etc etc

Vijana wenzangu hiz technolojia na the likes kwa nchi kama yetu hii utasubir sana kwa mwekezaj kuweka hela..vijana weng mnajikita kwenye biashara ngum ngum.kiukwel niwambie hizo hazina helaaaa..africa bado sana

Jikiten kwenye mambo ya kawaida tuu..usiumize kichwa snaa ..we unamwona bakheresa au mo biashara zao...wanauza viberiti, unga, juice etc

Nenda Kariakoo uone matajiri wafanyabiashara wanafanya nini wanauza vitu vya kawaida kabisa.

Kilimo.etc etc....buy and sell vitu rahisi rahisi tuu ..sasa mtu unahangaika weee..daah.

Kilichofanya niandike uzi ni kwamba nina ndugu yangu anamaliza chuo..nimemwambia anipe mchanganuo wa biashara nimpe mtaji yaani unaenda mwez wa sita huu ananipa michanganuo ya ajabu ajabu hadi nauliza amerogwa nini.
Mkuu tatizo sio ndugu yako tatizo ni wewe,Kwanza kabisa wabongo wengi katika swala la miradi ya teknolojia hawako disruptive zaidi wanafanya copy pasting,wanatengeneza solution ambazo tayari ziko sokoni wanasema wametengeneza kitu kipya na kinaposhindwa kushindana inakuwa tatizo.

Project za teknolojia zinapaswa kufanyika kama hoby zaidi na sionjia ya kupata bingo.Ila usiseme waachane nazo hapana bali wafikirie katika namna ya kutengeneza pesa.Waangalia Changamoto zilizopo katika mazingira yetu kisha walete disruptive technlogy kama hawatamake.Lazima wajifunze kufikiria nje ya BOX ila teknoljia bado inalipa we unaona ngumu kwa sababu sio fani yako.
 
kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,697
2,000
Usiwakatishe tamaa wenzio tunazinunua hizo app mi nina app ya kufungua geti na nimemuunga dogo na wateja wengine kumi anapiga hela.

Tengeneza app ya kumwagilia mpunga, tafuta soko kwa wakulima wa mpunga take trouble piga hela nunua gari honga uza app nyingine tena circle iendelee maisha yaende
Mleta mada kaleta mada pana. Maendeleo ktk nchi zetu bado sana. Kubuni app na mengineyo ya aina hiyo yanaweza vusha watu wa kuhesabu.

Lakini shughuli za kawaida eg biashara, kilimo, ufugaji nk inatoa ajira kwa wengi na soko ni kubwa. Binafsi natafuta ajira, lakini ufugaji wa kuku na bata ninao endelea nao wateja wa mayai asili ( Malawi, croiller na kienyeji wanalisha nje ndani ya fance kubwa) nashindwa kuwatosheleza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom