Vijana msilale bado mapambano

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Vijana ndio taifa. Vijana msinung'unike hata chembe. Msikatishwe tamaa na mapito ya dunia hii kila jambo huwa lina wakati wake.

Wapo vijana wasomi waliokosa ajira sababu ya siasa mpaka kufikia hatua kuhisi wana mikosi, wengine kwenda mbali zaidi mpaka kuhisi wamerogwa. Na hii yote sababu ya kukosa ajira kutokana na matumaini waliokuwa nayo.

Msipende kwenda kwa waganga au viongozi wa dini uchwara msije danganyika. Ni kweli inauma sana mtu au kikundi cha watu wachache wawe waamuzi wa kesho yako kwa kukutaka ufanye usichostahili; jitenge nao kisha kaa kimya tu isiwe sababu ya wewe kukata tamaa kijana.

Kumbuka kesho iliyo tamu ndiyo chungu ya leo. Usikate tamaa bado mapambano. Omba sana Mungu atakusikia kijana, usiamini siasa na watu wake maana Mungu hufanya njia pasipo njia, amini hilo.

Hata kama biashara unazojaribu kuzifanya zinakufa, kilimo unacholima kinashindwa au chochote unachokifanya kama hakiendi, usikate tamaa kijana. Ndio taifa, na nchi ukumbuke ndiyo inayokutegemea. Kumbuka bado mapambano.

Jipeni moyo wao wana familia chache wataisha siku moja na nyinyi mkumbuke mnafamilia za mitara mtafaidi siku za mbeleni. Gari moshi lazima litarudi mbele nyuma tena.

Karibu parapanda.
 
Umeandika vizuri.
Inatia moyo, faraja na matumaini.

Lakini vipi pale vijana na jamii wanapohitaji kupambania kilicho chao?

Nauliza kwa maana ideology zipo nyingi, kuna wale ambao ni internals. Hawa wanaamini ni lazima ujifunze kujinyakulia kilicho chako na siyo kusubiri mtu aje akupe au akutengenezee mazingira ya kukipata.

Na kwa mantiki yako hii naona kama hutoi nafasi ya kumhukumu aliyekudhurumu au kukukosesha kilicho stahili yako. Bali kuwa mvumilivu kungoja wakati utende kazi yake na zama zipite.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakati ni hakimu mzuri.si kila haki imewekwa kwa ajiri yako.waweza dai ila ukihisi kupata madhara angalia mambo mengine.achana na neno sikubali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom