Ndugu wanajamii, siku mbili zilizopita hivi nilishuhudia kikundi cha vijana eneo la Tabata Relini - Dar es Salaam - (walikuwa wanatokea direction ya Tabata Kisiwani wakakatiza Barabara ya Mandela na kuelekea kama wanaenda Ubungo Maziwa - yaani sambamba na reli). Walikuwa wakiimba na kupiga ngoma. Mwanzoni nilidhani ni mashabiki wa mpira, lakini nilishangazwa kusikia wakiimba matusi ya nguoni. Hata wafanyabiashara waliosikia maneno ya wimbo wao walisikitika sana kuona kuwa vijana wamefikia hatua kama hiyo. Jana nilikuwa naongea na wife na yeye akasema alikuwa Mbagala Kijichi jana yake na alipokuwa akirudi asubuhi alikutana na kundi la vijana waliokuwa wakikimbia mchakamchaka na kuimba nyimbo za matusi. Kwa vile ni mara ya kwanza kushuhudia haya nimeona ni kitu cha ajabu! Inawezekana yameshakuwa mazoea sehemu nyingine. Je, hata maeneo mengine mambo ni hivi?