Vijana jifunzeni programming you wont regret it

Mimi nimesoma HTML na CSS kupitia TheNewboston, code academy na Youtube. Nimesoma pia Udemy.com. Kimsingi, nimepata msingi wa web development kwa kuanzia na HTML na Css. Ninapenda sana programming. Hii ni moja ya skills ambazo nitapenda pia watoto wangu wawe nayo bila kukali wanachojifunza. Sijawa mzuri sana. Ninaendelea kujifunza. Nimefurahi kuipata free code camp. Ninaendelea kupiga msuli. Kila la kheri coders
 
mkuu endeleza mada basi
nimesoma highlights za coding kidogo baada ya kupita hapa
 
niko mbioni kuregister NGO itakuwa inafanya kazi kama TANZANIA HOUSE OF TALENT
but ya kwangu ni AFRO CODER CAMP

to empower young african talents develop coding skills
Involve me as well ukishafanikiwa kuregister pls.
 
Ni kweli ila inawezekana ukikusudia

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]
 
Duh! Ujifunzie tuu mtandao bila kwenda shule? Labda Html, lakini kwa Php,Javascript,C++,visual Basic.. tuache utani mimi nmesoma haya mambo ni magumu balaa yanahotaj muda wa kufundshwa pia kufanya kigroup zaidi

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
hapa wewe mwenyewe ujachangia umefanya yale yale uwezi kuchangia jambo ambalo una uelewa nalo hapa umefanya kujibu swali ambalo ujaulizwa.
 

unaweza kuwa partly right na partly wrong!
Sio wote hapa wenye interest kujifunza kupitia mitandaoni wataweza,wengi wataishia njiani maana watakua wanataka output mapema sana na wengine discipline ya kujisomea na kufanya mazoezi watakosa na hawa ndo wanaitaji kwenda shule kujifunza programming ila wapo wachache sana ndo wataweza kwa hiyo njia ya kujifunza mtandaoni kulingana na discpline yao!

Wengi pia wanaitaji mtu wa kuwa mentor maana utakuta wengi wataishia kuruka ruka hapa na pale lugha moja kwenda nyingine na mwishoni hawatakua na kitu wanajua cha kuweza ku solve matatizo kwa code!

Na kwenda chuo sio guarantee ya kuwa programmer wapo watu tunaowajua pengine classmates wana formal education ya hizo lugha ila hawajui hata wayatumie vipi maarifa yao na pengine waliona ni uzushi hawako interested kabisa ukimwambia aandike hata mistari kadhaa ya code hatoweza au kashasahau kabisa!

mwisho, kuna kitu ambacho nimeona kwako kimenisikitisha kama ulisoma hizo lugha kwa formal education na bado unaamnini mtu hawezi jifunza PHP mtandaoni kwa kusikiliza tuts basi unaitaji maombezi!

Usiwakatishe tamaa wenye nia japo na mm naamini sio wote wataweza maana sio rahisi kwa mtu ambae hana Juhudi
 
Kila mtu na mtazamo wake, sijasema kuwa siwez php.. mimi natengneza web Dynamic kwa php+html+css, nmewazungumzia wanaosoma mtandaoni.. hata kama najua lakin najua ugumu wake... sasa wew unanizarau kua nahitaj maomb.. kwanini huwez kuheshimu mawazo ya mtu?

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu nataka kujifunza sana ila nilijaribu nikashidwa sababu sina background nzuri ya ya masomo ya science..kila kitu niliona kipya..
Ila nampango wa kuingia darasani full..only for programming..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kwanza,hapo kwenye Bold,sijaandika popote maneno hayo ni wewe ume misinterpret.

Pili, Naheshimu mawazo yako ndo maana nikasema Uko sahihi kwa upande mmoja(partlty right) na hauko sahihi upande mwingine(partly wrong) lakini na wewe inabidi kuheshimu mawazo ya wengine kwenye forums maana tukisema tusijadili comment yako sijui kama forums zitakua na maana tena.
sentensi yako ulivoiweka ndo imenishangaza maana mimi nilitegemea useme PHP ndo lugha rahisi kwa watu kuanzia upande wa web development kwa urahisi wake sio tu wa kujifunza bali mpaka ku deploy project online ukilinganisha na lugha nyingine.

Kwa mtu kama wewe(mwenye formal education ya CS) nilitegemea uje na Guide kwa juniors wako na changamoto ulizokutana nazo na ulivoziepuka ila kinyume na matarajio yangu umekuja kivingine(kama kuwa discourage watu) pia hii inaweza kuwa hata opportunity kwako kuwa mentor watu hata kwa malipo kidogo ndo maana nkasema unaitaji maombi maana sikutegemea hiyo kauli kwa mtu kama wewe.

Lugha zote zinaweza kuwa ngumu ila Ugumu unaweza kutofautiana kulingana na learning curve na pia hata kulingana na level ya Project unayofanya au hata kuchagua lugha au Framework au Library ya lugha ambayo sio nzuri kwa project yako.

Vyuo vyenyewe havifundishi hata zile Top 10 programming languages kama sikosei, nimepitia baadhi ya prospectus za vyuo vingi unakuta ni C,Java,Visual Basic,PHP ambazo goal nafikiri nikumpatia mtu msingi na hii haimaanishi mtu hawezi jifunza Kotlin for android na akaichagua kuwa lugha yake kukamilisha projects zake au hii haimaanishi mtu hawezi jifunza Python na web frameworks zake kama Django au Flask kufanya web porjects zake.

All in all lazima uwe na maneno ya ku encourage watu,yes we know science haijawai kuwa rahisi ila wenye uwezo,juhudi na nidhamu watatoboa!
 
Basi tuishie hapo.

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…